Baadhi ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne ya Dkt. Jakaya Kikwete (Sehemu ya 1)

Baadhi ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne ya Dkt. Jakaya Kikwete (Sehemu ya 1)

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,536
Kumekuwepo na utaratibu au utamaduni wa kubeza mafanikio na kutokukubali kwa dhati kabisa na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Serikali rais Jakaya Kikwetena chama chake cha CCM. kuna wachache walisema hawauoni ubunifu wala utendaji kazi, uchapakazi wa Rais na uadilifu na uawaminifu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mimi ninaomba nitumie fursa hii kupingana nao hoja na kuwaomba waende wakafanye utafiti kwanza kabla ya kuongea, kubeza na kudharau mafanikio ya Serikali ya CCM ya awamu ya Nne. Lakini pia napenda kuwaasa tuondokane na utamaduni wa kubeza mafanikio na kudharau kila kitu ili mradi tu sisi ni Wapinzani, na kuwa mpinzani si kupinga kila kitu ikiwa pamoja na maendeleo.

Kumekuwepo na mafanikio mengine ya kujivunia tangu tupate uhuru ingawa kuna baadhi ya watu hawalidhishwi na kasi ya maendeleo iliyopo, ni ukweli usiopingika kuwa bado tunachangamoto za hapo na pale lakini yatupasa kuubali ukweli tumetoka mbali na mafanikio yamepatikana na yanaendelea kupatikana katika awamu zote tatu na ya a sasa anayomalizia rais Jakaya Kikwete.

Katika awamu hii ya nne kumekuwa na mafanikio ambayo hayakuwahi kutokea ktk nchi hii hata kama baadhi ya watu hawapendi kusikia hivyo, kwa uchache tumefanikiwa katika sekta mbalimbali kama elimu, afya, miundo mbinu na mambo chungu mzima ambayo tukisema tuyataje hapa hatutapa nafasi ya kutosha.

Tukianzia na elimu sote tunakumbuka kuwa serikali yake ilibua mpango wa ujenzi wa sekondari za kata kwa sababu nafasi za wanafunzi kuingia sekondari zilikuwa zimekuwa finyu kiasi cha kwamba ni asilimia kati ya 6 na 10 ya watoto wote waliokuwa wanamaliza shule za msingi mwaka 2005 walikuwa wanaingia sekondari wakati anaingia madarakani.

Pamoja kejeli nyingi zilizoelekezwa kwa shule za sekondari za kata kiasi cha kuitwa Yeboyebo katika miaka ya mwanzoni ya shule hizo, bado zimekuwa na mafanikio makubwa, ambayo ni sehemu ya mafanikio makubwa ya sekta ya elimu katika miaka tisa ya uongozi wa rais KIkwete.

Rais Kikwete alitangaza hivi karibuni kuwa Serikali yake imefuta katika shule za sekondari zilizo chini ya serikali, ili kuboresha sera ya elimu na kuhakikisha kila mwanafunzi anayeanza darasa kwanza anamaliza kidato cha nne. Hii ya kufuta ada itasaidia kila mtoto anayeanza darasa la kwanza anakuwa na nafasi ya kumaliza sekondari kwa maana ya kidato cha nne mpaka cha sita bila kulazimika kuacha shule kwa sababu ya ada.

Bajeti ya Elimu ndiyo iliyo kubwa kuliko zote kwa miaka mingi na imekuwa ikiongezeka. Kwa mfano, mwaka 2005/2006 zilitengwa shilingi bilioni 669.5 wakati mwaka 2014/2015 zimetengwa shilingi trilioni 3.1. Katika kipindi hicho, bajeti ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu imeongezeka kutoka shilingi bilioni 56.1 hadi shilingi bilioni 345. Kwa sababu hiyo idadi ya wanafunzi wanaofaidika imeongezeka kutoka 16,345 mwaka 2005 hadi 98,000 mwaka 2014.

Shule za msingi zimeongezeka kutoka 14,257 mwaka 2005 hadi 16,343 mwaka 2014 na hivyo kufanya idadi ya wanafunzi nayo kukua kutoka milioni 7.54 hadi milioni 8.23. Kwa upande wa sekondari shule zimeongezeka 531 mwaka 2005 hadi 4,576 mwaka 2014. Idadi ya wanafunzi nayo imeongezeka kutoka 524,325 mwaka 2005 hadi 1,804.056 mwaka 2014.

