Kuna implications zake iwapo ule wa miezi sita haukuwa mkataba halali. Kwanza, itakuwa sahihi kusema kwamba Simba walifanya mazungumzo kisha kumsajili mchezaji aliyekuwa huru (maana hakuwa na mkataba wa miezi sita). Pili, itakuwa sahihi kusema kwambaYanga katika mkataba wa miaka miwili waliouongeza (kama upo), watakuwa walimsainisha mkataba mpya kwa mara ya kwanza (maana hakuwa na mkataba wa miezi sita). Sasa hapo wote Simba na Yanga wamemsajili Morrison kwa mara ya kwanza tangu atue nchi, ilitakuja jambo kuhusu dirisha la usajili; je, ni nani amemsajili ndani ya dirisha la usajili, Yanga au Simba?