Baada ya Vyombo vya Kikatiba kushindwa kusimama kwenye nafasi zao hatimaye TLS yafanikiwa kuwa chombo pekee kinachosimamia misingi ya Kikatiba

Kikwete alikuwa mwana demokrasia kweli ila tabia za kutoheshimu Katiba na mifumo ya Katiba zilianza kuota mizizi kipindi chake.

mbona kama ni contradictory, kama alikuwa mwana demojrasia iweje tena awe na “tabia za kutokuheshimu katiba”?
 
mbona kama ni contradictory, kama alikuwa mwana demojrasia iweje tena awe na “tabia za kutokuheshimu katiba”?
Sahihi kabisa. Ila kuna maeneo hakufuata misingi ya Katiba
 
Mahakama ilijizika pale walipokubali kuwekewa Sheria kuruhusu Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa kuwa sehemu ya kamati ya nidhamu kwa Mahakimu. Palee Mahakama ndo walijipiga risasi rasmi.
Mhimili mwingine umejichimbia zaidi.
 
Inashangaza kuona lichama likubwa kama chama cha walimu pamoja na ukubwa wote huo eti wanateswa na kikokotoo, chama cha wafanyakazi, butuu, tumebaki na TLS, hongera sana TLS
 
Inashangaza kuona lichama likubwa kama chama cha walimu pamoja na ukubwa wote huo eti wanateswa na kikokotoo, chama cha wafanyakazi, butuu, tumebaki na TLS, hongera sana TLS
TLS wanasimama nafasi waliyotakiwa kusimama Mahakama, Bunge, Tume ya Maadili, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Hivi vyombo vya Kikatiba vingesimama katika nafasi yake leo wala TLS isingekuwa maarufu!
 
Nakuunga mkono mwana CCM katika kudai HAKI na Katiba mpya.

Katiba mpya ni hitaji la wote bila kujali vyama, dini, kabila kipato nk nk.

Ubarikiwe
 
Nakuunga mkono mwana CCM katika kudai HAKI na Katiba mpya.

Katiba mpya ni hitaji la wote bila kujali vyama, dini, kabila kipato nk nk.

Ubarikiwe
Bado tupo wana CCM ambao ni sober. Tunaangalia maslahi ya nchi na wananchi. Sio maslahi ya kikundi cha watu wachache!
 
Well said
 
Baada ya ccm kuanza kupoteza ushawishi kwa umma, ndio tulianza kuona kwa uwazi hivyo vyombo vya kikatiba kuacha kutenda kwa mujibu wa katiba, na kuanza kufanya kazi ya kuhakikisha ccm inabaki madarakani kwa shuruti.

Na kwa jinsi ilivyo sitegemei kuona hivyo vyombo vya kikatiba vikirejea katika misingi yake iwapo ccm itaendelea kubaki madarakani. Bila machafuko ama mapinduzi ya kijeshi, tusitegemee hivyo vyombo kufanya kwa weledi tena.
 
Hadi itokee uchaguzi wananchi wanasimamia matokeo ya uchaguzi ndio watapata akili. Chama kile kilishajua kwa uchaguzi wa haki hawashindi.
 
Chama changu CCM kinakosea sana kuangalia kwanza maslahi yake badala ya maslahi ya Taifa. Na wasipodhibitiwa na vyombo vya dola wanaweza kuja kulipasua hili taifa huko mbeleni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…