Baada ya zama za kubebwa na Yamoto Band kupita, Enock Bella atoa wimbo mbaya kupitiliza

Baada ya zama za kubebwa na Yamoto Band kupita, Enock Bella atoa wimbo mbaya kupitiliza

Sipendi kuchuma dhambi kwa Mwenyezi Mungu wala kuwa ' Mnafiki ' ukweli ni kwamba Wimbo ni mzuri tena sana tu na unachezeka isipokuwa nadhani alimpata Director mbaya wa Video kwani kuna baadhi ya ' scene ' hazikupangiwa vyema na Wahusika waliokuwepo hasa huyo Video Queen aliyemtumua alikuwa hachangamki na ni kama vile anajishtukia.

Kuhusu sauti tena nadhani sauti yake ameitumia vile inavyotakiwa na imekaa mule mule. Huyu Kijana kama akiendelea kujipanga vizuri na kurekebisha tu baadhi ya changamoto ndogo ndogo na akatulia namuona ni mzuri kuliko hata Dogo Aslay isipokuwa tu anazidiwa nae ' Kinyota ' tu.

Mwisho nitoe tu ushauri nadhani tujifunze ustaarabu wa kuwatia moyo hawa Wasanii wetu kuliko kuwaponda kwani nakumbuka kwamba hata wakati Diamond anaanza kuimba na kutoa ile Single yake ya Kwanza alipondwa mno ila hakukata tamaa akapambana na hatimaye leo anafanya vizuri huku akiwa na Pesa pamoja na Utajiri ambao kuna uwezekano mkubwa Mimi na Mleta mada hata tukisema tuchanganye Pesa zetu na tuuze mali zetu bado hatuwezi hata kufikia tu robo tatu ya Pesa alizonazo Diamond Platinum.

Kwa taarifa yenu ni kwamba huyu Msanii wa Kikongo Christian Bella ambaye huku Tanzania anaonekana ni ' Mfalme ' wa muziki na masauti wakati alipokuwa akiimba katika Bendi ya Koffi Olomide ya Quarter Latin pamoja na Kaka yake mkubwa alionekana hafai na hadi kudhihakiwa na Wakongo mpaka akaamua kuondoka huko na kuja Tanzania ambapo alikutana na Wenzake akina Tarsis Masela wakaanzisha Bendi yao ya AKUDO Impact ambapo kupitia hiyo Bendi ndipo ' nyota ' yake ikaanza kuwaka vyema na hadi leo ni Msanii mkubwa tu hapa nchini Tanzania.

Achilia mbali huyu Christian Bella huko nchini Congo DR mara baada ya huyu Mwanamuziki Kipenzi kwa sasa Fally Ipupa ' Dicaprio ' kuhama / kutoka kwa katika Bendi ya Koffi Olomide na kutoa ile album yake ya Kwanza ya ' Bakandja ' alichekwa na kudhihakiwa mno kwamba hajui na asingeweza kushindana na Mpinzani wake mkubwa Msanii Ferre Gola na alipokuja kutoa sasa album yake ya pili iitwayo Droit Chemen ndipo Wakongo na hasa wale ' Critics ' na ' Haters ' wake walipompigia ' Salute ' na leo amekuwa ndiyo Msanii Tajiri wa Kizazi cha Tatu cha nchini Kongo achilia kile cha pili cha akina Koffi Olomide, JB Mpiana ,Ngiama Makanda Werrason, Kanda Bongoman na Aurlus Mabele huku Kizazi cha Kwanza kikiwa ni kile kile cha akina Marehemu Luanzo Makiadi Franco, Yoka Longo, Madilu System, Tabu Ley ' Roucherou ' na Pepe Kalle.

Namtabiria makubwa sana ' Kimuziki ' huyu Kijana Enock Bella na namwomba Mwenyezi Mungu ampe ambariki, awe mvumilivu, asikate tamaa kwani naona taa ya Kijani na ya Kimafanikio Kwake inakuja na kuna siku huyu huyu aliyemponda vibaya leo atakuja kumpigia ' salute ' tena kubwa sana.

