Wakati rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribia kustaafu kwa kuwatumikia Watanzania kutoka pale ikulu ya magogoni, atakumbukwa kwa mambo mengi mazuri hususani kwa watu kutoka mikoani kuanzaia tarafani mpaka wilayani kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi chake chote cha miaka kumi tangu mwaka 2005 alipoingia madarakani mpaka sasa mwaka huu 2015 anapoondoka madarakani.
Miongoni mwa Sekta amabazo zimfanya rais Kikwete kukumbuka ni sekta ya miundo mbinu ambapo katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne, Serikaliimepata mafanikio makubwa katika kuboresha miundombinu ya barabara namadaraja nchini. Katika kipindi hicho, barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa17,762 zimekuwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji ambapo barabara zenyeurefu wa jumla ya kilometa 5,568 zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Aidha, barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 3,873 zinaendelea kujengwakwa kiwango cha lami, barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 4,965 zimefanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na Serikali inatafuta fedha za kuzijenga kwa kiwango cha lami. Vilevile, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara zenye jumla ya kilometa 3,356 unaendelea.
Pia serikali ya rais Jakaya Kikwete itkumbukwa kwa ujenzi ujenzi na ukarabati wa madaraja, hakuna asiyejua kuwa miaka ya nyuma ilikuwa ikifika wakati wa masika kuna wilaya mbali mbali zilikuwa zinakosa mawasiliano na mikoa pmoja na miji mikubwa mpaka hali ya mvua zinapopungu hali hii ilikuwa inawakera sana wananchi kwa kuwa shughuli nyingi za maendelo zilikuwa zinasimama.
Serikali ya awamu ya nne ililiona hilo na ikadiliki kulivali njuga kwa fedha zetu za ndani bila kusubiri wafadhili, katika hili hta kama wapinzani watapinga lakini wanancjhi wanajua ukweli wa hili n hata kama utafunga safari uende katika maeneo ambayo yalikuwa na tata katika madaraja utapa majibu yake. Tumeshudia jumla ya madaraja makubwa 30 yapo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Kati ya hayo, madaraja makubwa 12 yamekamilika kujengwa, ambayo ni Rusumo (Kagera), Umoja (Mtwara), Mwanhuzi (Simiyu), Kikwete (Kigoma), Nangoo (Mtwara), Ruhekei (Ruvuma), Mbutu (Tabora), Mwatisi (Morogoro), Ruvu (Pwani), Nanganga (Mtwara), Maligisu (Mwanza) na daraja la waenda kwa miguula Mabatini (Mwanza).
Aidha, madaraja makubwa 6 yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi, ambayo ni Kigamboni (Dsm), Kilombero (Morogoro), Kavuu (Katavi), Sibiti (Singida), Ruvu Chini (Pwani) na Lukuledi II (Mtwara). Madaraja makubwa 12 yako kwenye maandalizi ya kujengwa ambayo ni Momba (mpakani mwa Rukwa na Mbeya), Mwiti (Mtwara), Simiyu (Mwanza), Wami (Pwani), Ruhuhu (Ruvuma), Ubungo Interchange (Dar es Salaam), TAZARA Flover (Dar es Salaam), Selander (Dar es Salaam), Daraja jipya la Wami Chini (Pwani), Pangani (Tanga), Kirumi (Mara) na daraja la waenda kwa miguu la Furahisha (Mwanza).
