DOKEZO Baadhi ya Maafisa wa TMDA wanaofanya ukaguzi Maduka ya Dawa wachunguzwe, wanakiuka maadili

DOKEZO Baadhi ya Maafisa wa TMDA wanaofanya ukaguzi Maduka ya Dawa wachunguzwe, wanakiuka maadili

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Baadhi ya maafisa wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ambayo miezi kadhaa iliyopita ilikabidhiwa jukumu la kusimamia maduka ya dawa kutoka Baraza la Famasi ambao walikuwa na jukumu hilo awali, wamekuwa wakienda kwenye maduka ya dawa haswa yenye changamoto ya usajili wa baadhi ya dawa na kuzichukua dawa hizo kinyemera pia wakati mwingine kujenga mazingira ya kujipatia rushwa.

Katika maduka mengi ya dawa (Pharmacy) hasa yaliyopo jijini Dar es Salaam, mfano ni kuanzia Mbezi Beach kwenda hadi Tegeta na kwingineko, wengi wamekuwa wakinung'unika kwa kukumbana na changamoto hiyo, maafisa hao ambao ujitambulisha kuwa wapo kwenye oparesheni ya ukaguzi udai kuwa dawa hizo ambazo uzikamata kwa sababu mbalimbali kwamba wanaenda kuziteketeza endapo muhusika anashindwa kufuata taratibu kuzikomboa.

Lakini nimetonywa na vyanzo mbalimbali kuwa baadhi ya dawa maafisa hao uziuza kwenye maduka ya dawa mengine au wahusika kupeleka kwenye Pharmacy ambazo wanahusika uzimiliki au ambazo wana ushirika nazo.

Hata hivyo vyanzo mbalimbali vinadai kuna mazingira rushwa ambayo mara kadhaa yamekuwa yakijitokeza ambapo maafisa hao ili wawaachie wahusika waendelee kuuza dawa hizo ambazo udaiwa zipo nje ya usajili wao uomba au kujenga uwezekano wa kupokea rushwa ili kubariki uuzwaji wa dawa hizo kuendelea.

Mfano wanaweza kuchukua dawa hizo wanachukua namba za mmiliki baada ya muda wanampigia na kumwambia kwamba kama anataka kurejeshewa dawa hizo atupe pesa kadhaa azifuate au awaandalie wakija kuzirejesha waikute pesa hiyo, hali hiyo imekuwa kama utaratibu licha ya pesa hiyo kutolewa bila kuandikishana wala risiti.

Wamekuwa sana sana wakienda na fomu zao za kujaza aina ya dawa wanazochukua na gharama zake lakini jambo la kushangaza wamekuwa wakiandika bei za chini zisizo halisi na wakati mwingine baadhi ya dawa hawazijumuishi licha ya kuzichukua, na kibaya zaidi baadhi ya maafisa wamekuwa wakiwashinikiza wahusika wanaowakuta wakitoa huduma kusaini fomu hiyo huku wakiwapa hofu kuwa wakikataa watawafungia kwa kuwanyanganya vibali.

Pia maafisa vyanzo mbalimbali vinadai kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo rushwa pamoja na baadhi ya maduka ya dawa kumilikiwa na watu wenye ukwasi wa kifedha au watu maarufu wenye ushawishi wa mamlaka wamekuwa wamekuwa wakiwaacha bila oparesheni hiyo kuwagusa ingali nao wana changamoto za aina hiyo zinazofanana.

Kutokana na mazingira hayo hali hiyo inapunguza uwajibikaji badala ya kuchochea zoezi la usajili kufanyika kama inavyoelekezwa badala yake imekuwa sehemu ya watu kujinufaisha huku hao wakiendelea kuweka hatarini maisha ya Watu, kutokana na baadhi ya maduka ya dawa kutokidhi mashariti ya miongozo kuuza baadhi ya dawa, lakini mazingira hayo ya rushwa yanaweza kuwa nafasi kwa wengine kuingiza dawa feki zinazoweza kwenda kuleta matatizo zaidi.

Napendekeza au kuomba Serikali kufanya uchunguzi wa kina juu ya suala hili kisha kuchukua hatua, ikiwemo kuchunguza kama dawa hizo zimekuwa zikifika TMDA kama inavyoelezwa, sambamba na kubaini maafisa ambao watagundulika kujihusisha na mchezo huo ambao ni kinyume na maadili pamoja na sheria.

Sambamba na hilo TMDA itoke na kueleza wazi utaratibu wa oparesheni hizo, kwa kueleza zinafanyika kwa utaratibu upi na zinalenga nini ili kama kuna wanaokiuka taratibu wawajibike bila kuvunja Sheria au kuwanyima haki za msingi.

Ni muhimu sana kutambua kuwa suala lolote ambalo linagusa afya za raia linahitaji uadirifu zaidi ya tamaa kwa kuwa kutanguliza tamaa na kukosa uadirifu ni kuweka hatarini maisha afya za watu ambao ni mtaji wa kwanza katika nyenzo ya uchumi.


Majibu ya TMDA - TMDA yasema madai ya Watumishi wao kuhusishwa na Rushwa "Wanaolalamika, wajitokeze, walalamike rasmi na hatua zichukuliwe"
 
Acha janja janja binti sijui kijana... acha Maneno mengi fuata sheria
 
Acha upuuzi, sasa unasema yote hayo ya nini, hio biashara unaifanya au unaropoka tu,
 
hizo dawa zinapochukuliwa toka kwenye hayo maduka wamiliki huwa wanaaambiwa zina changamoto gani?
1. je huwa zimekwisha muda wa matumizi?

2. je hazina vibali vya kuuzwa na kisambazwa nchini tanzania?

3. ziko kwenye ngazi isiyo sahihi mfano duka la dawa baridi, duka la dawa muhimu au famasi?

4. je zinapochukuliwa zinaorodheshwa kwa majina na idadi yake?

5. je hao maafisa wanapokuja madukani wanakuwa na utambulisho wowote?
 
Back
Top Bottom