Yangu ni hayo tu.
Excellent brother.....ila mtoa posti kanikela roho sana ...anamponda tuu huyu DOGO pasipokumshauri....
 
Ama kweli majumba makubwa hustiri mambo hii kauli kwa namna fulani inashibahiana na hali inayomkuta sasa msanii Enock Bella

Huyu kijana kipindi yupo yamoto band aliwahi kutamba sana na sauti yake nzito na tungo tata zilizowachanganya vilivyo akina dada.

Mwanzoni huyu kijana alikuwa ni dancer tu wakawaida ila mkubwa fella akatumia kila aina ya ushawishi ili huyu jamaa naye aimbe kama wenzake kwenye kundi na akamsifia vilivyo kwamba sauti yake itaziba pengo la marehemu Muhiddin Gurumo lakini siku zote bwana mtu kama huna kipaji huna tu hata ufanye nini.

Alipokuwa Yamoto alijificha nyuma ya wenzake na kuimba maneno mawili matatu na hakuweza kugundulika kirahisi kwamba jamaa ni debe tupu ila tangu kundi livunjike huyu jamaa ana hali mbaya sana kimuziki na hilo limejidhihirisha mara baada ya kutoa wimbo kama solo artist uitwao Sauda.

Aisee huu wimbo ni mbaya mbaya mbayaa kupita maelezo hausikiliziki hauchezeki kwa kifupi hauvutii kabisa au kwa maneno mengine naweza kusema huu ndio wimbo mbovu zaidi kwa mwaka huu 2017/2018.

Jamaa bora aangalie tu ustaarabu mwengine mziki hawezi.

Huko IG watu wachache wamejitokeza kumsapoti lakini wapi ngoma haisapotiki ,imedoda.

View attachment 623529Pole sana Enock Bela tafuta kazi nyingine tu huku kwenye mziki unatukera huna ulichobakiza.
Nyimbo n nzuri acha roho mbaya
 
We jamaa unaroho mbaya, tukupe tuzo ya uchukiaji. Wimbo ni mzuri sikutegemea
 
Wimbo mzuri,na hata video ni nzuri pia.Watanzania tujifunze kuvipenda vya nyumbani.Na pia kuwapa ushauri chanya wanaovifanya.Mtoa mada,umekosea sana.Kumbuka sio kila wimbo unaweza ukaupenda,au ukawa kwenye mahadhi ya kile unachotarajia kukisikia.Acha wanaopenda muziki mzuri,wapate ladha wanayoitaka.Wewe subiri ,ladha za muziki unazozitaka.Chuki hazina maana.
 
Kama sijui mziki na iwe hivyo, ila wimbo mzuri nimemsikiliza mara 3
nimependa wimbo na sauti pia
 
Mtoa post utakuwa umegombana na jamaaa so,umeamua kuja kumchafua huku kwenye mitandao,acha kjana atafute riziki,kwani hao wengine wanaimba vitu vya maaana?
 
Huyu mleta mada inaonekana ni masikini wa fikra na kipato. Huwezi kuwa mwanaume mnafiki na mmbeya kama huyu. Mwenzio yuko kwenye utafutaji wewe unamkatisha tamaa na kushawishi wateja wasione hata bidhaa yake. Mimi siyo mpenzi wa bongo fleva ila sipendi wachawi
 
Acha ushamba na wivu wa kijinga.usituaminishe kuwa wewe ndio quality assuarance wa nyimbo za wenzio imba wewe tukusikie....
 
Mleta mada umewahi kushika mic na kuimba angalau kwenye birthday party ya jirani yako au ndugu yako?!

Upondaji wako upo too personal! Kwamba eti Fella alifanya kila ushawishi ili mradi tu aimbe ukijaribu kuonesha hakutakiwa kuwa mwimbaji hata huko Yamoto unaonekana wazi huufahamu muziki na mipangilio yake na umuhimu wa mtu kama Enock pale Yamoto!!

Hata hii single yake, kabla ya kukashifu kwa kiwango kikubwa kiasi hicho ulitakiwa kwanza kufahamu taste yako kwenye muziki hasa ni nini!
 
Back
Top Bottom