Kitaja
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 2,836
- 1,382
Ulimwengu umejikuta katika vita visivyoisha na wakazi wake kufanywa mawakala wa vita hizi. Jambo moja liko wazi nalo ni hili, mataifa yenye nguvu yamejitahidi kutwaa umiliki wa dunia nzima na hii imekuwa ni shauku ya kila taifa linalodhani lina nguvu kushinda wengine. Biblia hutaja mamlaka hizi kama zinazopita na hatimaye vita hizi zitakomeshwa na mamlaka kuu kushinda zote. Kumekuwepo mataifa yenye nguvu na dunia kupita katika milki ya falme kuu nne ambazo Mfalme Nebukadreza alionyeshwa katika kitabu cha Daniel 2. Tawala hizi zilitawala kwa mlolongo ufuatao;
1. Babeli: Utawala wa simba ama kichwa cha dhahabu (608-538 K.K)
2. Wamedi na Waajemi: Dubu ama kifua cha fedha (538-331 K.K)
3. Wayunani: Chui ama tumbo,kiuno cha shaba (331-168 K.K)
Huu utawala wa kiyunani uliofananshishwa na chui ulikuwa na mabawa manne ama uligawanyika katika falme nne.
4. Rumi: Chuma ama Mnyama wa ajabu (168 K.K.-476 B.K).
Huu uatwala ulikuja kugawanyika katika pembe kumi ama mataifa kumi ambayo ndiyo Ulaya ya leo.
i. Ujerumani-Alaman
ii. Ufaransa-Frank
iii. Uingereza-Anglo-Saxons
iv. Uswizi-Burgadian
v. Uhispania-Visogoths
vi. Ureno-Suev
vii. Uitaliano-Lombard
viii. Heruli
ix. Vandals
x. Ostrogoths
5. Pembe ndogo ilizuka kati ya hizo kumi na kuzing’oa pembe tatu za mwisho ( Heruli, Ostrogoths na Vandals) Daniel 7:24.Haya ni mataifa ambayo mamlaka zake ziliondolewa na Papa wa kirumi baada ya kukataa kumtii.
VITA KUU ZA DUNIA
1. Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia
Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilikuwa vita iliyopigwa kuanzia mwaka 1914 hadi 1918. Mataifa wapiganaji yalikuwa Ujerumani, Austria-Hungaria, Bulgaria na Uturuki (yaliitwa "Mataifa ya Kati", central powers) kwa upande mmoja dhidi ya Ufaransa, Urusi, Uingereza, Italia, Marekani na nchi mbalimbali zilizoshirikiana nazo (zilitwa "Mataifa ya Ushirikiano", allied powers).
Vita hii ilianza katika Ulaya ikapanuka haraka hadi Mashariki ya Kati, Afrika na Asia ya Mashariki ikasababisha vifo vya takriban watu milioni tisa.
Sababu na matokeo
Sababu yake ilikuwa mashindano makali kati ya mataifa ya Ulaya kuhusu kushika nafasi ya kipaumbele barani Ulaya na duniani kote.
Matokeo yake yalikuwa mwisho wa kipaumbele cha Ulaya duniani na kupanda ngazi kwa Marekani, mapinduzi katika nchi mbalimbali, mwisho wa falme za Ujerumani, Austria na Urusi pamoja na mwanzo wa utawala wa kikomunisti katika Urusi, mwisho wa Dola la Austria-Hungaria na wa Dola la Uturuki la Kiosmani pamoja na mwisho wa ukoloni wa Kijerumani duniani.Katika Ulaya nchi mpya zilijitokeza kama vile Chekoslovakia, Ufini, Latvia, Estonia na Yugoslavia pamoja na nchi za zamani zilizotokea tena katika uwanja wa kimataifa ndizo Austria, Hungaria, Lithuania na Poland.
Vita hii ilitwa "Vita ya Dunia" kwa sababu mapigano yalisambaa kote duniani. Sehemu kubwa ya mapigano yalitokea Ulaya na Asia ya Magharibi lakini pia katika makoloni ya Afrika, Asia na Pasifiki. Nchi za Amerika hazikuona mapigano kwenye nchi kavu lakini manowari za Ujerumani zilipigana na mataifa ya ushirikiano mbele ya pwani za Marekani na Amerika Kusini.
