Mkuu, lazima ujue upo kwenye nchi ya aina gani.
Nchi yako bado ni Maskini. IPO chini Sana.
Kutoa Tuzo ni sehemu ya kuleta hamasa kwa vijana wasio na Ajira Kutafuta kitu chakufanya kama wenzao waliojitafuta wakapata cha kufanya na sasa wamepewa Tuzo.
Coy Mzungu kahangaika kuisimamisha Standup Comedy, kupitia yeye vijana wengi wamejiingiza kwenye kujiajiri kupitia uchekeshaji wa jukwaani.
Mazingira bora ni pamoja na kuwatangaza vijana na vipaji vyao kupitia Tuzo.
Hivi unajua kijana akipewa Tuzo mbele ya Rais inamaana gani kwenye Tasnia au fani yake?
Mazingira wezeshi kwa Vijana ni Jambo Bora Sana. Hiyo ni hoja nyingine.
Na Tuzo ni sehemu ya motisha katika mazingira Bora na wezeshi kwa Vijana kujiajiri
Walitakiwa waweje?
Nchi inapambana na mambo mengi. Kuyawezesha yote kwa pamoja ni Kazi hasa kwenye jamii ambayo watu wengi hawana Elimu.
Kwa hiyo hoja yako ni vijana waliopambana wakafika hapo walipofika wasipewe Tuzo kwa Sababu ya serikali kutokuwekeza juu Yao?
Wewe unauhakika gani serikali haijachangia ukuaji wa vipaji wa hao vijana?