Tumefanya usaili katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) tangu mwezi Aprili, lakini hadi leo bado hatujaitwa kazini.
Cha kushangaza, waombaji wa kada nyingine tulioufanya nao usaili wameanza kuitwa kazini tangu mwezi Juni, huku sisi bado hatujapewa taarifa yoyote kuhusu hatma ya usaili wetu.
Kama mchakato wa ajira haukuwa tayari kuendelea, ingekuwa vyema waombaji tusiitwe kwenye usaili mapema. Tumetumia muda, gharama na nguvu kushiriki katika usaili huo, hivyo tunaomba MOI itoe ufafanuzi kuhusu hatua iliyofikiwa na lini tunatarajia kupata majibu kuhusu ajira hizo.