Ilikuwa pia vita ya kwanza iliyopigwa kote duniani ilhali habari zake ziliweza kufika katika muda wa masaa au siku chache kwa mataifa yote kutokana na upatikanaji wa vyombo vya mawasiliano hasa simu za kimataifa na redio.
Lakini kwa kweli haikuwa vita ya kwanza ya "dunia" maana vita ya miaka saba (1756-1762) ilipigwa pia kwenye mabara yote ya dunia baina ya nchi zenye makoloni hasa Uingereza, Ufaransa na Hispania.
Vita Kuu ya Pili ya Dunia
Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilikuwa vita vilivyodumu kuanzia mwaka 1939 hadi 1945 kati ya Ujerumani, Italia, Japani na mataifa yaliyoshikamana nazo(Romania, Hungaria na Bulgaria) dhidi ya nchi nyingi za dunia (ziliitwa mataifa ya ushirikiano) kati yake hasa Uingereza, Uchina, Urusi na Marekani.
Jina limetokana na vita ya miaka ya 1914-1918 iliyoona mapambano kati ya Ujerumani na wenzake dhidi ya nchi nyingi. Vita ya 1914/1918 iliitwa "Vita Kuu ya Dunia" kwa sababu mapigano yalienea pande nyingi za dunia, tofauti na vita zilizotangulia.
Kwa namna fulani vita iliyoanza 1939 ilikuwa marudio ya vita iliyotangulia. Hivyo imekuwa kawaida kuzitaja vita hizi kama Vita Kuu ya Kwanza na ya Pili ya Dunia.
Mwanzo wa vita. Vita hii ilianza huko Ulaya tarehe 1 Septemba 1939 kwa mashambulizi ya Wajerumani dhidi ya Poland. Wengine huhesabu mashambulizi ya Japani dhidi ya Uchina tarehe 7 Julai1937 kuwa mwanzo wa vita. Mwisho wake ulikuwa huko Ulaya tarehe 9 Mei 1945 halafu huko Asia tarehe 2 Septemba 1945.
Vita katika Ulaya
Mashambulizi ya Wajerumani dhidi Poland yalisababisha hali ya vita kati ya Ujerumani kwa upande moja na Ufaransa na Uingereza kwa upande mwingine waliokuwa na mkatabawa kulindana na Poland. Serikali za Australia, New Zealand, Nepal, Afrika Kusini na Kanada zilishikamana na Uingereza kwa kutangaza vita dhidi ya Ujerumani. Urusi, uliokuwa na mkataba wa siri na Ujerumani, ulichukua nafasi ya kuteka sehemu kubwa za Poland ya Mashariki.
Mwezi wa Aprili 1940 Waingereza walianza kupeleka wanajeshi Norway wakiwa na shabaha ya kuzuia kupelekwa kwa madini ya chuma kutoka Sweden kwenda Ujerumani kupitia bandari za Norway. Wajerumani walichukua nafasi hii kuteka Denmark na Norway na kufukuza Waingereza.
Mnamo Mei 1940 Wajerumani walishambulia Ufaransa pamoja na nchi za Uholanzi, Ubelgiji na Luxemburg. Vita hii ilikwisha haraka: Wajerumani walishinda na kupiga pia kikosi cha Waingereza huko Ufaransa. Baadaye walisitasita kushambulia Uingereza yenyewe. Mipango yao ilihitaji mbinu za kuvuka bahari. Wakajaribu kuvuruga nguvu ya kijeshi ya Waingereza kwa mashambulizi ya ndege lakini hawakuwa na uwezo wa kutosha. Katika shambulizi dhidi ya Ufaransa Waitalia walishiriki upande wa Wajerumani.
Mwisho wa mwaka 1940 Waitalia walianza kuwashambulia Ugiriki na jeshi la Waingereza huko Misri na Malta. Lakini mahali pote walirudishwa nyuma, hadi dikteta Mjerumani Adolf Hitler aliamua kuwasaidia Waitalia na kupeleka wanajeshi Wajerumani kwenda Afrika ya Kaskazini pamoja na Ugiriki mwaka 1941. Hii ilisababisha pia Wajerumani kuteka Yugoslaviawakiwa njiani kwenda Ugiriki.
Vita ya kidunia
Mwaka wa 1941 uliona vita kubadilika kutoka vita ya Kiulaya kuwa vita ya kidunia.
Wajerumani walishambulia Urusi wakifika hadi kando ya mji mkuu Moscow, lakini walishindwa kuiteka. Walikamata eneo lote la kusini mwa Urusi hadi milima ya Kaukazi na hadi mtoVolga.