Upanuzi huu mkubwa na wa kihistoria umetokea pia kwenye vyuo vya elimu ya ufundi stadi ambapo vyuo vimeongezeka kutoka 184 hadi 744 kati ya mwaka 2005 na 2014. Kwa upande wa elimu ya juu, idadi ya vyuo imeongezeka kutoka 26 hadi 50 kati ya mwaka 2005 na 2014 na kufanya idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu iongezeke kutoka wanafunzi 40,719 mwaka 2005 hadi wanafunzi 200,986 mwaka 2014. Leo hii, hatuna tena tatizo na fursa ya kupata elimu kwa elimu ya msingi, sekondari, ufundi na elimu ya juu.

Mwaka 2005, urari wa wanafunzi kati yetu na wenzetu wa Afrika Mashariki ulikuwa wa chini mno kwa upande wetu. Kenya walikuwa na wanafunzi wa sekondari 925,341 na wa vyuo vikuu 108,407 ikilinganishwa na Tanzania iliyokuwa na wanafunzi 524,325 wa sekondari na 40,719 wa vyuo vikuu. Uganda ilikuwa na wanafunzi 728,393 wa sekondari na 124,313 wa vyuo vikuu.

Sasa hali ni tofauti. Kwa mwaka 2013, kwa mfano, Kenya ilikuwa na wanafunzi wa sekondari 2,104,300 na wanafunzi wa vyuo vikuu 324,600. Katika mwaka huohuo, Uganda walikuwa na wanafunzi wa sekondari 1,362,739 na wa vyuo vikuu 140,403. Ongezeko hili linatuweka katika hali nzuri ya ushindani tunapoelekea katika ushindani wa soko la pamoja ndani ya Afrika Mashariki ikilinganishwa na hali ilivyokuwa miaka 10 iliyopita.

Tumekuwa nchi ya kupigiwa mfano katika kutekeleza Malengo ya Milenia (MDGs) yanayohusu fursa ya watoto kupata elimu ya msingi, na usawa wa kijinsi baina ya watoto wa kiume na wa kike kupata elimu ya msingi na sekondari.

Sote tu mashahidi ya kuwa Rais Kikwete alivyoingia alikutana na changamoto mbalimbali ikiwamo ukame ambapo tathimini inaonyesha kuwa mwaka 2006 jumla ya ngombe 250,000, mbuzi 130,000 kondoo 122,000 pamoja na punda zaidi 700 walikufa kutokana na ukame wa ukosefu wa maji, jumla ya mifugo yote hiyo ilikuwa na thamani ya zaidi ya billion 45.3

Baada ya ukame kupungua serikali ya rais kikwete ikakutana na mtihani mwingine wa kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na kusababisha ongezeko la bei katika sekta ya usafiri. Mtihani mwingine kwa serikali ya rais Kikwete ilikuwa ilikuwa ni mtikisiko wa wa uchumi duniani ambayo uliathiri kwa kiasi kikubwa kwa mataifa yanayoendelea na yaliyokuwa yameandelea na kuathiri bajeti za chi kadhaa duniani, lakinin kwa uimara wa serikali yake hatukuyumbishwa na mtikisiko huu wa uchumi wa dunia mwaka 2009.

Rais kikwete pia amefanikiwa kuondoa uhasama wa visiwani unguja na pemba uliodumu kwa miaka 10 ambapo aliyemstaafu Benjamini Mkapa aliwahi kukiri baada ya kutoka madarakani kuwa mgogoro wa visiwa hivyo vya Karafuu ulikuwa unamnyima usingizi wakati wa utawala.

Mgogoro huo wa kisiasa ulifikia hatua mbaya kiasi ambacho hata ndugu wa baba mdogo na mkubwa walishindwa kuzikana pamoja na kuombana maji kutokana na misimamo na itikadi ya vyama vyao, lakini leo twaona wazanzibar wote wamekuwa wamoja na wakimbizi waliokwenda Mombasa walirejea nchini.
 
Ngoja wanywa viroba na wabwia ugolo watakavyokuja na mitusi, fact hawa kazi mitusi tu
 
SAFI SANA KWA KWELI! kwenye barabara wamejtahidi kwa kweli..mikoa yote inafikika kwa lami!
 
Ngoja wanywa viroba na wabwia ugolo watakavyokuja na mitusi, fact hawa kazi mitusi tu

Badala ya wewe kuja na lugha ya ukakasi ungesaidia kusema alikuta deni la taifa ni kiasi gani na analiacha taifa na deni kiasi gani tupime na maendeleo yaliyopatikana. Nadhani ungefanya jambo la maana kwa kumsupport huyo bwana aliyeleta facts sio kumchafulia uzi wake kwa kuleta mitazamo yako ya kiitakadi hapa.
 
