Baada ya vikwazo vya Marekani, Huawei kutumia Mediatek chip kuanzia 2021

wote sawa tu mbona marekani anatuhuma za kudukua wenzake ikiwemo mazungumzo ya Markel?
 
wote sawa tu mbona marekani anatuhuma za kudukua wenzake ikiwemo mazungumzo ya Markel?
Huko ndo kunaitwa nipe nikupe..😅
Sasa lazima ujue na kujilinda ukizubaa unashangaa wamefika mpk chumbani wanazinyanyua nuclear..😅
 
Mkuu mediatek sio ya kuibeza. Ni moja kati ya chipset zinazowakimbiza wapinzani wake. Mimi sioni tatizo kwa upande wa ubora endapo huawei atahamia kwenye mediatek na kutoa vifaa vyenye latest chipset. Bado itakuwa ni simu nzuri.
Hawana chochote cha kukimbiza watu, labda huawei amwage mpunga watu wafanye tafiti zaidi, mwaka sijui wa ngapi huu mediatek hana flagship soc, mara ya mwisho ilikuwa ni p25 miaka zaidi ya mitano iliopita.
 
Sidhani hata kama mediatek wanauwezo wa kutengeneza soc bila technology za marekani, mpaka leo hawatoi source code za chip zao sababu tech sio yao na wana makubaliano ya kuificha, ni muda tu na wao pia watafungiwa.
 
Nokia , erickson, AT&T mungu anawaona. Mbeleko hii ...
 
Sidhani hata kama mediatek wanauwezo wa kutengeneza soc bila technology za marekani, mpaka leo hawatoi source code za chip zao sababu tech sio yao na wana makubaliano ya kuificha, ni muda tu na wao pia watafungiwa.
Naona Huawei ni pigo juu ya pigo.

Huu ni uamuzi wa leo. Baada ya Commerce Department kuwaweka blacklist imefuata FCC.
FCC designates Huawei, ZTE as risks to national security

Mkuu Chief, hiyo 5nm ikoje?
 
Naona Huawei ni pigo juu ya pigo.

Huu ni uamuzi wa leo. Baada ya Commerce Department kuwaweka blacklist imefuata FCC.
FCC designates Huawei, ZTE as risks to national security

Mkuu Chief, hiyo 5nm ikoje?
5nm hio ni manufacturing process, ukubwa wa transistor. Nm kirefu chake ni nanometer kwenye kila mita 1 kuna nanometer bilioni 1, hivyo unaona jinsi zilivyo ndogo.

Jinsi nanometer zilivyo ndogo ndio jinsi unavyozipack nyingi kwenye die ya processor na ndio jinsi processor inavyokuwa na nguvu.

Hii ni picha ya die ya processor ikionesha transistor zenye ukubwa wa 843nm

Hio 5nm ndio tech ya kisasa zaidi kwenye utengenezaji chip kwa sasa na makampuni mengi kama Apple, Amd, Samsung, Qualcomm etc wanatumia.
 
Mkuu mediatek sio ya kuibeza. Ni moja kati ya chipset zinazowakimbiza wapinzani wake. Mimi sioni tatizo kwa upande wa ubora endapo huawei atahamia kwenye mediatek na kutoa vifaa vyenye latest chipset. Bado itakuwa ni simu nzuri.
Usitetee utopolo
 
Hawana chochote cha kukimbiza watu, labda huawei amwage mpunga watu wafanye tafiti zaidi, mwaka sijui wa ngapi huu mediatek hana flagship soc, mara ya mwisho ilikuwa ni p25 miaka zaidi ya mitano iliopita.
Na ndo anachofanya huawei, ndo maana anatumia 40% kwanye RnD na naamini tangu hili saga limeanza, hili alilijua
So nadhani atakuwa na solution. But huawei haiwezi mufa
 
Na ndo anachofanya huawei, ndo maana anatumia 40% kwanye RnD na naamini tangu hili saga limeanza, hili alilijua
So nadhani atakuwa na solution. But huawei haiwezi mufa
Haiwezi kufa sababu ipo backed na serikali ya china. Ila mediatek sio solution sababu na wao pia wanategemea tech za usa siku yoyote ile wanapigwa Pin na wao.

Na hata hizo research za Huawei zipo Ulaya za kutosha, Finland anawasaidia sana Tu hasa kwenye simu ila indirect wamempiga chini Nokia kwenye Tenda zao. Kifupi hawa jamaa watapata tabu sana sababu hawana marafiki.

Hadi nchi zinazowazunguka singapore, Tibeti, taiwan, south Korea, Hongkong, vietnam, India etc wote wamempiga chini Huawei kwa security reasons.
 
Aise Mimi naamini ukibwana na kushambuliwa na mashoga na marafiki uwezo wa kufikiri unaongezeka, hope mchina atakuja na new idea....
 
Usitetee utopolo
Technolojia haiendi kiushabiki kama tunavyochukulia hapa jf kama vile ligi za mpira. Na haimaanishi kwamba basi marekani ndio ameshikilia kila kitu. Wachina hawalali na walishafikiria hili suala muda sana. Hatua zilishaanza muda na kina oppo na huawei walishaanza kujihami na kujiwekea misingi kwaajili ya hali kama hii isiwaangushe kibiashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…