DOKEZO Baadhi ya mabasi kwenye njia ya Tabora-Mbeya yana hitilafu za kiufundi na barabara hiyo ina mashimo mengi

DOKEZO Baadhi ya mabasi kwenye njia ya Tabora-Mbeya yana hitilafu za kiufundi na barabara hiyo ina mashimo mengi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kuna wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa mabasi yanayofanya safari kati ya Tabora na Mbeya. Inadaiwa kuwa baadhi ya mabasi yanayotumika katika njia hiyo yana hitilafu za kiufundi, huku yakisafiri kwa mwendo kasi kwenye barabara yenye mashimo na makorongo mengi.

Kinachotia wasiwasi zaidi ni kwamba baadhi ya mabasi hayana hata mikanda ya usalama kwa abiria, hali inayoongeza hatari endapo ajali itatokea. Mara nyingi Watanzania huchukua tahadhari baada ya majanga kutokea badala ya kuyazuia mapema.

Pia kuna malalamiko kuwa askari wa usalama barabarani huwaona mabasi hayo katika vituo vya kuanzia safari lakini bado wanayaruhusu kuendelea na huduma, jambo linalozua maswali kuhusu utekelezaji wa sheria na wajibu wa kulinda usalama wa wananchi.

Aidha, baadhi ya abiria wamekuwa wakifurahia uendeshaji wa mwendo kasi bila kuzingatia hatari zinazoweza kujitokeza. Ni muhimu kutambua kwamba usalama barabarani ni jukumu la kila mmoja, na kulinda maisha ya wengine ni sehemu ya kulinda usalama wetu wenyewe.
 
Back
Top Bottom