Baada ya wamachinga, malori Kariakoo ni shida mpya

Baada ya wamachinga, malori Kariakoo ni shida mpya

pye Chang shen

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Posts
11,422
Reaction score
6,108
Mamlaka zisipoliangalia hili kwa sasa basi baadae itakuja kuwa ngumu kama ilivyokuwa kwa wamachinga.

Mitaa husika hasa ni mtaa wa agrey, masasi, magila, narun'gombe na tandamti, yote ni kati ya mtaa wa ndanda na muheza, hapo kuna kero ya kufa mtu kwa wakazi wa maeneo hayo na hata wapita njia, ukitilia maanani hizo ndio njia kubwa kwa sasa ili kuipata barabara ya uhuru kwa waendao ilala na buguruni hadi tabata na viunga vyake.

Mkuu wa wilaya tembelea hayo maeneo ujionee mwenyewe kwani diwani ameshindwa katika hili, viofisi vya usafirishaji vimewekwa hadi barabarani.

Natabiri kero hii itashinda hata wamachinga kwa uharibifu wa barabara ambazo zote ni mpya ila hazina muda kwani milori yenyewe ni ile misemitrela.

Kila mdau mwenye mapenzi na inchi alisemee hili huku ni kufuja fedha bure sio kwa uharibifu huu wa barabara
 
Kwa hiyo malori wala kirukuu zisije Kariako kupakia bidhaa?

Hizo bidhaa zina miguu kwamba zimefika hapo zenyewe na zikitaka kwenda Congo zitatembea zenyewe?

Dah wabongo!
 
Kwa hiyo malori wala kirukuu zisije Kariako kupakia bidhaa?

Hizo bidhaa zina miguu kwamba zimefika hapo zenyewe na zikitaka kwenda Congo zitatembea zenyewe?

Dah wabongo!
Hatujasema kirikuu wala canter,
Ni masemi trailer na mapulling ndio tumetaja,
Yanaziba njia na kuharibuvbarabara pia
Canter, fuso na kirikuu hazina madhara
 
Hii issue siyo ya kudharau, naamini iko siku madhara makubwa yatatokea baina ya malori na either waendesha gari ndogo au watumiaji wengine wa barabara, haiwezekani mtu afunge njia akipakia mizigo kisa analipia posho au rushwa ya 20,000 au 50,000 sijui kima sahihi hjku wengine wakuteseka barabarani
 
Diwani wa hii kata ya misheni kota ameshindwa kabisa hii kazi, haimtoshi viatu ni vikubwa,
Malori ni kero mpya kariakoo serikali angalieni hili, mimi na wenzangu wengi tu ni watumiaji mkubwa wa hii barabara tunakuwa napata changamoto sana, msingoje maafa yatokee
 
Anaejua anifundishe,
Nataka kuweka hapa picha za malori jinsi yalivyofunga barabara na pia picha za gari ya halmashauri ya jiji wakichukua posho na kuwacha malori yaendelee kuharibu barabara zetu,
Mie mwenzenu sina ujuzi huo najua kuandika tu
 
Kweni hawajapangiwa muda maalum wa Loading na offloading?.
Aah wapi!
Saa mbili asubuhi ngoma tayari zipo ndani ya kariakoo zimeshafunga baadhi ya baeabara,
Yaani bandika bandua ikitoka hili linakuja kubwa zaidi ya hilo mpaka saa sita usiku
Nasikia kila gari wahusika wanachukua 20,000 mpaka 50,000 iki wasisumbuliwe na huku wanasjmbua watumiaji wengine wa barabara yaani hili jiji watu wanakula kupita kiasi bila kujali maisha ya raia wao
 
Wajenge pale jangwani kama ilivyo kwa Machinga ambao watajengewa.Mizigo ishushwe pale wafanyabiashara waje wabebe wenyewe vichwani.
Wasilite utani kuna siku lori litakurupuka lije lilete headline

Kule kuwe kweupe..na nyie mnaoenda kununua mpaki Jangwani kusudi kule waonekane watu na maduka tu.
#Mawazo ya Mtanzania huru.
 
Authorities waweke utaratibu maana Kariakoo ni Soko la Kimataifa,Wageni wengi wanafunga mzigo,wanapakia kwenye Malori makubwa na kupeleka kwenye Mataifa yao,
Pawekwe utaratibu ambao hautawaathiri Wafanyabiashara,Watembea kwa miguu,na Wasafirishaji wa Mizigo mizito Win Win kwa kila mmoja.
 
Ni wazo zuri
Ila kubeba kichwani haiwezekani,
Ni canter na kirikuu tu ziruhusiwe kuingia kariakoo
Hili ndio suluhisho na wahusika wanajua ila nadhani utekeleaji ndio shida hapa
Sijui kwa ajili ya kipato au makusanyo
 
Hilo litawezekana tu kwa kutenga maeneo ya malori makubwa nje ya nchi na canter ndio zisombe na kupeleka huko kwenye malori
Lakini kuruhusu malori kariakoo ni uharibifu naweza kusema kuzidi uhujumu uchumi wa kuharibu barabara
 
Ni wazo zuri
Ila kubeba kichwani haiwezekani,
Ni canter na kirikuu tu ziruhusiwe kuingia kariakoo
Hili ndio suluhisho na wahusika wanajua ila nadhani utekeleaji ndio shida hapa
Sijui kwa ajili ya kipato au makusanyo
Asante Mkuu kwa ustaarabu wa Bongo ulivyo mbovu hata Virikuu vitakuwa kero kubwa mno.

Vitakuwa kama nyuki kule katikati ya mji.Turudi tu zama za ujima..akili ikikaa sawa.Lifanyike unalosema
 
Back
Top Bottom