The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,942
- 20,077
Baada ya Marekani kuituhumu Huawei kuwa ni tawi la jeshi la China na kuiongezea vikwazo, mambo yamezidi kuwa magumu kwa Huawei.
Kuanzia mwakani Huawei hataweza kuzalisha chip zake za Krin zinazotumika sasa kwenye simu zake za P series.
Huawei alikua na mpango wa kutumia chipset ya 5mn+ zake mwenyewe ila mambo yamekua magumu sasa baada ya suppliers wake wote kusitisha kumpa huduma ili kuepuka vikwazo vya Marekani.
Mwezi wa 5 mwaka huu Marekani ilitunga sheria ya kuyabana makampuni yasiyo ya Kimarekani ila yanayotumia teknolojia ya Marekani kuipatia huduma Huawei. Ukigundulika ni vikwazo hadi unafilisika.
Marekani iliipa Huawei msamaha wa siku 90 hadi September 15 mwaka huu ili iweze kuuziwa vifaa inavyohitaji ili angalau simu zake za mwaka huu zitoke na chipset ya Krin. Baada ya hapo haitaruhusiwa tena. Makampuni mengi ikiwemo Samsung yamesitisha kuipatia vifaa Huawei kuepuka mkono mrefu wa Marekani.
Huawei sasa anaangalia Mediatek kama mbadala iwapo tu Mediatek ataweza kumuuzia Huawei vifaa vyake ambavyo havina hata chembe ya teknolojia ya Marekani.
Future ya Huawei haieleweki kuanzia 2021 kama vikwazo vya Marekani vitaanza kufanya kazi September 2020.
Huawei's 2021 flagship could use a third-party 5nm chipset - Gizmochina