Baada ya vikwazo vya Marekani, Huawei kutumia Mediatek chip kuanzia 2021

Baada ya vikwazo vya Marekani, Huawei kutumia Mediatek chip kuanzia 2021

Sasa kama watu wapo billion unafikiri nini..
Mkuu hao wanatumia huo mwanya ili wakunase ila watakupa ukitakacho ila kina kitu ndani yake.. kwenye ulimwengu wa ujasusi huko Mambo hayalali na ndicho unachotakiwa uwe makini..
Sasa huku kwetu mnaweza pewa hata komputa za msaada ati zinaenda kutumika ofisi za bunge..!!!
Hapo kaa ukijua upo uchi wa mnyama..😅
wote sawa tu mbona marekani anatuhuma za kudukua wenzake ikiwemo mazungumzo ya Markel?
 
wote sawa tu mbona marekani anatuhuma za kudukua wenzake ikiwemo mazungumzo ya Markel?
Huko ndo kunaitwa nipe nikupe..😅
Sasa lazima ujue na kujilinda ukizubaa unashangaa wamefika mpk chumbani wanazinyanyua nuclear..😅
 
Mkuu mediatek sio ya kuibeza. Ni moja kati ya chipset zinazowakimbiza wapinzani wake. Mimi sioni tatizo kwa upande wa ubora endapo huawei atahamia kwenye mediatek na kutoa vifaa vyenye latest chipset. Bado itakuwa ni simu nzuri.
Hawana chochote cha kukimbiza watu, labda huawei amwage mpunga watu wafanye tafiti zaidi, mwaka sijui wa ngapi huu mediatek hana flagship soc, mara ya mwisho ilikuwa ni p25 miaka zaidi ya mitano iliopita.
 
Sidhani hata kama mediatek wanauwezo wa kutengeneza soc bila technology za marekani, mpaka leo hawatoi source code za chip zao sababu tech sio yao na wana makubaliano ya kuificha, ni muda tu na wao pia watafungiwa.
 
Nokia , erickson, AT&T mungu anawaona. Mbeleko hii ...
Baada ya Marekani kuituhumu Huawei kua ni tawi la jeshi la China na kuiongezea vikwazo, mambo yamezidi kuwa magumu kwa Huawei.

Kuanzia mwakani Huawei hataweza kuzalisha chip zake za Krin zinazotumika sasa kwenye simu zake za P series.

Huawei alikua na mpango wa kutumia chipset ya 5mn+ zake mwenyewe ila mambo yamekua magumu sasa baada ya suppliers wake wote kusitisha kumpa huduma ili kuepuka vikwazo vya Marekani.

Mwezi 5 mwaka huu Marekani ilitunga sheria ya kuyabana makampuni yasiyo ya Kimarekani ila yanayotumia teknolojia ya Marekani kuipatia huduma Huawei. Ukigundulika ni vikwazo hadi unafilisika.

Marekani iliipa Huawei msamaha wa siku 90 hadi September 15 mwaka huu ili iweze kuuziwa vifaa inavyohitaji ili angalau simu zake za mwaka huu zitoke na chipset ya Krin. Baada ya hapo haitaruhusiwa tena. Makampuni mengi ikiwemo Samsung yamesitisha kuipatia vifaa Huawei kuepuka mkono mrefu wa Marekani.

Huawei sasa anaangalia Mediatek kama mbadala iwapo tu Mediatek ataweza kumuuzia Huawei vifaa vyake ambavyo havina hata chembe ya teknolojia ya Marekani.

Future ya Huawei haieleweki kuanzia 2021 kama vikwazo vya Marekani vitaanza kufanya kazi September 2020.

Huawei's 2021 flagship could use a third-party 5nm chipset - Gizmochina
 
Sidhani hata kama mediatek wanauwezo wa kutengeneza soc bila technology za marekani, mpaka leo hawatoi source code za chip zao sababu tech sio yao na wana makubaliano ya kuificha, ni muda tu na wao pia watafungiwa.
Naona Huawei ni pigo juu ya pigo.

Huu ni uamuzi wa leo. Baada ya Commerce Department kuwaweka blacklist imefuata FCC.
FCC designates Huawei, ZTE as risks to national security

Mkuu Chief, hiyo 5nm ikoje?
 
Naona Huawei ni pigo juu ya pigo.

Huu ni uamuzi wa leo. Baada ya Commerce Department kuwaweka blacklist imefuata FCC.
FCC designates Huawei, ZTE as risks to national security

Mkuu Chief, hiyo 5nm ikoje?
5nm hio ni manufacturing process, ukubwa wa transistor. Nm kirefu chake ni nanometer kwenye kila mita 1 kuna nanometer bilioni 1, hivyo unaona jinsi zilivyo ndogo.

Jinsi nanometer zilivyo ndogo ndio jinsi unavyozipack nyingi kwenye die ya processor na ndio jinsi processor inavyokuwa na nguvu.

Hii ni picha ya die ya processor ikionesha transistor zenye ukubwa wa 843nm

032.jpg

Hio 5nm ndio tech ya kisasa zaidi kwenye utengenezaji chip kwa sasa na makampuni mengi kama Apple, Amd, Samsung, Qualcomm etc wanatumia.
 
Mkuu mediatek sio ya kuibeza. Ni moja kati ya chipset zinazowakimbiza wapinzani wake. Mimi sioni tatizo kwa upande wa ubora endapo huawei atahamia kwenye mediatek na kutoa vifaa vyenye latest chipset. Bado itakuwa ni simu nzuri.
Usitetee utopolo
 
Hawana chochote cha kukimbiza watu, labda huawei amwage mpunga watu wafanye tafiti zaidi, mwaka sijui wa ngapi huu mediatek hana flagship soc, mara ya mwisho ilikuwa ni p25 miaka zaidi ya mitano iliopita.
Na ndo anachofanya huawei, ndo maana anatumia 40% kwanye RnD na naamini tangu hili saga limeanza, hili alilijua
So nadhani atakuwa na solution. But huawei haiwezi mufa
 
Na ndo anachofanya huawei, ndo maana anatumia 40% kwanye RnD na naamini tangu hili saga limeanza, hili alilijua
So nadhani atakuwa na solution. But huawei haiwezi mufa
Haiwezi kufa sababu ipo backed na serikali ya china. Ila mediatek sio solution sababu na wao pia wanategemea tech za usa siku yoyote ile wanapigwa Pin na wao.

Na hata hizo research za Huawei zipo Ulaya za kutosha, Finland anawasaidia sana Tu hasa kwenye simu ila indirect wamempiga chini Nokia kwenye Tenda zao. Kifupi hawa jamaa watapata tabu sana sababu hawana marafiki.

Hadi nchi zinazowazunguka singapore, Tibeti, taiwan, south Korea, Hongkong, vietnam, India etc wote wamempiga chini Huawei kwa security reasons.
 
Aise Mimi naamini ukibwana na kushambuliwa na mashoga na marafiki uwezo wa kufikiri unaongezeka, hope mchina atakuja na new idea....
 
Usitetee utopolo
Technolojia haiendi kiushabiki kama tunavyochukulia hapa jf kama vile ligi za mpira. Na haimaanishi kwamba basi marekani ndio ameshikilia kila kitu. Wachina hawalali na walishafikiria hili suala muda sana. Hatua zilishaanza muda na kina oppo na huawei walishaanza kujihami na kujiwekea misingi kwaajili ya hali kama hii isiwaangushe kibiashara.
 
Back
Top Bottom