Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Baada ya mastaa wa Bongo, Wema Sepetu, Zuchu, Maua Sama kupata watoto hivi karibuni, mwimbaji wa Marekani, Ciara (40) na mumewe Russell Wilson wanatarajia mtoto mwingine, ikiwa ni mtoto wa tano kwa mwimbaji huyo na wa nne katika ndoa yao.
Ciara ametangaza habari hizi njema siku ya jana Jumapili kupitia picha na video fupi zikimwonesha akiwa na tumbo la uzazi, huku akiongeza maelezo yanayosema, "Mtu mmoja zaidi wa kumpenda ".
Tangazo hilo pia limehusisha majina ya watoto wao Future, Sienna, Win, na Amora yakiwa yameandikwa kwenye nguo zilizotundikwa, pamoja na vazi dogo la mtoto mchanga kuwakilisha mwanafamilia wao mpya.
Wawili hawa walifunga ndoa mwaka 2016 na walisherehekea miaka 10 ya ndoa yao hivi karibuni, hata hivyo bado hawajataja jinsia ya mtoto huyo wala tarehe anayotarajiwa kuzaliwa.