Baada ya vita ya Ukraine, Nchi za Afrika zinatakiwa kupata Mateso Makali ya Kiuchumi kutoka kwa EU & USA

Baada ya vita ya Ukraine, Nchi za Afrika zinatakiwa kupata Mateso Makali ya Kiuchumi kutoka kwa EU & USA

Mleta mada kwa taarifa yako, wakati wa vita baridi ya kwanza, nchi za Afrika zilikuwa na unafuu mkubwa. Imeanza vita baridi ya pili nina uhakika, Afrika tutapumua zaidi kama viongozi wetu watatambua umuhimu wa kuhakikisha waafrika wanajitegemea kiuchumi na kijamii.
 
Wewe utakuwa mtoto na hujui historia!Kasome kisa Cha Nyerere kuwaambia watanzania wakaze Mikanda!
Israel inachofanya huko Palestina,US alichofanya huko Afghan,Yugoslav na kwingineko,ni wapi ambapo tulichagua upande?
Tuliamua hatutafungamana na upande wowote,na Huo ndio msimamo wa nchi yetu!
Hii vita imekuja imetukuta tayari tuna msimamo wetu,Wala halikuwa jambo la kwenda kutafakari!
Baada ya vita,tutashirikiana na yeyote ambaye Yuko tayari!Ambaye hataki,ruksa kuondoka!
Huko walikuwa wanafurushwa magaidi, wafadhili Ugaidi na vikundi vyao vya Ugaidi.

Sihitaji kusoma historia ya Nyerere, Rais aliyetaifisha mali za watu, Rais aliyefanya mpaka leo Tanzania wananchi wanaishi kijima, akatuachia shetani wa maendeleo CCM.
 
Watu wa green card hawawezi kukuelewa. Umeona majibu yake, Mkuu.
 
1. Unafiki wameuanza wao sisi tunamaliza, Wametutawala kimabavu, wametuua na Kutuibia Mali nyingi sana, wamevamia Nchi nyingi sana bila sababu kuiba Mali, Afghanistan, Iraq, Syria nk. nk.

2. Pili, Dunia inatakiwa iwe na Balance of Power, Africa itamsapoti yoyote atakayekua kinyume na wamagharibi Nikimaanisha Ulaya na Marekani Ili kuhakikisha kunakua na Balance of power. Kwa muda mrefu sana tumekua mateka maana hakuna anaeweza kumuwajibisha Marekani anapofanya Dhuluma. Ndo maana unaona anafanya anachotaka Duniani.

3. Tatu, Tunarudisha fadhila Kwa Urusi, wao walilisaidia sana Bara la Africa kujitawala na kupinga Ukoloni .
Point no moja, huko walifuatwa wafadhili wa Ugaidi na magaidi.

Point no mbili nakubaliana na wewe.

Point no Tatu, hata EU pamoja na kutawala tayari wamerudisha fadhila vya kutosha, USA amekuwa kimbilio la wanamageuzi/wanaharakati na Demokrasia duniani, nchi kama Afrika kusini imejengwa na makaburu pamoja na madhira yote waliyowafanyia waafrika, kwahiyo kama ni fadhila hata EU na USA walipwe fadhila kwa sababu misaada yao ndiyo inainua na kukuza uchumi wa nchi za Afrika.
 
Mleta mada kwa taarifa yako, wakati wa vita baridi ya kwanza, nchi za Afrika zilikuwa na unafuu mkubwa. Imeanza vita baridi ya pili nina uhakika, Afrika tutapumua zaidi kama viongozi wetu watatambua umuhimu wa kuhakikisha waafrika wanajitegemea kiuchumi na kijamii.
Tutapumua kivipi Wakati uchumi wetu unategemea misaada?

Unalima lakini huwezi kuprocess mwenyewe?

Una rasilimali, lakini huna teknolojia ya kuzitumia, hapo utapumua vipi?
 
Huko walikuwa wanafurushwa magaidi, wafadhili Ugaidi na vikundi vyao vya Ugaidi.

Sihitaji kusoma historia ya Nyerere, Rais aliyetaifisha mali za watu, Rais aliyefanya mpaka leo Tanzania wananchi wanaishi kijima, akatuachia shetani wa maendeleo CCM.
Unajenga hoja kitoto sana, hujakomaa kudiscuss facts na badala yake unaishia kutoa tu kauli za rejareja!

Kuhusu ugaidi, US alisema Iraq Kuna silaha za Nuclear, akavamia na hazikuwepo!
Huko Afghan, Julian Assange aliwaumbua wamarekani Kwa kutoa ushahidi wa war crimes kwenye WikiLeaks, mpaka Leo mmarekani anamtafuta Assange Kwa kutoa nyaraka hizo za Siri!

