KERO Baadhi ya kada tulizofanya usaili Taasisi ya Afya Muhimbili hatujaitwa hadi sasa, nini kinaendelea?

KERO Baadhi ya kada tulizofanya usaili Taasisi ya Afya Muhimbili hatujaitwa hadi sasa, nini kinaendelea?

  • Thread starter Thread starter Anonymous (9d66)
  • Start date Start date
  • Tags Tags
    kazini
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba kuwasilisha kero kuhusu mchakato wa ajira katika Taasisi ya Afya Muhimbili. Tulifanya usaili wa nafasi mbalimbali, lakini hadi sasa imepita miezi kadhaa bila kuitwa kazini, huku mwaka ukiendelea kumalizika.

Kinachotushangaza ni kwamba kada nyingine zilizofanya usaili katika taasisi hiyo hiyo tayari zimeitwa kazini, lakini sisi bado hatujapata taarifa yoyote kuhusu hatua iliyofikiwa au hatma ya mchakato wetu.

Tulitumia gharama kubwa za usafiri kwenda na kurudi kwenye usaili, hivyo tunaomba mamlaka husika itoe ufafanuzi kuhusu mchakato huu. Kama bado hawakuwa tayari kuajiri, ingekuwa vyema kutoa taarifa mapema ili waombaji wajue hali halisi.

Soma Pia: Watumishi wa afya wa Wilaya ya Siha tuliajiriwa 2024, hadi sasa hatijathibitishwa kazini


Pia tunaomba kuwepo kwa uwazi kuhusu matokeo ya usaili huo ili kujua waliofaulu na hatua zinazofuata.
 
Tumefanya usaili katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) tangu mwezi Aprili, lakini hadi leo bado hatujaitwa kazini.

Cha kushangaza, waombaji wa kada nyingine tulioufanya nao usaili wameanza kuitwa kazini tangu mwezi Juni, huku sisi bado hatujapewa taarifa yoyote kuhusu hatma ya usaili wetu.

Kama mchakato wa ajira haukuwa tayari kuendelea, ingekuwa vyema waombaji tusiitwe kwenye usaili mapema. Tumetumia muda, gharama na nguvu kushiriki katika usaili huo, hivyo tunaomba MOI itoe ufafanuzi kuhusu hatua iliyofikiwa na lini tunatarajia kupata majibu kuhusu ajira hizo.
 
Back
Top Bottom