Wajapani walishambulia Marekani pamoja na makoloni ya Waingereza na Waholanzi huko Asia. Hitler alitangaza pia vita dhidi ya Marekani akitaka kuwasaidia Wajapani ingawa Japan haikushambulia Urusi.
Katika miaka iliyofuata nguvu ya Ujerumani na Japani ilipungua. Hasa uwezo wa kiuchumi wa Marekani ulizalisha mitambo na silaha kwa mkasi usiopatikana kwa Wajerumani na Wajapan. Ukali wa utetezi wa Warusi ulichosha nguvu za Wajerumani.
Kuanzia mwaka 1943 mataifa ya ushirikiano yalianza kusogea mbele pande zote. Warusi walisukuma Wajerumani polepole warudi nyuma. Waamerika na Waingereza walipeleka wanajeshi Italia ya Kusini. Italia ilifanya mapinduzi: dikteta Mwitalia Mussolini aliondolewa madarakani na serikali mpya ilijiunga na mataifa ya ushirikiano.
Mwaka 1944 askari wa mataifa ya ushirikiano waliingia Ufaransa wakielekea Ujerumani. Wakati huohuo Warusi walisogea mbele zaidi wakikaribia mipaka ya Ujerumani. Huko AsiaJapan ilipoteza sehemu kubwa sana ya meli zake za kivita na Jeshi la Marekani lilikaribia visiwa vya Japani tayari.
Mwisho wa vita
Mwaka 1945 iliona mwisho wa vita. Mataifa mengi yaliyokuwa mbali, kama Argentina, Peru au Mongolia, yalitangaza pia hali ya vita dhidi ya Ujerumani na Japani. Pia nchi zilizowahi kushikamana na Wajerumani waligeukia mataifa ya ushirikiano. Ujerumani yenyewe ilivamiwa kutoka Magharibi na Mashariki. Warusi walifika mji mkuu wa Berlin na Adolf Hitler alijiua tarehe 30 Aprili 1945; wanajeshi wake walitia sahihi mkataba wa kusalimu amri tarehe 8-9 Mei 1945.
Wingu la kinyuklia juu ya Nagasaki tarehe 9 Agosti 1945
Huko Asia Japani iliendelea kupigana na Waamerika walioweza kufikisha ndege zao zilizobeba mabomu hadi Japani yenyewe. Mnamo Agosti 1945 Waamerika walitumia silaha mbili za kinyuklia walizokuwa nazo wakati ule na kuua watu wengi sana huko Hiroshima tarehe 6 Agosti na Nagasaki tarehe 9 Agosti 1945. Siku zilezile Warusi walianza kuwashambulia wanajeshi Wajapani huko Uchina. Haya yote yalisababisha serikali ya Japani kukubali wameshindwa wakatia sahihi mkataba wa kusalimu amri tarehe 2 Septemba 1945.
Waliokufa vitani
Kwa jumla takriban watu milioni 60 walikufa kutokana na vita hivi. Makadirio hutaja wanajeshi milioni 25 na raia milioni 35. Taifa lililopoteza watu wengi ni Urusi walipokufa kati ya milioni 20-28, idadi kubwa wakiwa raia.
Takriban watu milioni 10 waliuawa na Wajerumani au walikufa kutokana na kutendewa vibaya nje ya mapigano, kama vile milioni 6 za Wayahudi, wengine Wapoland, Warusi, Wasinti, walemavu n.k.
Umoja wa Mataifa
Tokeo moja la vita kuu ya pili ni kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa. Uliundwa 1945 kama chombo cha kuzuia vita zijazo. Kutokana na historia hii mataifa yenye nafasi za kudumu na kura ya veto katika Baraza la Usalamailitokana na mataifa washindi wa vita kuu ya pili: Marekani, Uchina, Ufaransa, Uingereza na Urusi. Kutokana na kura ya veto hawawezi kuondolewa bila kukubali wenyewe hata kama siku hizi Ufaransa na Uingereza sio tena nchi zenye nguvu sana duniani kama ilivyokuwa hapo awali.
