Baada ya Watuhumiwa wawili wa wizi kuuliwa na Wananchi, Polisi Arusha yawaonya wanaojichukulia sheria Mkononi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2025-03-13 at 14.14.23_93aaa4de.jpg

Jeshi la Polisi Mkoa watu Arusha limesema kuwa tarehe 13, machi,2025 muda wa saa 12:30 asubuhi huko katika maeneo ya mtaa wa njiro ndogo kata ya sokoni one katika halimashauri ya jiji la Arusha watu wawili wasiofahamika majina wanaume wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 28 walifariki dunia baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao na watu wasiofahamika huku likawaonya watu wanajichukulia sheria Mkononi.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisii (SACP) Justine Masejo amesema kuwa Watu hao walishambuliwa mara baada ya kuiba pikipiki iliyokuwa imeegeshwa Jirani na kituo cha mafuta cha simba oil kilichopo eneo la njiro ndogo ambapo pia walichoma pikipiki yenye namba ya usajili Mc 438 ESG aina ya Sinoray iliyokuwa inatumiwa na watu hao.
Justine Masejo.jpg

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisii (SACP) Justine Masejo
Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi Mkoani humo linaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hili ili kuibaini chanzo cha tukio na hatua zitachukuliwa kwa wale watakaobainika kuhusika na tukio hili.

SACP Masejo amebainisha kuwa miili ya marehemu imehifadhiwa katika kituo cha Afya Murieti kwa ajili ya utambuzi na uchunguzi wa daktari.

Kamanda Masejo Pia amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawaonya watu wanaoendelea kujichukulia sheria mkononi kuwa waache mara moja na badala yake watoe taarifa za uhalifu na wahalifu ili hatua sstahiki ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria.
 
View attachment 3269094

Sipendi wenzio,ila Wakati mwingine tunawaua hata watu wasiokuwa wenzio kwa kupiga tuu kelele za mwizi,mwizi!,Noma sana hii.
 
Wananchi nao hawana akili hao wezi badala wawakamate wawahoji wawafikishe polisi wanawaua na pikipiki yao je kama hio pikipiki walioichoma niyawizi je inakuaje
 
Kama wamedakwa na mzigo wa wizi ni kuchoma moto tu hamna mda kama hutaki acha uwizi
 
Back
Top Bottom