Baadhi ya bidhaa za machinga zifuatiliwe kwa umakini

Baadhi ya bidhaa za machinga zifuatiliwe kwa umakini

mtingi1

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2020
Posts
957
Reaction score
935
Wadau Habari,

Niende moja kwa moja kwenye mada, juzi nikiwa kwenye mizunguko ya kutafuta shilingi jijini Dar (coz nowadays siishi Dar) nikapita mtaa mmoja wenye machinga wengi usiku kama saa moja na kidogo hivi.

Nikaona jamaa anatangaza, “sabuni sabuni huku jero huku mia saba” sasa kilichonishangaza ni bei kuwa ndogo maana sabuni zenyewe zilikuwa Dettol

Ikabidi ninunue dettol ya jero(500) ili kujua imekuwaje leo ikauzwa bei hiyo. Nilipoiangalia kwenye tarehe ya ku expire nikakuta ilisha expire toka mwaka jana.

Angalizo:

Unaponunua bidhaa kwa matumizi ya mwili wako kutoka kwa machinga kwa bei rahisi zaidi tafadhali zingatia kuangalia expiry date.
Pia serikali itusaidie kutoa elimu kwa machinga has a wauza sabuni na mafuta ili watambue umuhimu wa kuilinda jamii yetu.

IMG_6482.jpg
 
Mzee baba kwa kifupi ni kwamba umekutana na vijana wa mjini, full stop...
 
Wadau Habari,

Niende moja kwa moja kwenye mada, juzi nikiwa kwenye mizunguko ya kutafuta shilingi jijini Dar (coz nowadays siishi Dar) nikapita mtaa mmoja wenye machinga wengi usiku kama saa moja na kidogo hivi.
Unaponunua bidhaa kwa matumizi ya mwili wako kutoka kwa machinga kwa bei rahisi zaidi tafadhali zingatia kuangalia expiry date.
Pia serikali itusaidie kutoa elimu kwa machinga has a wauza sabuni na mafuta ili watambue umuhimu wa kuilinda jamii yetu
 
mbona naona expire date ni 2024 au
Kuna ujanja hapo. Hiyo namba ya mwisho ni 1 ila wameweka dots ionekane kama namba 4. Ila namba nne haina kitako au mstari wa chini, lakini namba 1 ina mstari wa chini. Hivyo hiyo ni namba 1 ila ukiangalia unaweza kusema ni namba 4
Cc: Mshana Jr
 
Wadau Habari,

Niende moja kwa moja kwenye mada, juzi nikiwa kwenye mizunguko ya kutafuta shilingi jijini Dar (coz nowadays siishi Dar) nikapita mtaa mmoja wenye machinga wengi usiku kama saa moja na kidogo hivi.
Kwa masikini wa hali ya chini hata kuoga kwa dettol iliyoexpire bado ni anasa
 
Back
Top Bottom