Baada ya Uingereza kuazimia kuiwekea vikwazo Nigeria juu ya uvunjifu wa haki za binadamu, Nigeria imeenda kuomba isamehewe

Baada ya Uingereza kuazimia kuiwekea vikwazo Nigeria juu ya uvunjifu wa haki za binadamu, Nigeria imeenda kuomba isamehewe

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Wiki chache zilizopita Nigeria ilikumbwa na maandamano ya kupinga ukatili wa jeshi la polisi maarufu kama #EndSARS ambapo Jeshi la Nigeria lilituhumiwa kuua watu.

Bunge la UK Liliazimia kuwawekea vikwazo maafisa kadhaa wa Nigeria, jeshi la polisi na jeshi la ulinzi kwa uvunjifu wa haki za binadamu. Uamuzi huo umeungwa mkono na vyama vya upinzani na mashirika ya kimataifa, UN na nchi nyingine zimeombwa kuingilia zaidi na kuweka vikwazo.

Serikali ya Nigeria imetuma wataalamu wa mahusiano kwenda Uingereza ili kulizungumzia hili na kuomba Uingereza isifikie huo uamuzi kwani serikali iko inafanya mabadiliko makubwa na kushughulikia malalamiko ya wananchi.

 
Halafu hapa juha moja eti anajigamba kuwa sisi ni nchi huru tusiingiliwe wakati kila bajeti unatembeza bakuli.

Nigeria ndio nchi ya kwanza katika Afrika yenye uchumi mkubwa. Sasa itakuwaje kwa sisi tunaochakachua takwimu ili ionekane uchumi wetu unakua wakati uko taabani.
 
Jitu linapewa madaraka linaanza kuua watu hovyo, wakati halina uwezo wa kuumba hata siafu. Minya hao, nao waheshimu utu wa wengine.
 
Back
Top Bottom