Baada ya Tito Magoti na mwenzake kutiwa hatiani ni dhahiri kuwa sio kila anayejinasibu mkosoaji wa Serikali anabambikiwa kesi ya Uhujumu Uchumi

Hoja dhaifu
 
Acha upuuzi,wamekiri kosa na wamekiri kuunda hili genge na kumiliki namba za simu za nje. Kuna mtu aliwalazimisha kukiri?
Tumia akili japo kidogo,unadhani kwao ipi ilikuwa chaguo sahihi
1) Kuozea gerezani Kama Masheikh wa uamsho bila upelelezi kukamilika au
2) Kukubali kosa la kubambikiwa kisha kulipa faini ya kujenga Daraja la Busisi na kutoka nje?
 
Sema wamekubali kuchangia makusanyo,na sii kweli unapenda haki,vinginevyo tuthibitishie uyasemayo.
 
🤔🤔🤔🤔
 
Nakubaliana na wewe hapa. Kama mtu hujatenda kwa nini ukubali kununua uhuru wako kwa kukubali kosa ambalo hukulifanya. Mimi nina mashaka sana na hizi plea bargaining, kwa upande flani zinakuwa za kweli na sio kununua uhuru tu kama tunavyojaribu kuaminishwa. Mbona kina Mandela walovumilia tena enzi ambazo hata upashanaji wa taarifa ulikuwa hafifu. Tukiachana na hayo ya kuichafua serikali, mbona kina mzee Rugemalila hadi leo wamekomaa na naamini ipo siku watatoka tu. Mie toka Kabendera akubali makosa eti kwamba ananunua uhuru wake, nimekuwa na mashaka makubwa ya hawa wanaosema wamebambikiwa kesi. Akili za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Acha upuuzi,wamekiri kosa na wamekiri kuunda hili genge na kumiliki namba za simu za nje. Kuna mtu aliwalazimisha kukiri?
Hata Kama huna akili hata za kuokoteza,unashindwa kuelewa kuwa siku zote walizokaa Getezani upande wa mashitaka wameshindwa kukamilisha upelelezi.


Erick Kabendera upelelezi wa shauri laki ulikamilika?
Rugemalila na Sethi leo ni miaka mingapi wako Jera,je upelelezi wa shauri lao umekamilika?
Tumua hata akili za kuzaliwa kutofautisha Mambo ya msingi.

Siyo lazima upost au uchangie ,unaweza kukaa kimya na kusoma maoni ya watu wenye akili timamu na ukajifunza kitu.
 
Tumia akili japo kidogo,unadhani kwao ipi ilikuwa chaguo sahihi
1) Kuozea gerezani Kama Masheikh wa uamsho bila upelelezi kukamilika au
2) Kukubali kosa la kubambikiwa kisha kulipa faini ya kujenga Daraja la Busisi na kutoka nje?
Bado unarudia kuwa ni kosa la kubambikiwa?
 
Tumia akili uliyo nayo iwe msaada kwa jamii au familia yako?

Kesi ya kina Rugemalila upelelezi umesha kamilika?
Je Kama mashitaka waliyonayo ni ya kweli,kitu gani kinafanya upande wa mashitaka ushindwe kukamilisha upelelezi kwa miaka yote?
Je huoni Kama wangekuwa namekiri makosa yao,pesaa zao zingekuwa zimepolwa kupitia DPP? na wangekuwa wameachiwa kutoka Jera?
 
Kwa hiyo wewe unaamini inatumia akili kuliko wengine? Acha dharau, hatuwezi kuwaza sawasawa wakati wote, na usijione kuwa upo sahihi kwa unayoyasema. Hoja yangu hapa ni kwamba watu watakuwa wanafanya makosa kweli halafu wanajificha kwenye plea bargaining kwamba wamelazimika kununua uhuru wao. Hivi unajua uzito wa kukubali kosa la kuendesha genge la kihuni, na madhara ya kutiwa hatiani kwenye kesi ya jinai. Unaweza kudhani kuwa dunia inaamini kuwa unaonea, lakini hiyo inakwenda kwenye kumbukumbu zako kuwa uliwahi kutiwa hatiani bila kujali kama ulinunua uhuru wako au hapana. Innocence always gives courage, haijalishi unapitia katika madhila gani. Kabla hatupiga kelele kwamba flani kanunua uhuru wake, tuwe tunajiuliza mara mbili kwanza. Plea bargaining limekuwa chaka la pande zote mbili. Kuna wengine na wakosaji kabisa, lakini wanafurahi wakipewa kesi ya uhujumu uchumi kwa sababu wanajua watapitia hapo kuukwepa mkono wa sheria. Sio kila kosa la jinai mtu anaweza kuplea bargain. Ila likiwemo la kuplea bargain kuna watu wanatumia mwanya huo kujifanya wamenunua uhuru, tuwe makini.

