Baada ya Uchumi wa Tanzania kuporomoka kuna haja ya maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba kufanyika mwaka huu?

Baada ya Uchumi wa Tanzania kuporomoka kuna haja ya maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba kufanyika mwaka huu?

Kabla ya yote naomba kukiri kwamba mimi na makampuni yangu tumeshiriki maonesho ya kibiashara ya kimataifa kwa zaidi ya miaka 10 , tukijikita zaidi kwenye local products kwa ajili ya export ( yaani bidhaa za kitanzania za kuuza nje ya nchi ), 90 % ya bidhaa zetu tunauza Ulaya na Marekani, tulilazimika kushiriki maonesho haya kwa lengo la kutafuta network ya kimataifa kutoka kwa mabalozi na watu wengine wageni waliotembelea banda letu .

Baada ya Corona ambayo kimsingi imezuia baadhi ya wadau wakubwa ambao ni Wazungu kuingia nchini mwetu, na huku hali halisi ya uchumi wa Tanzania ukiporomoka kwa kasi ya ajabu, hatuoni haja tena ya kushiriki maonesho haya, tutaendelea kusafirisha vifurushi vyetu katika nchi za wadau wetu huku tukipunguza uzalishaji kwa kiasi, tumeona tuendelee na International marketing through internet badala ya kusimika mabanda katikati ya masikini wasio na uwezo wa kununua chochote

Ndio maana nimeuliza baada ya hali ya uchumi wa nchi hii kuanguka , kuna haja yoyote ya maonesho haya kufanyika kwa mwaka huu?
Kwa hali inayoendelea ya kupuuza kila jambo, naonesha yataendelea ikiaminiwa ni njia ya kuukuza au kuufufua uchumi kama na wao watauona unakufa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom