Baada ya Trump kumdhalilisha Zelensky, Waziri Mkuu wa Uingereza atangaza kuwa UK iko tayari kupeleka wanajeshi wake Ukraine

Baada ya Trump kumdhalilisha Zelensky, Waziri Mkuu wa Uingereza atangaza kuwa UK iko tayari kupeleka wanajeshi wake Ukraine

Ya kwamza mpaka 5 ni akina nani?
Hawa hapa mpaka 10
Screenshot_20250303_125246_Chrome~2.png
 
Kwenye hili la kusaidia Ukraine hata wapinzani wa Starmer nchini UK wanamuunga mkono.

Hata nchi nyingi za UE wataunga tella maana wanamuona Putin kama tishio kwa hatma ya Ulaya ambaye ni lazima adhibitiwe.
Wanajua "usipoziba ufa utajenga ukuta"
Na hapa ndo tutarajie mlipuko....
 
Marekani chini ya trump ni ovyo sana
Wale wote walikuwa wanashangalia na kumpigia kura kawafukuza kazi kwa kumtumia Elon musk
Sasa hivi ni vilio kwa kwenda mbele walidhani ni wale waliompigia kura Kamala ndio watafukuzwa 😀
Marekani kuna wajinga wengi sana per capita kulinganisha na nchi za ulaya
 
Kwa hiyo wangekaaa tu wasifanye lolote? Nyumba yako inavamiwa umekaa tu unamuambia jirani abebe kila kitu?

Huko majuu wangekuwa wanawaza hivyo wasingekuwa hapo walipofika
Naona umemjibu bila hata kuelewa hoja yake.
Jamaa anamaanisha hivi,kabla kabisa ya Urusi kuivamia Ukraine kulikua Kuna nafasi kubwa TU ya kuepusha vita hii kwa njia za mazungumzo na makubaliano kama ya Minsk.
Yaani Urusi walitumia muda mwingi sana kuomba madai yake yasikilizwe lkn zelensky alilewa ahadi ambazo ndio zimemfikisha hapa.
Jamaa ana hoja.
Kabla ya uvamizi kulikua Kuna nafasi za mazungumzo ya kuepusha vita zelensky hakuzitumia,mkumbuke Boris Johnson statement "let's do war"
 
Wewe utakuwa unamsikilizaga sana George Galloway.
Muingereza aliwekeza sana kwenye teknolojia za vita hasa huko upande wa AI na alishaanza kupunguza wanajeshi wake........nchi za ulaya kutoa tu misaada ya silaha mfano ujerumani baadae akajikuta hata silaha zake mwenyewe za kujilinda zimepungua.....Mmarekani anaviwanda ambavyo vinamuwezesha kutoa mzigo mkubwa na hapohapo kufidia zilizotoka Mjerumani viwanda vyake vingi sio vya silaha akitaka aende sawa na mmarekani labda hivyo viwanda vya magari afunge avibadili kua vya silaha, hana ubavu wa kufanya kama anavyofanya Marekani, na Ujerumani kwa ulaya ndo powerhouse yao ya uzalishaji na amefloat sembuse hao wengine
 
No, TRUMP is realistic, hawa kina Steimer ni wanafiki tu, hivi Cameron aliyemlazimisha Zelensky kuendelea na vita na sio amani, leo yuko wapi?. Hakuna Bunge lolote la Ulaya litaridhia wanajeshi wake kwenda UKRAINE, kwa sababu hizi;
1. Ukraine imeshapoteza pakubwa mno.
2. Hakuna Morali ya umma wa wazungu juu ya vita hii tena. March 2022 ilikuwa wakati sahihi and not now. Raia wao watawauliza wanataka kupeleka wanajeshi ili wapate nini?
3. Hali ya kiuchumi ya nchi za ulaya si nzuri, so kuingia vitani ni kuziumiza zaidi nchi zao kisiasa
4. Anguko la Kisiasa la Serikali zitazoridhia mchakato huo ni dhahiri.
5. Hawana Support ya Marekani. Uingereza haiwezi pigana na Mrusi direct pekee yake bila Marekani. Juzi Steimer kakili hili mwenyewe.

Kinachowasumbua hawa Waulaya ni namna gani watasurrender maana ni fedheha kwao.
✔️
 
Wakuu,

Baada ya Trump kuonekana kuanza kuringaringa na kumnyanyasa Ukraine, Uingereza imeamua kuuvaa wenyewe huu ugomvi.

Akiwa anaongea hivi karibuni, Starmer amesema kuwa ukiachana na Euro Bilioni 2, Uingereza pia iko tayari kupeleka wanajeshi wake Ukraine kupambana na Urusi na pia iko tayari kupeleka ndege zake za kivita

========================================

Starmer inabidi ajitafakari sana.

Yaani Marekani ikiamua, hata yeye anaweza kuondolewa madarakani vilevile.