Pesa kuongezeka hata kana ubora umeshuka ni mafanikio pia? Basi hata kuua elimu ni mafanikio
 
Hii ni hoja nzuri sana bali wanaoichallenge wanasema alivyoingia madarakani exchange rate ya dollar ilikuwa $1=sh.700/-, sasa ukifanya conversion usije kushanga ni kitu kile kile.
Bajeti ya Elimu ndiyo iliyo kubwa kuliko zote kwa miaka mingi na imekuwa ikiongezeka. Kwa mfano, mwaka 2005/2006 zilitengwa shilingi bilioni 669.5 wakati mwaka 2014/2015 zimetengwa shilingi trilioni 3.1. Katika kipindi hicho, bajeti ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu imeongezeka kutoka shilingi bilioni 56.1 hadi shilingi bilioni 345. Kwa sababu hiyo idadi ya wanafunzi wanaofaidika imeongezeka kutoka 16,345 mwaka 2005 hadi 98,000 mwaka 2014.
Hapa pia nami nakubali lakini wasiwasi ni huu hapa; haya manyunyu yanayoendelea kuna barabara moja leo nimekuta kipande kimezolewa hivyo nikawa najiuliza zitaweza kustahimili miaka mingapi japo tumeambiwa kuwa gharama zinazotumika ni (standard costs for standard road construction).
SAFI SANA KWA KWELI! kwenye barabara wamejtahidi kwa kweli..mikoa yote inafikika kwa lami!

Katika yote mtakayosifia tafadhali msisahau kulitaja deni la taifa lilivyopanda zaidi ya mara tatu huku maendeleo yakionekana kwa baadhi ya watu huku maendeleo ya kweli ya wananchi mfano huduma za afya, elimu, maji yakizidi kudidimia.

 
Napingana na wewe - Legacy ya Kikwete ni kama ifuatavyo!

Wakale walisema actions speaks louder than words. Kwa matendo yake, over the last 10 years, it is obvious to everyone kuwa kuwa Falsafa ya Uongozi wa Rais Jakaya Kikwete, na serikali yake ya awamu ya nne ni ile ya OMBAOMBA. Bwana Kikwete anaamini katika omba omba mpaka aliwahi kutetea falsafa hiyo kwa kusema kuwa yeye ni baba na huwa anaondoka nyumbani kila wakati kwenda nje kuhemea ili atuletee watoto (watanzania) fedha za matumizi. Sasa je wachambuzi wabobezi wanasema nini kuhusu falsafa ya Ombaomba?

Kila mtu anaelewa kuwa omba omba huwa haheshimiwi.

Hata wale waungwana ambao kwao ni kawaida kutoa sadaka kila mara, huwa hawawaheshimu ombaomba. Ombaomba hawaheshimiki kwa sababu moja tu, kwamba wanaishi kwa kutegemea fadhila za watu wengine.

Hali inakuwa mbaya zaidi inapokuwa ombaomba anaonekana ni mtu anayeweza kufanya kazi na kujipatia kipato, lakini hafanyi kazi kwa sababu anaona kazi ni ngumu zaidi kuliko kuzurura akikinga bakuli.

Wafadhili wanaotupa misaada wanatushangaa kama sisi wenyewe tunavyowashangaa ombaomba wanaoonekana kuwa na viungo na akili timamu. Rasilimali tulizojaliwa kuwa nazo zinatosha kabisa kutuwezesha kujitegemea iwapo tungezitumia vizuri.

Badala yake tunaona ni rahisi zaidi kuwaachia wageni wachukue rasilimali zetu waende kuzifanyia kazi za kuwanufaisha wao, halafu sisi tuletewe makombo kama misaada. Hapa kuna kitu kimetusibu katika uwezo wetu wa kufikiri, kama vile tumeingiliwa na ‘virus' katika bongo zetu, na ndiyo maana tunafanya mambo ambayo hayaingii akilini.

Nimewahi kutoa mfano wa tumbili tunaowaona kandokando ya njia katika mbuga ya Mikumi. Wanatoka msituni ambako kuna matunda mengi na yenye ubora wa upya (kwa maana ya ‘fresh') kuja kushinda barabarani wakisubiri watalii wawarushie maganda mabovu ya ndizi zilizonyauka.

Ndivyo tulivyo, na wahisani hawatuheshimu kwa sababu hatuheshimiki. Kila kitu tunataka tufanyiwe na wengine, hata pale ambapo ni dhahiri kwamba tunaweza kujifanyia sisi wenyewe.

Tuambizane ukweli. Ni kwamba wanatuona sisi ni sawa kabisa na nyani. Dharau waliyonayo kwetu inazidi pale tunapopewa ‘misaada' kwa masharti fulani, na hayo masharti tunayakubali haraka haraka, lakini tukiisha kukabidhiwa ‘misaada' hiyo tunayasahau yale masharti na kufanya tunavyotaka.