Yaani mfichua maovu ya matendo ya jeshi la US huko Afghan anatafutwa Kwa kutoa classified information! Na hapo Bado unataka Africa iwe na mtizamo kama anataka US!
Kama US alitumia kigezo Cha ugaidi, Russia yeye kasema anawafagia Nazis huko Ukraine! Kama hujui, Nazis walisababisha warusi milion 27 kuuwawa wakati wa world war 2!
 
Point no moja, huko walifuatwa wafadhili wa Ugaidi na magaidi.

Point no mbili nakubaliana na wewe.

Point no Tatu, hata EU pamoja na kutawala tayari wamerudisha fadhila vya kutosha, USA amekuwa kimbilio la wanamageuzi/wanaharakati na Demokrasia duniani, nchi kama Afrika kusini imejengwa na makaburu pamoja na madhira yote waliyowafanyia waafrika, kwahiyo kama ni fadhila hata EU na USA walipwe fadhila kwa sababu misaada yao ndiyo inainua na kukuza uchumi wa nchi za Afrika.
Tuambie kuhusu Julian Assange ambaye alitoa Siri za uhalifu wa Kivita za US nchini Afghan!Iweje leo US imtafute Ili imshughulikie Kwa kutoa Siri za jeshi la US?
 
Unajenga hoja kitoto sana,hujakomaa kudiscuss facts na badala yake unaishia kutoa tu kauli za rejareja!
Kuhusu ugaidi,US alisema Afghan Kuna silaha za Nuclear,akavamia na hazikuwepo!Julian Assange akawaumbua wamarekani Kwa kutoa ushahidi wa war crimes kwenye WikiLeaks,mpaka Leo mmarekani anamtafuta Assange Kwa kutoa nyaraka hizo za Siri!
Yaani mfichua maovu ya matendo ya jeshi la US huko Afghan anatafutwa Kwa kutoa classified information!Na hapo Bado unataka Africa iwe na mtizamo kama anataka US!
Kama US alitumia kigezo Cha ugaidi,Russia yeye kasema anawafagia Nazis huko Ukraine!Kama hujui,Nazis walisababisha warusi milion 27 kuuwawa wakati wa world war 2!
Bwana Bome-e nafurahi kuona unaendelea kujibu hoja zangu za kitoto na reja reja.

Huyo Julian Assange alikuwa kibaraka wa Urusi, kwahiyo ni lazima atafutwe popote alipo ili aje athibitishe mbele ya Mahakama.
 
Majibu yake ya kitoto sana,hajakomaa kifikra kujenga hoja na badala yake Yuko kama kifaranga Cha kuku ambacho kimempoteza mama yake!
Bwana Bome-e hakuna haja ya kupandisha mishipa ya hasira na kumwaga povu namna hii.

Umekereka na hoja za kitoto, unakaa pembeni, yaani hamna haja ya kutumia nguvu sana.
 
Point no moja, huko walifuatwa wafadhili wa Ugaidi na magaidi.

Point no mbili nakubaliana na wewe.

Point no Tatu, hata EU pamoja na kutawala tayari wamerudisha fadhila vya kutosha, USA amekuwa kimbilio la wanamageuzi/wanaharakati na Demokrasia duniani, nchi kama Afrika kusini imejengwa na makaburu pamoja na madhira yote waliyowafanyia waafrika, kwahiyo kama ni fadhila hata EU na USA walipwe fadhila kwa sababu misaada yao ndiyo inainua na kukuza uchumi wa nchi za Afrika.
1. Usichokijua ni kwamba misaada ya Tunachopewa Africa ni Robo/theluthi ya wanachoendelea Kutuibia. Pesa zote wanazotupa Africa hawatoi mifukoni mwao Bali Gawio la Fedha waliyoingiza kutokana na wizi wa Mali za Africa. Na sasahv hawaji na Bunduki Wala Vifaru, Wanatumia Ubabe wa kiuchumi walionao. Wanafanya intimidation katika Mikataba, rejea Mikataba ya EPA nk.

2. Katika Ku deal na magaidi Kuna mitandao ya Kimataifa ya Kufanya Shughuli hizo ikiwemo Interpol, U.N nk. lakini sio Uvamizi wa Nchi Moja kuivamia Nchi nyingine Kijeshi. Marekani iliivamia Iraq Kijeshi Yaani Total war Kwa kisingizio Inamiliki Mabomu ya Nuclear kitu ambacho Mpaka Leo wameshindwa kuthibisha. Nchi za Ulaya zilivamia Africa na Dunia kutafuta Raslimali Kwa Nguvu na kuua watu lakini mpaka Leo hakuna aliyethubutu kuwawajibisha. Huu ni unafki wa Hali ya Juu.
 