Sambamba na ujenzi wa madaraja makubwa, madaraja madogo madogo zaidi ya 7,200 yamejengwa na kukamilika. katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2015 Serikali pia imeimarisha Mfuko wa Barabara ambapo mapato ya Mfuko yameongezeka kutoka Shilingi bilioni 73.08 katika mwaka wa fedha 2005/06 hadi Shilingi bilioni 751.7 katika mwaka wa fedha 2014/15 ikiwa ni ongezeko la asilimia 928.6. ni ajabu sana pale kina Mbowe, Lipumba pamoja na Mbatia wanavyojifanya vipofu katika mafaniko haya ya awamu ya nne ambayo tangu uhuru yalikuwa kero kubwa kwa wananchi.
wakati Serikali ya Awamu ya Nne inaingia madarakani mwaka 2005, vivuko vya Serikali vilivyokuwa vinatoa huduma vilikuwa kumi na tano (15) tu. Hadi kufikia Aprili, 2015, idadi ya vivuko vya Serikali vinavyotoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini imeongezeka na kufikia ishirini na nane (28).
kwa upande wa nyumba na majengo ya Serikali, Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ilijenga nyumba 173 za makazi ya Viongozi wa Umma na kuanza mradi wa ujenzi wa nyumba 10,000 za Watumishi wa Umma ambapo nyumba 643 zilikamilika katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2015 na nyumba 270 zinaendelea kujengwa.
Aidha,Serikali kupitia TBA imeendelea kuhakikisha kwamba ujenzi wa nyumba na majengo yanayotumiwa na umma unazingatia mahitaji maalum hususan kwa watu wenye ulemavu. Suala hili limeendelea kutekelezwa kupitia miradi ya ujenzi wa majengo yote ya Serikali ambayo Wakala wa Majengo umesanifu na kusimamia kama ifuatavyo: Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara, Majengo ya Ofisi za Wakuu wa Wilaya za Bariadi, Rorya, Kilolo, Nyamagana na Mvomero. Mengine ni jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi – Kitengo cha Wakimbizi,
Jengo la hospitali ya Manyara na ukumbi wa mikutano na Vituo vya Afya ya Msingi (Primary Health Centre Institutions – PHCI) – Iringa, majengo ya Ofisi za Wakuu 6 wa Mikoa ya Katavi, Njombe, Geita na Simiyu pamoja na majengo ya Ofisi za Wakuu wa Wilaya 19 za Buhigwe, Busega, Butiama, Chemba, Gairo, Ikungi, Itilima, Kalambo, Kaliua, Kakonko, Kyerwa, Mbogwe, Mkalama, Mlele, Momba Nyang`hwale, Nyasa, Uvinza na Wanging'ombe.
Katika mwaka wa fedha 2014/15, wakati ambao serikali ya awamu ya imeendelea na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayosimamiwa na Wizara ya ujenzi inaendelea vizuri. Kwa upande wa barabara kuu, jumla ya kilometa 504.4 kati ya kilometa 539zilizopangwa kujengwa kwa kiwango cha lami zilikuwa zimekamilika hadi kufikia Aprili, 2015. Na kilometa 87.75 zilikua zimekarabatiwa kwa kiwango cha lami. Kwa upande wa barabara za mikoa, kilometa 40.5 zilijengwa kwa kiwango cha lami. Vile vile, kilometa 450 zilifanyiwa ukarabati kwa kiwango cha changarawe katika kipindi hicho.
Wakati ris Jakaya akiwa anasubiri muda wake ufike akapumzike hataliacha hivi suala la msongamano mkubwa wa magari katika Jiji la Dar es salaam, serikali yake kupitia Wizara ya ujenzi na Mamlaka mbalimbali zikiwemo Halmashauri za Jiji zimechukuliwa hatua mbalimbli za kukabiliana na tatizo hilo la msongamano wa magari. Tayari maandalizi ya ujenzi barabara ya njia sita ya Dar es Salaam – Chalinze – Morogoro (km 200) sehemu ya Dar es Salaam –Chalinze (km 100) imepangwa kujengwa kwa kiwango cha "Expressway".
Maandalizi ya mradi huu utakaotekelezwa kwa utaratibu wa ubia baina ya Serikali na Sekta Binafsi (Public Private Partnership - PPP) yamekamilika na yameanza kufanyiwaAprili, 2015, Mshauri Mwelekezi (Transaction Advisor) ambaye ni Kampuni ya Cheil Engineering Company Limited kutoka Korea ya Kusini alikwishateuliwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 7.72 na amekamilisha utafiti wa mwelekeo wabarabara (route survey).