Tito Magoti na mwenzake hawajamaliza muda mrefu kiasi hicho kama ambavyo unataka kutuaminisha. Mashekh wa uamsho nao unawazungumziaje?

Tazama mambo kwa macho mawili, hatuhukumu mtu hapa, lakini kuna walakini mkubwa hapa.
 
Kwani ulikuwa umekamilika? Hujui kuwa ni Murder case na uhujumi uchumi ndio hujuchukia muda mrefu?
Upelelezi wa hizo kesi sio sifa kuchukua muda mrefu mpaka ukamilike, hilo linasababishwa na uzembe wa waendesha mashtaka wa serikali, una mdororo mkubwa wa akili.
 
Upelelezi wa hizo kesi sio sifa kuchukua muda mrefu mpaka ukamilike, hilo linasababishwa na uzembe wa waendesha mashtaka wa serikali, una mdororo mkubwa wa akili.
tindo hii ishu imekufanya uwe baridi
 
Acha upuuzi,wamekiri kosa na wamekiri kuunda hili genge na kumiliki namba za simu za nje. Kuna mtu aliwalazimisha kukiri?
Kaka sijui Dada endelea tu kuandika unacho jisikia hapa, siku ukipata bahati ya kufahamu nini kinaendelea kule gerezani na pale ofisi ya DPP ndiyo utakuja kujua kwa nini upelelezi huwa haufiki mwisho na watu huamua kukubali yaishe ili kununua uhuru wao.
 
We kweli ni mjinga wa mwisho. Unaandika kama mtanzania unayeishi nchi za Scandinavia, kumbe upo hapa hapa nchini. Shikirisha akili zako bhana
 
Nimeipuuza mada yako, naona unanilazimisha kunilisha ujinga. Niko above hiki unachokiamiani na kukitetea.
Hata siku moja ukweli na uongo haukai pamoja. Hii kesi jinsi ilivyowekwa hadharani ni wazi kuwa huwa mnaongea uongo wa kukaririshwa tu.
 
Umesahau kuandik namba ya simu
 
Wanapewa kesi za uhujumu uchumi sababu hazina Dhamana na pia ushahidi huwa haukamiliki ni Hadi utoe pesa ununue uhuru wako ndipo ushahidi utakamilika,kukubali kosa hakumaanishi kwamba umetenda kosa ni kuepuka kukaa ndani miaka watakayotaka wao, lengo kuu la kesi za uhujumu uchumi ni kukukomoa,thus pana dabo standard kwa hili ukiwa na chapa hizo kesi hazikuhusu hata utende the same case study makonda,chenge,kange,musiba,heri,nk.
Pana jamaa yangu KILA kitu documents zote zilikuwa safi na zote zimelipiwa na hakuna ushahidi wa kumtia mashakani shida ni kukaa ndani ujui lini utatoka baada ya kukaa ndani mwaka akapima kipi bora aendelee kukaa ndani miaka Ili apate haki yake au akiri kosa alipe faini, Ili aokoe familia akaona familia ni bora kuliko Kazi na kukaa ndani ujui mwaka gani utatoka.
Mwaka wa pili sasa na Mungu kamjalia anapambana na biashara zinamuendea vizuri kuliko hata Kazi na familia inaenda vizuri.Kuliko kukaa ndani huku familia ikikosa muongozo na kusambaratika kabisa unatoka watoto washakuwa machokora,mke alishaolewa unaanza upya.
Hii ni sheria kandamizi kabisa na yenye dabo standard,sijui huwa wanajisikiaje kushiriki ibadani Hali wao ni wa motoni umuongopeana nani sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…