Hivi ni nani aliyewadanganya wakristo kuwa Yesu amezaliwa katika hori la kulishia Ng'ombe?
Mbona hili andiko linapingana na huo uzushi
Luka 2:7
akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Andiko linasema amemlaza katika hori ya kulia Ng'ombe na sio kamzaa katika hori ya kulia Ng'ombe
Pia andiko linasema amemlaza hapo katika hori ya kulia Ng'ombe Kwa sababu alikosa nafasi katika nyumba ya wageni
Maana yake ni kwamba kama angepata nafasi katika nyumba ya wageni hapo katika hori ya kulia Ng'ombe Mariam na mwanawe Yesu wasinge fika
Nyinyi wagalatia sijui huwa mnakwama wapi hadi mnadanganywa kirahisi hivi