Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 652
- 1,058
Maana halisi ya nguvu ya umma sasa imeonekana. Uwazi wa kura wanazopata wagombea katika hatua ya Vyama inahamasisha sana na wananchi tunaona maana ya kura sasa. Vyama vyote ambavyo kwa vyovyote vile vitabadili wagombea na kuwaacha wale ambao wanaonekana vinara wanatakiwa wafanye hivyo kwa umakini sana kwani wanaweza kupoteza kwenye Uchaguzi.
Thamani ya mpiga kura imeonekana sana katika Uchaguzi huu wa ndani ya Vyama. Anayetakiwa anapata hata kama elimu yake ni chini au hata kama hana kitu. Tunatoka katika hatua ya wajumbe na sasa tunaenda katika hatua ya wapiga kura. Wale amabao hawakujiandikisha kupiga kura sasa wanajuta kwani wanaona sasa thamani ya kura.
Thamani ya wajumbe na uwazi katika kuhesabu kura unaonesha wazi kuwa wananchi wengi wanatamani Uchaguzi wa Mwaka huu ufuate mlolongo huo huo. Katika Uchaguzi Mkuu wapiga kura wote watakuwa ndiyo wana"portray" neno "wajumbe".
Chama changu CCM naona kinafundishwa kuona mbele - msijaribu kubadili dhamira ya wajumbe kwa sababu huyo ni mtu wao - yawezekana kabisa wanampenda kwa sababu huwapa chochote ambacho nyie mnaifanya hiyo ni rushwa. Wajumbe hawajui kama hiyo ni rushwa bali wanaithamini kama ukarimu.
Kwa maana hiyo mwaka 2025 tutegmee wananchi wengi zaidi watakuwa wamejiunga kwenye vyama vya siasa na pia wananchi wengi zaidi wataamua kujiandikisha kuwa wapiga kura. Umuhimu wa wapiga kura sasa unaonekakana- hata ambaye hajasoma hata darasa moja kura yake katika kuweka uongozi ina maana sana. Wameaibika sana wale waliopata sifuri. Kazi kweli kweli.
Angalieni Sengerema na Bunda walikoshinda darasa la saba hao watu wana uwezo wa kifedha na wanaishi na wajumbe so ni ngumu kuwatenganisha nao. Vivyo hivyo mnaweza kumbuka hata Lameck Airo - ni la saba lakini kwenye ubunge kadumu sana mapka alipoamua kujiondoa mwenyewe. Ni hayo tu!
Tunakoenda nami ni Mjumbe come Oktoba!