Hivyo ieleweke kuwa chanzo kikuu cha vita hizi ni ubinafsi wa watawala hasa wale wanaojiona wana nguvu kushinda mataifa mengine. Kama watawala walivyojaribu kuunganisha nguvu ili kuwawezesha kutawala dunia kirahisi, lakini juhudi hizi zimekuwa hazizai matunda zaidi ya kuchochea uharibifu. Tangu ensi hizo, dunia watatwala wamejaribu kuunganisha dunia lakini wameshindwa. Mfano wa muungano unaodha iniwa kuwa wenye nguvu wa European Union (EU) umeishia tu kuunganisha sarafu za nchi wananchama lakini kila nchi inabaki na madara yake ya kisiasa na kiuchumi.Kama Neno la Mungu lisemavyo”….hawataungana kamwe” (Daniel 2:45).
Baada ya vita hizi za dunia na hatimaye kuanzishwa umoja wa mataifa kama njia ya kukomesha vita za kidunia, nini kinafuata?
Kwa wanafunzi wazuri wa Biblia, wanatambua kuhusu vita kuu ya Har-Magedoni ambayo ni vita kuu ya mwisho baina ya mawakala wa Shetani wakiongozwa na shetani mwenyewe dhidi ya Yesu Kristo na Kanisa lake. Na huo ndio utakuwa mwisho wa vita na uovu. Watakatifu watapewa milki ya milele ( Daniel 2:44).
Jambo la msingi kulitambua ni kwamba, kabla ya vita kuu ya Har-magedoni, kutakuwa na nguvu kubwa ambayo Biblia huita “ Mnyama” itakayotenda kinyume na mapaenzi ya mwenyezi Mungu. Kwa kushirikiana na “washirika wake” mamlaka hii iatweza kushinkiza wakazi wote wa dunia yote wamsujudu huyo mnyama na kupokea chapa ya jina lake ama hesabu ya jina lake (666) katika vipaji vya nyuso zao ama katika mikono yao ya kuume ( Ufunuo 13:15-18).
Lakini Mungu ni mwenye upendo, kabla ya kumuangamiza huyu mnyama wenye makufuru pamoja na washirika wake, anatoa wito mkuu wa onyo. Hili ni onyo kuu kupita yote yaliyokwisha kutolewa kabla. Nalo linapatikana katika kitabu cha ufunuo 14: 9,10.
“Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo”.
Maelezo haya ni ya kutisha mno na tofauti kabisa na mafungu mengine katika Biblia. Lakini yanaeleza wazi jinsi mabavyo Rehema ya Mungu itaondolewa duniani toka kwa wale ambao watamedelea kukataa mamlaka yake na kujiunga na mnyama katika ibada potofu. Ifahamike kwamba vita kuu ya mwisho itahusu utii bandia kwa mamlaka ya mnyama, ambayo mara kwa mara hutajwa katika unabii wa Biblia.Mwishoni ulimwengu utagawanyika katika makundi mawili, wale wanaomwabudu Mungu wa kweli; na wale wanaomsujudu mnyamawa ufunuo 13. Jambo la kuhoji, ni kitu gani kitasababisha mgawanyiko huu? Jibu ni rahisi sana, Nabii Yohana baada ya kueleza hatima ya watu watakaomsujudu mnyama na sanamu yake, anatoa faraja kwa wale watakaodumu kuwa waaminifu kwa Mungu wa Mbinguni. Ufunuo 14:12 “Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu”.
Hivyo suala hili linahusu utii wa amri za Mungu. Wale wasio na chapa wanaelezwa kuwa ni watiifu wa amri za Mungu, wakati wale wote wanaopokea chapa ni wale wanaovunja amri za Mungu. Jambo la kusikitisha wantheolojia wengi hasa wachungaji wamekuwa wakipuuza ujumbe uliomo katika ufunuo 14:9, 10. Hatari nkubwa ni kwamba wengi hukubali kusomewa Biblia na kupewa tafsiri potofu.Wachungaji wao huwaambia ujumbe huu sio wa kizazi hiki! Ama husema ulihusu watu wa mahali fulani huko nyuma! Hatari kubwa hii! Wengi hudai kitabu cha Ufunuo kimefungwa na ujumbe wake si wa wakati huu. Lakini hebu tuzingatie ahadi iliyomo katika kitabu hicho. Ufunuo 1:3, “Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu”. Hivyo Biblia husisitiza kuwa ujumbe wa kitabu cha ufunuo wakati wake u karibu na wala haujapitwa kama wengi wanvyopotosha.
Mada inayofuata: Washindani wawili wenye nguvu katika vita vinavyoeendelea
Karibuni sana.