Baadhi ya Daladala Mwanza wasitisha huduma wakisubiri kauli ya Serikali kupandisha nauli

Baadhi ya Daladala Mwanza wasitisha huduma wakisubiri kauli ya Serikali kupandisha nauli

Mafuta yakishuka je, na wao watashusha nauli..??
 
safi sana, bado Daslamu
Hilo suala linaniudhi kinoma sasa nauli kupanda ya nini wakati mafuta ni yale yale imeongezeka buku tu kwani buku ndio ya kuongeza nauli si wavumilie hii vita sio ya milele, mimi naingia kwenye gari natakiwa kulipa let say 1500 natoa 1000 namwambia kondaee mimi leo jero sina anakua mkali mwanzoni ila mwishoni anapotezea kwa maana anaelewa hali halisi ilivyo nakwea ndinga safari inaendelea kwa hio hao jamaa waingia kwenye viatu vya wananchi wa hali ya chini wawaone wakiwapandishia nauli maisha yao yatakuaje?
 
mda wa LATRA kuleta basi zao kisha watoze bei za awali
 
Kuna vitu kadhaa navibaini kwenye video hii.
1. Kwa nini hakuna mdau mwingine aliyehojiwa?
2. Siku hizi wafanyakazi wa daladala wakiacha kazi, wanakenda kuaga ofisi za chama?
3. Kumbe wafabyakazi wa daladala ni mafundi na saidia fundi? Kwa hiyo kwenye ujenzi bei ya kutwa imepungua?
4. Ukiangalia video haina mahusiiano na maelezo. Anaonekana mpiga debe akishawishi abiria wapande basi lake, kwanini na magari 400, hayapo barabarani?

5. Hawa wapiga debe malipo yao pia yamepanda? Kwa siku kiasi gani kinawalipa hawa?
Mwisho, niwapongeze kwa kuanza kupeleka daladala njia ya Bulale- Buhongwa- Posta.
Ila kweli mafuta yamepanda, hili halina ubishi.
 
Back
Top Bottom