Bwana Bome-e nafurahi kuona unaendelea kujibu hoja zangu za kitoto na reja reja.

Huyo Julian Assange alikuwa kibaraka wa Urusi, kwahiyo ni lazima atafutwe popote alipo ili aje athibitishe mbele ya Mahakama.
Ndio maana nasema hujakomaa na uko misinformed! Julian Assange hatafutwi kuja kuthibitisha mbele ya mahakama, anatafutwa kwasababu ya kuhatarisha usalama wa US Kwa kutoa classified information!

Kwenye mashtaka 17 aliyofunguliwa, yote hayahusiani na kuthibitisha nyaraka zile kama ni aunthetic maana ni kweli they are!

Moja ya nyaraka hizo alizotoa,ni camera onboard kwenye ndege vita ambapo wanajeshi wa US wanaonekana wakishambulia raia wakiwemo watoto halafu wanajeshi hao wanasikika walisema Kwa kebehi "that's what you get for bringing a child into a war zone"!

Fanya utafute interview ya Stephen sackur na Mke wa Assange anayeitwa Stella, utajifunza mengi!
 
Bwana Bome-e hakuna haja ya kupandisha mishipa ya hasira na kumwaga povu namna hii.

Umekereka na hoja za kitoto, unakaa pembeni, yaani hamna haja ya kutumia nguvu sana.
Uko mweupe sana,ni bora ukawa msomaji zaidi kuliko mchangiaji sana Kwa mambo ambayo huna uelewa nayo!
 
1. Usichokijua ni kwamba misaada ya Tunachopewa Africa ni Robo/theluthi ya wanachoendelea Kutuibia. Pesa zote wanazotupa Africa hawatoi mifukoni mwao Bali Gawio la Fedha waliyoingiza kutokana na wizi wa Mali za Africa. Na sasahv hawaji na Bunduki Wala Vifaru, Wanatumia Ubabe wa kiuchumi walionao. Wanafanya intimidation katika Mikataba, rejea Mikataba ya EPA nk.

2. Katika Ku deal na magaidi Kuna mitandao ya Kimataifa ya Kufanya Shughuli hizo ikiwemo Interpol, U.N nk. lakini sio Uvamizi wa Nchi Moja kuivamia Nchi nyingine Kijeshi. Marekani iliivamia Iraq Kijeshi Yaani Total war Kwa kisingizio Inamiliki Mabomu ya Nuclear kitu ambacho Mpaka Leo wameshindwa kuthibisha. Nchi za Ulaya zilivamia Africa na Dunia kutafuta Raslimali Kwa Nguvu na kuua watu lakini mpaka Leo hakuna aliyethubutu kuwawajibisha. Huu ni unafki wa Hali ya Juu.
Majibu atakayokupa ni mepesi mno mpaka utaishiwa nguvu ya kumjibu!
 
Ndio maana nasema hujakomaa na uko misinformed!Julian Assange hatafutwi kuja kuthibitisha mbele ya mahakama,anatafutwa kwasababu ya kuhatarisha usalama wa US Kwa kutoa classified information!
Kwenye mashtaka 17 aliyofunguliwa,yote hayahusiani na kuthibitisha nyaraka zile kama ni aunthetic maana ni kweli they are!
Moja ya nyaraka hizo alizotoa,ni camera onboard kwenye ndege vita ambapo wanajeshi wa US wanaonekana wakishambulia raia wakiwemo watoto halafu wanajeshi hao wanasikika walisema Kwa kebehi "that's what you get for bringing a child into a war zone"!
Fanya utafute interview ya Stephen sackur na Mke wa Assange anayeitwa Stella,utajifunza mengi!
Bwana Bome-e, mashtaka 17 dhidi ya Julian Assange yamefunguliwa peponi?

Kama ni mahakamani, basi umejitoa ufahamu maksudi.
 
Huo ni unafiki kama umekukubali kushirikiana na mtu, lazima hata wakati wa shida uwe naye, ukishindwa maana yake wewe siyo rafiki wa kweli upo kwa lengo la maslahi tu.

Sasa nchi za Afrika Zinatakiwa zipunguziwe misaada kutoka US& EU, Russia naye yupo ataziba gap. Unafiki haukubariki kamwe.
Russia ana pesa gani za kutoa misaada ili hali nchi yake ina watu ni masikini kama huku kwetu. Bado hapo ana vikwazo vya kufa mtu.
 