Suala la kuheshimu makubaliano tuliyoyatilia saini ni muhimu mno. Ndipo tunapata tofauti kati ya muungwana na mhuni. Mhuni atatia saini waraka wowote, (bila hata kuusoma) alimradi kuna kitu anakitaka sasa hivi, lakini katika dhamira yake hana nia ya kuheshimu chochote kilicho ndani ya waraka huo. Akiisha kupata anachohitaji, anaweza wala asiuangalie huo mkataba tena.

Muungwana huheshimu makubaliano aliyoingia na wenzake, na katika kila hatua za utekelezaji ataurejea mkataba huo mara kwa mara kuhakikisha haendi kinyume cha makubaliano. Huo ndio uungwana. Ukiisha kuvunja makubaliano yako na ‘mfadhili' kwa kulipeleka gari la ‘msaada' kule ulikokatazwa, unakuwa umejiweka mahali pa kukemewa na mama ambaye alikwisha kutuona kama watu wa hovyo.

Tulipopata uhuru tukaamua kujenga taifa moja kutokana na mipaka ya utumwa wetu, lakini tumefika katikati ya safari tumesahau tulikuwa tunakwenda wapi, na tunachofanya sasa ni kukimbia katika mduara tukifuata mikia yetu: Tulikotoka hatuko tena, na tulikokusudia kwenda hatukumbuki ni wapi. Sasa tunagawana mbao za mashua yetu.

Sasa tumekuwa kama watu waliotekwa kiakili ambao hawawezi kufurukuta katika jambo lolote. Kama hatuna hata lugha tunayoweza kuiita na kuifanya kuwa lugha ya taifa, hatuwezi kujiita taifa. Kuiita lugha ya taifa ni jambo rahisi; tulikwisha kufanya hivyo, na tumefanya hivyo kwa muda wa miongo mitano. Lakini si kweli kwamba Kiswahili ni lugha ya taifa. Ni kama vile ambavyo tumekuwa tukisema kwa miongo minne kwamba Dodoma ndio mji mkuu wa Tanzania wakati tukijua kwamba hilo nalo si kweli. Kila mtu anajua kwamba akitaka makao makuu ya serikali yafanye jambo fulani inabidi aende Dar es Salaam, na kama wahusika wako Dodoma kwa sababu ya kikao cha Bunge, atawasubiri warudi.

Ugumu wa kukubali ukweli katika hili, na hususan kwa watu wanaoiona lugha ya kigeni kama yenye hadhi ya utukufu kuliko lugha yao wenyewe umekuwapo kila mahali duniani. Lakini vile vile, inapotokea kwamba jamii inayojitambua kama taifa, hata kama ni taifa dogo, ikajihisi kwamba lugha yao inahujumiwa, jamii hiyo itachukua hatua za kupambana dhidi ya hujuma hizo, wakati mwingine kwa kumwaga damu.

Ikifikia hatua hiyo, jamii hiyo inakuwa na haki ya kujitambulisha kama taifa, na wakati mwingine utaifa huo unaweza ukawa hauna nchi, hauna ardhi ulipojisimika, lakini utaifa unadumu ndani ya nyoyo za watu wake, kokote kule waliko, hata kama wamesambaa na kutapakaa duniani kote.

Sisi hatuko hivyo.

By Jenerali Ulimwengu
Raiamwema Toleo 396
March 11, 2015
 
shule zimeongezwa kwa sababu idad ya watu imeongeza.mikopo ya elimu ya juu imeongezeka kwa sababu wanafunz wanaomaliza form 6 wameongezeka.huwez ukawa na watu mil40 halafu ukawa na shule chache na huduma nyingne chache.labda tu kafuata muendelezo wa MMES kutoka MMEM.hakuna alichofanya
 
Haya mambo yakutulazimisha kukubali kile munachotaka Huwa munanikera sana,Kwanini munalazimisha kuwa JK kafanya mambo makubwa na musiache wananchi wenyewe waseme, Mbona mtu ukifanya jambo jema wala huhitaji kupiga mbiu, wananchi wanaona. Juzi tu nilikuwa uswahilini kwangu nanunua chips nikakuta mjadala sijui ulianzia Wapi Ila nilisikia wakimsifia Ben kuwa katika utawala wake walikuwa chips mayai kwa shilingi 500 mpk Jamaa anaondoka madarakani,Ila tangu aingie muheshimiwa sana......hah!
 