Mzee ajitafakari sana huyu

hv ukimya wa mataifa ya Ulaya , unakudanganya ? ULAYA WALIANZA KUONA USA SIO MTU MWAMINIFU KITAMBO SANA WALISHAANZA KUJIKUSANYA KITAMBO SANA , USA HAEZ ATTEMP KUPAMBANA NA ULAYA MAANA KILA MTU DUNIANI ANAOMBA USA AANGUKE , SO ITAKUWA FURSA KWA MAADUI WA USA
 
Hayo ni maneno matupu ya mkwara, lakini hayatekelezeki bila msaada wa Marekani. UK kwa sasa kipaumbele chake ni kuimarisha jeshi lake ili kujilinda yenyewe. Haina uwezo wa kuingilia mgogoro wa nchi nyingine kwa nguvu kubwa maana itapunguza sana uwezo wa kujilinda yenyewe.
duh kisa huon UK ikisifiwa jf bas ushaidharau?
 
Wakuu,

Baada ya Trump kuonekana kuanza kuringaringa na kumnyanyasa Ukraine, Uingereza imeamua kuuvaa wenyewe huu ugomvi.

Akiwa anaongea hivi karibuni, Starmer amesema kuwa ukiachana na Euro Bilioni 2, Uingereza pia iko tayari kupeleka wanajeshi wake Ukraine kupambana na Urusi na pia iko tayari kupeleka ndege zake za kivita

========================================

Starmer inabidi ajitafakari sana.

Yaani Marekani ikiamua, hata yeye anaweza kuondolewa madarakani vilevile.

Mzee ajitafakari sana huyu

Waendeee mara ngapi?
 
Muingereza aliwekeza sana kwenye teknolojia za vita hasa huko upande wa AI na alishaanza kupunguza wanajeshi wake........nchi za ulaya kutoa tu misaada ya silaha mfano ujerumani baadae akajikuta hata silaha zake mwenyewe za kujilinda zimepungua.....Mmarekani anaviwanda ambavyo vinamuwezesha kutoa mzigo mkubwa na hapohapo kufidia zilizotoka Mjerumani viwanda vyake vingi sio vya silaha akitaka aende sawa na mmarekani labda hivyo viwanda vya magari afunge avibadili kua vya silaha, hana ubavu wa kufanya kama anavyofanya Marekani, na Ujerumani kwa ulaya ndo powerhouse yao ya uzalishaji na amefloat sembuse hao wengine
Nchi za ulaya ziliendelea kwa kunyonya makoloni, mfano Uingereza wakijizolea pamba za bure India na China waliwafanya mateja wa opioid. Baadae wakaja Afrika kunyonya pia.

Pesa walizopata wakatumia kwenye majeshi na kufanya maisha yao kuwa ya juu. Sasa nchi walizozinyonya zimeendelea na resources walizojiokotea kirahisi hazipo tena, hivyo hawawezi tena kugharimia majeshi makubwa kama zamani.
 
Tatizo Una low IQ . Jitathmini .

Which countries have given the most to Ukraine?


European countries have provided €132 billion in aid (military, financial and humanitarian) as of December 2024, and the United States has provided €114 billion. Most of the US funding supports American industries who produce weapons and military equipment.
Katika kitu kibaya kwenye maisha ni kuwa na uwezo mdogo wa ufahamu na kisha ukajiona unajua kuliko waliokuzidi utaharibu na kupotea njia, ni bora uwe na uwezo mdogo na utambue nafasi yako katika uwezo utapata nafasi ya kujifunza.

Kwanza hoja ilikuwa kwamba UK anatoa sana kuliko US hapo nafikiri kutokana na uwezo wako mdogo sana umeshajimaliza kwa kujipinga mwenyewe kuwa hicho kitu hakipo bila kujua kuwa umejipinga na ukaamua kutoa data za Europe combined na siyo UK vs US ( Very low IQ)

Tukirudi kwenye data ulizotoa as per december 2024, wanaposema US aid yake kubwa kwenye military ni kwa sababu yeye ndiye mtengeneza silaha mkubwa kuliko yeyote kwenye NATO hivo anapeleka silaha kwa kuwa huyo Ukraine anahitaji hilo.

Lakini pia ametoa kiwango kikubwa kama financial and humanitarian aid

Mgawanyo wa hizo aid as per december 2024 kama report ya Ukraine inavosema hapa👇


Europe has allocated EUR 70 billion in financial and humanitarian aid as well as EUR 62 billion in military aid. (Ndiyo hiyo total 132B) This compares to EUR 64 billion in military aid from the US as well as EUR 50 billion in financial and humanitarian allocations.(Ndiyo hiyo 114B)

Sasa ndugu hapo UK alone anamzidi vipi US, wakati hao Europe wote waungane wapo margin ndogo na US

Na ukitaka data hadi February 2025 sema.
 
maneno kama haya ndio mliokuwa mnayatumia kutudanganya pia kuhusu israel,
Kama tangu mwaka 1946 yupo na amezungukwa na maadui katika ardhi inayolingana na Kigamboni, kwanini tusiamini ana jeshi imara?
 
Kwani putin bado anao?
Hukusikia baada ya kuishiwa askari alienda kuomba na akapewa msaada wa wapiganaji 10k kutoka North Korea, ambao pia wameshamalizwa chap?
Huo moto wanaopelekewa Ukraine na mercemaries wa NATO hauoni?

Hizo za wanajeshi wa N.K ni cheap propaganda
 
Back
Top Bottom