DOKEZO Baadhi ya maafisa wa serikali wanadhulumu sana watu kwa kigezo cha "kutekeleza majukumu ya kikazi"

DOKEZO Baadhi ya maafisa wa serikali wanadhulumu sana watu kwa kigezo cha "kutekeleza majukumu ya kikazi"

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Trainee

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
3,118
Reaction score
4,238
Nianze na tukio lililotokea juzi na likanihuzunisha mno. Watu wa maliasili wamepita barabara ya Nangurukuru-Liwale wakakusanya na kuchukua mkaa wa walalahoi wote wanaouza mkaa barabarani, wengi ni wanawake walioporwa mkaa wao aisee wamelalamika mno!

Tukibaki na maliasili haohao, mtu akikutwa kwenye gari na kidumu Cha asali (5L) eti wanaichukua; chumvi, vifaa vya mbao, nyama, nk vyote wanachukua. Ajabu ni kwamba ukibeba chupa 5 za Lita mojamoja za asali kutoka supermarket hawachukui!

Polisi wao ndiyo funga kazi aisee sijui ni kipi wanakiacha katika operesheni zao... Yaani wakikosa hela wako radhi hata ugali wachukue!

Sina nia ya kuwafundisha namna ya utendaji kazi lakini naumia kuona maumivu wanayowaachia watu huku mtaani. Mfano wale wamama wa mkaa unachukua mtaji wao wote sasa unafikiri ndiyo wataacha hiyo kazi?

Hivi hakuna njia nyingne ya kudili na watu kwenye kazi zenu zaidi ya kuwanyang'anya vitu vyao?

Yaleyale ya polisi kujazana kwenye difenda kwenda kutimua watu waliokusanyika kipindi cha corona
 
Mkuu kufanya chochote bila kibali maalumu ujue hayo ni magendo. Kwenye mishe za magendo hakunaga huruma
 
Mkuu kufanya chochote bila kibali maalumu ujue hayo ni magendo. Kwenye mishe za magendo hakunaga huruma
Dah, sawa

Inabidi nikubali tu maana sina elimu nalo hilo jambo lakini watu wanaumia sana
 
Dah, sawa

Inabidi nikubali tu maana sina elimu nalo hilo jambo lakini watu wanaumia sana
Ni Ile kukosa ubinadam tu ila kubeba Ile mikaa barabaran hasa ukikuta ni ya wamama dah lazima uingie Imani. Hawatafuti hela za kutajirika ni za kula tu
 
Hoja kuu hapo..Baada ya kukamata hivo vitu wanavipeka wapi? au wanapeleka kutumia na familia, Ndugu na Jamaa? Nani anawafatilia wanapokamata na wanapokabidhi? Aiseee ! KATIBA MPYA haikwepeki.
 
Wanawachekea huko,.wajaribu kwetu watakipata cha kuwasimulia wanao watuma na ndugu zao.
 
Kukata miti bila kibali hairuhusiwi

Polisi kuchukua na kwenda kutumia na familia zao hiyo pia haiko sawa.

Ili likome hili basi washushe bei ya gesi, utaona kama wanakata miti na kuchoma mkaa kinyemela.

In short, sisapoti pande zote....kwa police na raia
 
Back
Top Bottom