Mwelekeo wa barabara uliochaguliwa unaanzia Charambe katika barabara ya Kilwa kupitia Kisarawe, Kibamba, Kibaha, Mlandizi hadi Chalinze.
Barabara itakuwa na urefu wa kilometa 128 itakuwa ya njia sita (6) na barabara za juu (interchanges) tano (5) katika maeneo ya Charambe, Kisarawe, Kibamba, Mlandizi na Chalinze. Pia itakuwa na vituo vikuu viwili (2) vya kulipia tozo ya barabara (Toll Plaza) maeneo ya Charambe na Chalinze.
Pia barabara hii itakuwa na eneo la kupumzika (rest station) pale Visiga na maeneo mawili (2) ya kuegesha malori ambayo yatakuwa Mbezi na Mbala.
Vilevile Mshauri Mwelekezi atafanya utafiti wa jinsi ya kuunganisha barabara hii kutoka Charambe hadi bandari ya Dar es Salaam. Kwa sasa Mshauri Mwelekezia naendelea na kazi ya kuandaa nyaraka za zabuni na baadaye atasimamia taratibu za kumpata Mbia/Mwekezaji (Concessionaire) wa mradi huu. Gharama za mradi huu wa ujenzi zinakadiriwa kufikia Shilingi Trilioni 2.397 na utatekelezwa kwa njia ya Ubia na Sekta Binafsi (PPP).
Tunajua pia kuwa huwezi kuondoa Msongamano wa magari ya jiji Dar ers Salaam bila kulitaka Daraja la Selander, Rais Jakaya Kikwete anaondoka magogoni akiwa keshalipati ufumbuzi wa kudumu eneo hilo la selander, Serikali ya Korea Kusini imekubali kuipatia Serikali ya Tanzania mkopo wamasharti nafuu kwa ajili ya ujenzi wa Daraja jipya la Selander. Upembuzi yakinifu wa mradi huu umekamilika na maandalizi ya kutiliana saini makubaliano ya mkopo wa kugharamia ujenzi wa daraja kati ya Korea Exim Bank (kwa niaba yaSerikali ya Korea Kusini) na Serikali ya Tanzania yanaendelea.
Daraja hili pamoja na barabara zake za maingilio litakuwa na urefu wa jumla ya kilometa 7.2 na litaanzia eneo la Koko Beach kupitia Kenyatta Drive na kuingia baharini na kisha kuungana na barabara ya Barack Obama eneo la Hospitali ya Aghakan. Mradi huu tagharimu Shilingi Bilioni 197.5. Aidha, Daraja la Kigamboni linaendelea kujengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 236.524.
Ujenzi wa barabara za juu (flyovers na interchanges) na maboresho ya makutano ya barabara katika jiji la Dares Salaam,mpkaAprili, 2015 hali utekelezaji upo kama ifuatavyo kama ifuatavyo: Barabara ya Juu (Flyover) ya TAZARA: Usanifu wa kina umekamilika chini ya ufadhili wa Serikali ya Japan. Taratibu za kumpata Mkandarasi wa ujenzi atakayekidhi vigezo zinaendelea huko Japan.
Kazi ya ujenzi wa Flyover ya TAZARA ambayo itagharamiwa na Serikali ya Japan ikishirikiana na Serikali ya Tanzania inatarajiwa kuanza katika ya mwaka, 2015. Gharama za mradi huu ni Shilingi Bilioni 93.622. Interchange ya Ubungo Benki ya Dunia imekubali kugharamia utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara za juu (Interchange) katika makutano ya Ubungo. Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Interchange ya Ubungo umekamilika. Zabuni ya kumpata Mhandisi Mshauri kwa ajili ya usimamizi wa ujenzi zimetangazwa. Serikali inakamilisha taratibu kwa ajili ya kutangaza zabuni za kumtafuta Mkandarasi wa ujenzi.
