Baada ya uteuzi wa Katibu Mkuu wa CCM sasa Tanga itatulia hongera Rais Samia

Baada ya uteuzi wa Katibu Mkuu wa CCM sasa Tanga itatulia hongera Rais Samia

Standards Person

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2021
Posts
672
Reaction score
860
Kulikua na tetesi kwamba RC wa Tanga Martin Shigela angekua katibu mkuu wa CCM ili kuziba nafasi ya Bashiru Kakurwa. Baada ya tetesi hizo inasemekana chamani hapo Tanga ilikua ni pokopoko na nong'onong'o na vijiweni kwa jamaa au washikaji wa mtajwa wakaanza kutembea vifua mbele na mabega juu kwani walishajitabiria makubwa.

Wenye upeo walijiuliza,kwani katibu mkuu wa chama ndio anateua maDAS, RAS, RC, DC, DED nk?

Pia watu wakajiuliza itakuaje mtu apewe ukatibu wa chama wakati wakazi wa Tanga mjini hawamfahamu vizuri,wakaazi wameporwa ardhi,watumishi halmashauri wananyanyasika na kudharauliwa na baadhi ya maofisa ilihali RC huyo ameshindwa kumbana mkurugenzi aliyepo,je itakuaje akipewa chama pendwa? Wapambe hao walishaanza kuota ndoto kwa kujenga taswira ya halmashauri watakazoenda.

Walienda mbali zaidi wakasema katibu mkuu akiungana na waziri wa Tamisemi ushawishi unakua mkubwa hivyo wapambe hao watapata nafasi hatimae kula keki ya taifa mapande makubwa makubwa.

Pamoja na maumivu hayo ya kupigwa kumbo na kete kwenda kwa Mh. Chongolo bado wanajifariji kwamba Tamisemi yupo mpiganaji wao ambaye walimpigania hivyo lazima fadhila zilipwe.

Mh.Rais kutopendekeza jina la binadamu huyo nikwamba kwavyovyote vile Tanga hataonekana tena Shigela,DED na DC ndio wanatakiwa wafungashe virago,mabegi wayaandae kabisa kwa safari maana mama atatoa orodha mpya ya wateule. Hawa waondoke maana wamekaa sana Tanga wakajenga mazoea kazini.

Ukweli nikwamba wakati wao Tanga ushaisha. Uzembe kazini,rushwa,manyanyaso,dhuluma na kufukuzana makazini ndio basi tena.
Furaha ya wanatanga waliokumbana na adha ya wateule wa Rais na wakuu wa idara nikuwaondoa wasibaki hata mmoja.

Mh. Rais muangalie Ummy asije akakuletea watu wenye mikonomikono,wavivu,wazembe,wababe kazini na walipa visasi. Waziri Ummy alimsifia pia RC huyo nadhani alikua nae anaishi katika ule ulimwengu wa kufikirika kwamba RC huyo atapewa ukatibu mkuu. Binafsi ningeshangaa mtu ambae amekaa Tanga na hajulikani kwa wakaazi wengi wa Tanga ingekuaje apewe chama dume akakipiganie

Mh Rais hongera sana kwakutopeleka jina hilo kwenye Mkutano Mkuu. Mh.Rais Ummy nae muangalie asije akalipa fadhila kwa jamaa zake wanaharakati.

Mh. Rais hongera kwa kutopeleka jina la Shigela Mkutanoni na hatinae Tanga imetulia. Wamalizie DC,DED nao waondoke Tanga ili amani ipatikane
 
Back
Top Bottom