Baada ya uamuzi wa jana CHADEMA na Halima wana mtihani mkubwa

Baada ya uamuzi wa jana CHADEMA na Halima wana mtihani mkubwa

Fundi Mchundo

Platinum Member
Joined
Nov 9, 2007
Posts
10,448
Reaction score
8,705
Hii sakata ya Halima na wenzake inatoa fursa kwa Chadema kujisahihisha. Kuna uwezekano mkubwa kuwa Halima aliamua kufanya alichofanya baada ya kuhisi kuwa kuna orodha mbadala ilitayarishwa tofauti na ile ambayo yeye na wenzake waliona kuwa ni ya haki. Wasiwasi huo usingekuwa bure kwa sababu vyama vyetu vyote vya siasa vina mtindo wa kudharau maoni ya wanachama wao linapokuja suala la udiwani na ubunge.

Nakumbuka Chadema jinsi walivyomuacha binti aliyeshinda kura za maoni na kumpa John Mrema nafasi ya kugombea badala yake. Mambo kama hayo yanasababisha watu waamini kuwa chama hicho kina wenyewe. Kwa vile kuna uwezekano wa Chadema kuteua wabunge wa kuchukua nafasi za wakina Halima, ni muhimu mno wajiepushe ya kuweka watu ambao uongozi unawapenda badala ya wale ambao wapiga kura wanawapenda.

Ningeshauri kuwa wawakataze jamaa zao au watu wewote wenye ukaribu nao kugombea nafasi hizi. Wahakikishe kuwa Bawacha ndio wanaongoza mchakato mzima. Na Bawacha nao waepuke makundi na wachague wale ambao ni wamethibitisha loyalty yao kwa chama na ni wapiganaji haswa. Wafanye jitihada za makusudi kuhakikisha nafasi hizo hazitawaliwi na watu kutoka eneo moja. Na muhimu zaidi mchakato mzima uwe wa uwazi na uwashirikishe wanachama wake wote bila upendeleo wowote.

Halima anastahili pongezi kwa kuweza kuhakikisha kuwa kikundi anachokiongoza kimeshikamana mpaka hatua hii. Challenge yake ni kuendelea nao hivyo hivyo wakati tumaini la kuwa wabunge limepotea. Anaweza kuanzisha vita dhidi ya chama chake cha awali ( kama Waitara na Lijualikali) au kutafuta njia ya kutibu majeraha yao bila ya kuleta mpasuko katika chama anachosema anakipenda na bila shaka bado kuna wengi wanampenda ( kama Selasini).

Kwa vyovyote vile wote hawa wanatakiwa kujitathmini vizuri na kukiri makosa waliyofanya na kuhakikisha hawatayarudia tena hapo mbeleni.

Amandla...
 
Back
Top Bottom