Vile vile Interchange ya Ubungo itakuwa na levels tatu ambapo magari yanayotoka katikati ya jiji la Dar es Salaam kuelekea Morogoro yatapita chini, magari yanayotoka TAZARA kuelekea Mwenge yatapita juu na magari yanayokata kulia yatapita katikati. Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa Shilingi Bilioni 126.661. Upanuzi wa barabara ya Gerezani (Bendera Tatu – KAMATA) unakadiriwa kugharimu Shilingi Bilioni 29.135. serikali inaendelea na maandalizi ya Maboresho ya Makutano ya Chang'ombe, Magomeni, Mwenge, Tabata, KAMATA, Uhasibu na Morocco yanaendelea.
Serikali ya Kikwete imeendelea kutekeleza miradi ya barabara za kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam zenye urefu wa kilometa 109.35. Barabara hizo ni pamoja na Ubungo Bus Terminal – Mabibo – Kigogo Roundabout (km 6.4); Kigogo Roundabout – Bonde la Msimbazi – Twiga/Msimbazi Jct (km 2.7); Jet Corner – Vituka – Devis Corner (km 10.30); Tabata Dampo – Kigogo (km 1.60); Ubungo Maziwa – External (km 0.65); Mbezi (Morogoro Road) – Malambamawili – Kinyerezi –Banana (km 14); Tegeta Kibaoni – Wazo Hill – Goba – Mbezi Mwisho (km 20); Tangi Bovu – Goba (km 9); Kimara Baruti–Msewe (km 2.6); Kimara –Kilungule – External Mandela Road (km 9); na Kibamba – Kisopwa (km 12.0). Pia ukarabati unaoendelea katika barabara za Ukonga – Mombasa –Msongola , Kimbiji – Tundwisongani, Misheni – Kijichi – Zakhem, barabara ya Uhuru, Kutengeneza Mifereji ya Maji, uhamishaji miundombinu maeneo ya miradi, malipo ya fidia, n.k. vyote vinakadiriwa kugharimu Shilingi Bilioni 181.795.
Pia Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (Bus Rapid Transit Infrastructure – BRT) ambao unajumuisha Ujenzi wa Barabara ya Morogoro kutoka Kimara hadi Kivukoni, barabara ya Kawawa kutoka Magomeni hadi Morocco na barabara ya Msimbazi kutoka Fire hadi Kariakoo zenye jumla ya urefu wa kilometa 20.9. Pia kuna vituo vya mabasi 29, vituo vikubwa vitatu namadaraja ya waenda kwa miguu matatu. Pia Ujenzi wa Karakana (Depot) na Kituo cha Mabasi cha Ubungo; Ujenzi wa Karakana (Depot) ya Jangwani; Ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi (Terminal) cha Kivukoni; vyote hivyo mchakato wake unaendelea kwa hatua mbali mbali, kwa m,tu ambaye anayeishi mikoani akija nleo Dar es Salaam maeneo ya katikati ya mji atashangaa kasi ya ejenzi inavyoendelea leo.
Pamoja na juhudi kubwa hizo za serikali ya awamu ya nne lakini bado wapinzani wamekuwa wakibeza kuwa miradi mingi haitekwelezi napenda kuwapa changamoto moja wawe wakweli kutoka mioyoni mwao waangali hali ya barabara zetu leo ni sawa na miaka kumi iliyopita
Bado hatujasahu ndugu zetu walivyokuwa wakiliwa na simba njia ya kusini ambapo leo unapamba basi kwenda mtwara kutoka dar es Salaam kwenda mtwara unafika safari yako ndani ya masaa tisa, pia tunakumbuka wakazi wa kanda ya ziwa walivyokuwa wakiteseka kulala njiani mpaka kwa siku tatu wakati leo wanafika ndani ya siku moja.
