Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Kabla ya kwenda moja kwa moja napenda kuweka wazi kuwa mimi ni mtu ambaye sipendi kuona watu wakionewa na hasa kunyimwa haki zao za msingi.
Kumekuwepo na dhana potofu hapa Tanzania kuwa kila mtu anayeikosoa Serikali ya sasa ya awamu ya tano lazima akutane na mkono wa chuma.Dhana ambayo imekuwa ikiwafanya watu wengi wadhanie kuwa kuna ubabe na uvunjifu wa haki za raia hapa BongoTz.
Na mbaya zaidi ni hii ya kuaminisha watu kuwa kila anayeikosoa serikali basi lazima abambikiwe kesi ya uhujumu uchumi ili baadae pesa zimtoke ili akomolewe.
Lakini hivi majuzi baada ya Tito Magoti na mwenzake kukiri kosa ukweli wa mambo umejulikana,na ni wazi kuwa sio wote wanabambikiwa kesi,maana hili la kubambikiana kesi nalo lina siri kubwa.
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi,Tito Magoti na mwenzake waliunda genge la uhalifu ili waweze kueneza proganda za uongo kuwa serikali ya Tanzania inagandamiza haki za binadamu. Na wamekiri kuwa kulikuwa na mtandao unaojiita Tanzania on Twitter ambao ndio uliratibu kuundwa kwa hili genge. Ni genge ambalo linaonekana kujidhatiti ili kuchafua sifa ya nchi yetu.
Tito na mwenzake walipewa namba za simu zilizosajiliwa Holland na walishirikiana na watanzania wanaoishi nje kufanya uhalifu huo,huku wakiahidiwa kujipatia kipato kikubwa tu. Hii ilikuwa ni pamoja na kumiliki programu za komputa ili kufanikisha uhalifu wao.
Wamekiri makosa na kisha kulipa mil 17354535. Na hii inatupa ukweli kuwa sio kila anayeikosoa serikali anakosoa kwa nia njema. Na sio kila anayekosoa anabambikiwa kesi za uhujumu uchumi.
Kwa muktadha huu huenda hata genge la akina Eric na wenzake pia kuna mambo makubwa yaliyojificha nyuma ya pazia,lakini watu kwa kuangalia shilingi upande mmoja waliituhumu serikali kumbambikia kesi.
Maoni; Tujihadhali na wanasiasa kama Zitto ni watu wabaya sana ambao hutumia watu kwa manufaa yao kisiasa, huku wao wakila bata na kunufaika na kuwaacha vijana wenye tamaa wakitiwa nyavuni.