Baada ya TCRA kuzuia local channels, Chaneli za Kigeni zinazotumia Kiswahili zashika usukani. Kenya yatawala soko

Baada ya TCRA kuzuia local channels, Chaneli za Kigeni zinazotumia Kiswahili zashika usukani. Kenya yatawala soko

mkuu una idadi ya watanzania wanaoangalia channels za nje vs TBC
tafiti hupingwa kwa tafiti mpya , 98% ya watanzania hawatazami TBC , hao 2% wanaoifuatilia ni wafanyakazi na hasa walimu wanaofuatilia nyongeza ya mishahara kama itatangazwa siku moja
 
Nimeshangaa jana mda fulani nimewasha king'amuzi cha Azam channel za ndani zilikua zinaonyesha lkn baada ya mda zikakata tena
 
Sifahamu aliyewashauri TCRA kutenda waliyoyafanya , kama ni mkono wa mtu basi kafanikiwa na hongera zake , Kiukweli pamoja na ving'amuzi vingi kubaki na TBC pekee watanzania hawataki kabisa kuangalia Channel hii , na kwa uchunguzi wangu wa valuvalu nilioufanya unaonyesha kwamba ukitaka taarifa zako zisiwafikie walengwa basi tangaza TBC 1 , bado sijafahamu hasa kisa cha watanzania kuisusia TV hii inayoendeshwa kwa kodi zao.

Lakini cha ajabu sasa Channel za Kiswahili kutoka Nairobi zikiwemo K24 , KBC , KTN NEWS zikiongozwa na KTN ndio zinazotazamwa mno na watanzania hasa wanaotumia AZAM na DSTV channels zenye watazamaji lukuki nchini Tanzania

Nachukua nafasi hii kuwashauri wafanyabiashara wenzangu kujaribu kutangaza bidhaa zao na Channels kutoka Kenya maana ndio zinazobamba hasa nchiniTanzania .
Ktk hili ni kana kwamba unawalaumu TCRA, binafsi siamini kama ni kosa ktk kusimamia kweli, kama wahusika walipaswa kuonyesha chaneli husika bure ila walikuwa wakitutoza fedha kwa kipindi chote hicho, sidhani kama kuna kosa limefanywa na Serikali ktk kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma inaendelea kufanywa kwa wananchi wake. Siamini kwamba kila linalofanywa na Serikali kwamba ni jambo baya, mazuri tusifie, mabaya tukosoe na KUONYESHA NAMNA BORA YA KUYASHUGHULIKIA. Tutoe solutions kwa yake tunayoonza utatuzi wake una changamoto, tusiishie kulaumu pekee!
 
Nadhani ni kampeni za CCM tusipate habari kwa uhuru tubaki TBC.
Mbona DSTV waliambiwa wasionyeshe local channels ila TBC tuu.
Tumeminywa tusione news hata kwenye blogs.
Huo ni udekteita kama China na Urusi etc.
News napata BUKEDE UG.
 
Sasa kama hizo chanels zitatazamwa bure kulipia, hivi kuna sababu gani mtazamaji kulipia kifurushi, na makampuni yatapataje faida kibiashara… ruhusu watu wafanye biashara na sio kulazimisha bure…. TBC ndio halali ya mlipa kodi.
Makubaliano yalikuwa wanabadilisha analojia kuja dijitali bila gharama za ziada kwa mwananchi, sasa hata ukisaidiwa unaponda mkuu wewe hv ni mkenya au mtanzania
 
Bora wamezitoa hizo local chanel mana kama wangezifanya zote ziwe za bure tusingelipia ving'amuzi maisha yote 😂
 
Tatizo wabongo wengi mkono wa birika,mkipewe chaneli tano bure ndiyo hamlipi tena! Ndiyo maana jamaa nao wakabana ili mlipe!
Ishu sio wabongo, ishu ni kuwa makubaliano yapo hivyo, stesheni zetu za ndani ziendelee kuwa free, maana tangu mwaka 2002 huko Dstv ilikuwepo fresh na hakukuwa na tatizo, ila tulivyohamia dijitali makubaliano ndo yalikuwa kile kilichokuwa kinahitajika ni kununua kisimbusi tu kwa anayetaka channel za ndani awe anaangalia fresh free, anayetaka za ziada alipie gharama, sasa kipya kipi hapo mkuu, wewe unapenda tu kuropoka hasira zako bila kujua unataka kumuumiza mwananchi mwenzio ambaye anapenda aangalie channel zake for free km alivyozoea, kuwa mzalendo ndugu.
 
tafiti hupingwa kwa tafiti mpya , 98% ya watanzania hawatazami TBC , hao 2% wanaoifuatilia ni wafanyakazi na hasa walimu wanaofuatilia nyongeza ya mishahara kama itatangazwa siku moja
Mawazo yako tu, sio kila anayelalamika akifika kwake haangalii TBC, unajua kila mtu ana familia yake, mnakutana mtaani mnaponda kila kitu akifika kwake anaangalia fresh tuu
 
Ktk hili ni kana kwamba unawalaumu TCRA, binafsi siamini kama ni kosa ktk kusimamia kweli, kama wahusika walipaswa kuonyesha chaneli husika bure ila walikuwa wakitutoza fedha kwa kipindi chote hicho, sidhani kama kuna kosa limefanywa na Serikali ktk kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma inaendelea kufanywa kwa wananchi wake. Siamini kwamba kila linalofanywa na Serikali kwamba ni jambo baya, mazuri tusifie, mabaya tukosoe na KUONYESHA NAMNA BORA YA KUYASHUGHULIKIA. Tutoe solutions kwa yake tunayoonza utatuzi wake una changamoto, tusiishie kulaumu pekee!
Watu masikio yao yamejaa nta za chuki, macho yamezibwa na tongotongo za wivu na hasira binafsi so hawawezi kukuelewa kabisa mkuu
 
MImi naangalia sana the stiry of kawangare. Maisha magic east. Nishasahau kama nipo Tanzania.
Hii ni kwa sababu ya upumbavu wa viongozi wetu.

Mpaka nikienda dukani naanza kununua kimbo, royco mchuzi mix. Yani najiona mkenya kabisa. Imebaki tu kuhamia Kenya.

Clouds 360 nishaisahau kabisa kwa sababu ya kenge hawa na walaaniwe kabisa
Mimi badala ya wasafi TV na tazama MTV base mpaka najiona niko naija
 
MImi naangalia sana the stiry of kawangare. Maisha magic east. Nishasahau kama nipo Tanzania.
Hii ni kwa sababu ya upumbavu wa viongozi wetu.

Mpaka nikienda dukani naanza kununua kimbo, royco mchuzi mix. Yani najiona mkenya kabisa. Imebaki tu kuhamia Kenya.

Clouds 360 nishaisahau kabisa kwa sababu ya kenge hawa na walaaniwe kabisa
Karibu sana ila umechelewa.
 
Kenya itawambukiza Watanzania uchu wa demokrasia. Demokrasia imekomaa Kenya.
 
Back
Top Bottom