Vita ya Ukraine endapo itamalizika salama nchi za Afrika zinatakiwa kupata mateso makali kwa sababu zimeonekana Kumuunga mkono dikteita Putin dhidi ya uvamizi wake kwa nchi ya Ukraine.

Nchi za Afrika zikiongozwa na Senegal, Afrika kusini, Mali, Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Nigeria, zinatakiwa kukatiwa misaada yote ya kiuchumi kuanzia elimu, afya, miundombinu, kupambana na Ugaidi, Njaa, ulinzi ili zitie adabu na iwe fundisho kwa watu wote Wanaosapoti madikteita duniani.

IMF & WB zinatakiwa kupunguza mikopo kabisa kwa nchi za Afrika ili zijitegemee au zikakopeshwe na Bank of Russia na China.

Misaada ya Vifaa tiba, madawa, teknolojia na mingineyo ya taasisi mabali mbali (USAIDS, ICAP, MDH , WORLD VISION, TASAF n.k) za kupambana na magonjwa hatari kama ukimwi, cancer, kisukari, pressure, ini, figo, Malaria inatakiwa kupunguzwa ili nchi za Afrika zipate akili.

Nchi zote zilizo piga kura ya hapana kwa Urusi, zinatakiwa kukatiwa misaada yote moja kwa moja ili zikafadhiliwe na Urusi.

Nchi zote ambazo hazikupiga kura zikiongozwa na Tanzania, zinapaswa kupunguziwa misaada kwani kutopiga kura ni kuogopa na ina maanisha wanakubaliana na Putin anachokifanya Ukraine.

Rais Ramaphosa, Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Rais wa Cameroon, Rais wa Senegal, Rais wa Nigeria hawatakiwi kuendelea kubaki madarakani kwa sababu wanamuunga mkono Putin.

USA & EU zinatakiwa kukata kabisa misaada kwenye nchi za Kiislamu zote duniani, kwani nchi hizo zinamuunga mkono Putin na zinajinasibu kuwa na utajiri wa mafuta, Putin atazipatia misaada.

Baada ya hatua hizi kuchukuliwa nchi zote zinazosapoti udikteita zitakuwa zimepata somo.

Bara la Afrika linatakiwa liendelee kubaki kwenye lindi la umasikini kwa sababu viongozi wa nchi za Afrika ni wanafiki na waliowengi wanapenda udikteita na hawako tayari kuleta mageuzi ya haki kwa ajili ya maendeleo ya bara la Afrika.

View attachment 2270692
Hujitambui hapa umeandika upuuzi Tu.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
1. Usichokijua ni kwamba misaada ya Tunachopewa Africa ni Robo/theluthi ya wanachoendelea Kutuibia. Pesa zote wanazotupa Africa hawatoi mifukoni mwao Bali Gawio la Fedha waliyoingiza kutokana na wizi wa Mali za Africa. Na sasahv hawaji na Bunduki Wala Vifaru, Wanatumia Ubabe wa kiuchumi walionao. Wanafanya intimidation katika Mikataba, rejea Mikataba ya EPA nk.

2. Katika Ku deal na magaidi Kuna mitandao ya Kimataifa ya Kufanya Shughuli hizo ikiwemo Interpol, U.N nk. lakini sio Uvamizi wa Nchi Moja kuivamia Nchi nyingine Kijeshi. Marekani iliivamia Iraq Kijeshi Yaani Total war Kwa kisingizio Inamiliki Mabomu ya Nuclear kitu ambacho Mpaka Leo wameshindwa kuthibisha. Nchi za Ulaya zilivamia Africa na Dunia kutafuta Raslimali Kwa Nguvu na kuua watu lakini mpaka Leo hakuna aliyethubutu kuwawajibisha. Huu ni unafki wa Hali ya Juu.
Afrika ilikuwa primitive hizo rasilimali walikuwa hawazijuhi, kuja kwa wakoloni ndiyo wakaambiwa na kuweza kutambua thamani ya rasilimali hizo, kwahiyo hata kama wasingekuja wakoloni bado Afrika ingekuwa masikini wakutupwa maana hizo rasilimali hata matumizi yake walikuwa hawana.

Mpaka sasa Afrika imejaa rasilimali za kutosha karibia kila nchi lakini zimewashinda kutumia kwa hawana teknolojia ya kutosha ya kuwafanya wao wenyewe wazisimamie na wanufaike nazo.

Ni sawa umenunua gari alafu hujuhi kuliendesha, umelipaki tu nyumbani kwako unasubiri aje mtu anayejua kuendesha gari ndo akuendeshe.

Kwahiyo kuwa na rasilimali alafu huna teknolojia ya kutumia ili unufaike nazo, hizo mali ni useless.
 
Back
Top Bottom