Hatujasahau ndugu zetu wa Kagera walikuwa wanalazimika kutumia mpaka siku tano kupitia Kenya na Uganda kufika mkoani, kwao hali ni tofauti na sasa ile hali ya kushuka mipakani na kugonga visa hakuna tena na gharama za usafiri na matumizi za kupitia Kenya na Uganda hazipo tena. Haya yaliwezekanaje ndani miaka 10 ya jakaya kikwete na yashindikane hayo mengine, rais Jakaya anamuachia vema rais ajaye kwenye sekta ya miundo mbinu, ambayo ni miongoni mwa kero kubwa tangu uhuru kwa watanzania.
Kwa wale wanaosema rais Jakaya Kikwete hana lolote alilowafanyia watanzania ningependa kuwaasa jambo moja kuwa wanachofanya ni kujidanganya kwani watanzania wanajua mengi na yanaonekana kwa macho.
Vile vile niwaambie wabunge wa upinzani walikuwa wakibeza miradi ya wizara ya ujenzi ya miundo mbinu kuwa miradi hiyo niliyoitaja hapo juu kuwa haitekelezeki napenda kuwaambia hata huu mtandao wa barabara nchini walikuwa wakiubeza lakini leo wapo kimya hawana la kusema. Kwa wale wanaopinga ningewashauri wafunge safari siku moja ya kuzunguuka nchi yetu kwa njia ya barabara watajionea wenyewe, kwanza wangeanza safari Arusha kwenda Singida kupitia Manyara.
Halafu angewauliza wanaotoka Dodoma kwenda Iringa kupitia mtera, halafu nenda njia ya Manyoni hadi kigoma kupitia Tabora, na kwa wakazi wa kusini akawaulize wanaotoka Masasi kwenda Songea kupitia Tunduru. Pia aangalie safari ya kutoka Songea kwenda mpaka Sumbawaga.
Kwa wakazi wa kanda ya ziwa angalie Safari ya kutoka Manyoni kwenda Mwanza kupitia Singida mjini, Nzega, Shinyanga mpaka Mwanza yenyewe. Halafua anzia Shinyanga kwenda Bukoba. Rudi tena anzia Dar es Salaam kwenda Lindi na Mtwara.
Nani asiyejua kuwa miaka kumi iliyopita kwa makazi wa Dar es Salam mwenye asili ya ya mikoa ya Lindi, Mtwara, Kigoma,Rukwa, Simiyu, Geita, Ruvuma na Katazi wakipata misiba kufika kwao ilikuwa shughuli pevu kufika makwao.
Mwisho napenda kumpongeza mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe wakati akichangia hotuba ya wizara ya fedha 2014/2015 kwa mara ya kwanza nimemshuhudia akiuunga mkono bajeti kwa kusema wakati anaingia madarakani miaka 4, iliyopita katika jimbo lake kulikuwa na vijiji vitatu tu vyenye umeme katika vijiji 60 kwa sasa jimbo Ludewa ina vijiji 50 vyenye umeme na vingine vitapata umeme kabla ya rais Kikwete kuondoka madarakani, filikunjombe anasema wakati anaingia madarakani kulikuwa hakuna lami lakini kwa sasa kuna kilometer 50 za lami kati ya kilometer `200 za barabara katika jimbo lote la Ludewa na zinaendea kujengwa.
Filikunjombe amesema kuwa kama atapinga mfanikio ya awamu ya nne basi hata wananchi wake watamkataa, alifika mbali zaidi mpaka kutaja idadi ya madaraja tata ambayo yalikuwa yanawasumbua kipindi cha masika lakini kwa sasa yanapitika msimu wote. Napenda kumalizia kwa kumtakia mapumziko mema na afya tele kwa rais waetu Jakaya pale muda wake wa kustaafu utakapofika.