Penye mazuri mengi mabaya machache hayatakosekana.Mh.Rais ni bina adamu na hakuna binadamu akiyekamilika.Muhimu tuyachukuwe mazuri na yale mabaya tuyarekebishe kwa ujumla wetu.
 
Napingana na wewe - Legacy ya Kikwete ni kama ifuatavyo!


Wakale walisema actions speaks louder than words. Kwa matendo yake, over the last 10 years, it is obvious to everyone kuwa kuwa Falsafa ya Uongozi wa Rais Jakaya Kikwete, na serikali yake ya awamu ya nne ni ile ya OMBAOMBA. Bwana Kikwete anaamini katika omba omba mpaka aliwahi kutetea falsafa hiyo kwa kusema kuwa yeye ni baba na huwa anaondoka nyumbani kila wakati kwenda nje kuhemea ili atuletee watoto (watanzania) fedha za matumizi. Sasa je wachambuzi wabobezi wanasema nini kuhusu falsafa ya Ombaomba?



Kila mtu anaelewa kuwa omba omba huwa haheshimiwi.

Hata wale waungwana ambao kwao ni kawaida kutoa sadaka kila mara, huwa hawawaheshimu ombaomba. Ombaomba hawaheshimiki kwa sababu moja tu, kwamba wanaishi kwa kutegemea fadhila za watu wengine.
HEBU FIKIRIA KAMA WW NDO UWE RAIS,UNAWEZA KUDHUBUTU CHOCHOTE PASIPO KULAUMIWA??? WATU WANASHINDWA HATA KUONGOZA FAMILIA ZAO SEMBUSE KUWA RAISI!! THINK TWICE
 
shule zimeongezwa kwa sababu idad ya watu imeongeza.mikopo ya elimu ya juu imeongezeka kwa sababu wanafunz wanaomaliza form 6 wameongezeka.huwez ukawa na watu mil40 halafu ukawa na shule chache na huduma nyingne chache.labda tu kafuata muendelezo wa MMES kutoka MMEM.hakuna alichofanya
Wewe umefanya nini? umemudu hata kuingoza familia yako? kusaidia maskini? jitathmini kabla hujaropoka
 
shule zimeongezwa kwa sababu idad ya watu imeongeza.mikopo ya elimu ya juu imeongezeka kwa sababu wanafunz wanaomaliza form 6 wameongezeka.huwez ukawa na watu mil40 halafu ukawa na shule chache na huduma nyingne chache.labda tu kafuata muendelezo wa MMES kutoka MMEM.hakuna alichofanya

Macho unayo lakini hayaoni, masikio unayo lakini hayasikii, moyo wako una maradhi.
 
Kweli itatuweka huru, upande wa kujenga miundo mbinu anastahili pongezi sana tu.

Mahuaiano ya kidiplomasia ya meongezeka sana. Tanzania inasomeka kimataifa.

Hisia za udini kati ya ukristo na uislamu zimekua sana kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya nchi hii. Kwa hili kafanikiwa sana tu na muda si mrefu tutanza kuvuna kilicho pandwa.
 
Mara nyingi najiuliza na kusikitika, kwa nini Tanzania yenye watu wenye vipaji, mantiki kunjufu, fikra pevu kama mwandishi, hawapewi nafasi? Au kuna 'conspiracy'? Ni dhahiri kwamba hatutaweza kuendelea kama hatuna dira na kuifuata. Kilichopo sasa ni vuruga mechi. Huyu ombaomba, yule mtaifishaji na mwengine rukhsa. Sijui ajaye atakuwa nini- bomoa?
 
Penye mazuri mengi mabaya machache hayatakosekana.Mh.Rais ni bina adamu na hakuna binadamu akiyekamilika.Muhimu tuyachukuwe mazuri na yale mabaya tuyarekebishe kwa ujumla wetu.

Watu wote hufanya makosa, hata viongozi. Lakini inapokuja kwa kiongozi kufanya makosa ambayo kwa kweli si ya lazima, kwani anaweza kuyatibu (see, ufisadi), hakuna namna ya kumtetea. Hebu jiulize, kama bila ya ufisadi aliokuwa na uwezo wa kuuzuia, Tanzania ingekuwa wapi katika miaka 10? Ufisadi wa ESCROW pekee ungeweza kumaliza matatizo yote ya maji Dodoma kwa miaka 30 ijayo.
 
Nakumbuka wakati fulani kutoka bahi kupitia manyoni mpaka ikungi ktk jimbo la tundu lissu tulikuwa tunalala njiani siku 2 wakati eneo lenyewe halifiki hata kilometer 130! Heko Dr. Jk
 
Back
Top Bottom