MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Mtu anakuja kwako na kuanza kutamani vitu kisha kuchukua haijakaa poa. Mimi nilikuwa na track suit yangu nzuri sana ya bei mbaya ila tayari wameshachukua.
Mmoja alichukua jacket na mwingine akachukua track ya chini. Ni kama waligawana. Tshirts kadhaa pia zimechukuliwa.
Majuzi hapa nilinunua blender baada ya kuona ni bora nijitengenezee juice. Bahati mbaya kutokana na ratiba zangu za kuondoka mapema na kurudi usiku nikawa sijaitumia kabisa. Mdada alitaka aondoke nayo ikiwa ndani ya box sijafungua. Hii sio sawa.
Ninajua hali ni ngumu ila mjikaze mnapowatembelea watu wenu. Pia mkija njooni na vitu kama tray la mayai, kuku, hata debe la mpunga ni sawa, kinachobebeka kutoka huko kwenu njoo nacho.