Baada ya Uchumi wa Tanzania kuporomoka kuna haja ya maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba kufanyika mwaka huu?

Baada ya Uchumi wa Tanzania kuporomoka kuna haja ya maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba kufanyika mwaka huu?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
143,138
Reaction score
288,731
Kabla ya yote naomba kukiri kwamba mimi na makampuni yangu tumeshiriki maonesho ya kibiashara ya kimataifa kwa zaidi ya miaka 10 , tukijikita zaidi kwenye local products kwa ajili ya export ( yaani bidhaa za kitanzania za kuuza nje ya nchi ), 90 % ya bidhaa zetu tunauza Ulaya na Marekani, tulilazimika kushiriki maonesho haya kwa lengo la kutafuta network ya kimataifa kutoka kwa mabalozi na watu wengine wageni waliotembelea banda letu .

Baada ya Corona ambayo kimsingi imezuia baadhi ya wadau wakubwa ambao ni Wazungu kuingia nchini mwetu, na huku hali halisi ya uchumi wa Tanzania ukiporomoka kwa kasi ya ajabu, hatuoni haja tena ya kushiriki maonesho haya, tutaendelea kusafirisha vifurushi vyetu katika nchi za wadau wetu huku tukipunguza uzalishaji kwa kiasi, tumeona tuendelee na International marketing through internet badala ya kusimika mabanda katikati ya masikini wasio na uwezo wa kununua chochote

Ndio maana nimeuliza baada ya hali ya uchumi wa nchi hii kuanguka , kuna haja yoyote ya maonesho haya kufanyika kwa mwaka huu?
 
Jibu nafikiri unalo. Hata tukifosi iwepo ni shoti tu. Maana watu watakosekanika na ukizingatia hatuna pesa. Na bado wafanyabiashara kutoka nje wasije.
 
Yatafanyika tu kwani zaidi ya mabanda kujaa taasisi za serikali huwa kuna jipya gani?
 
...badala ya kusimika mabanda katikati ya masikini wasio na uwezo wa kununua chochote
😬
 
Back
Top Bottom