Baadhi ya mambo yaliyofanywa kwa upendo na Rais Samia mkoani Lindi

Baadhi ya mambo yaliyofanywa kwa upendo na Rais Samia mkoani Lindi

msuyaeric

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2014
Posts
862
Reaction score
1,264
Na Mwl Udadis,

KATIKA ELIMU: Mkoa wa Lindi umewezeshwa fedha za kujenga shule mpya za sekondari 11 ikiwepo shule ya Sekondari Maalum ya Wasichana katika eneo la Kilangala ndani ya Manispaa ya Lindi. Pia serikali imetoa fedha kwaajili ya kutumika kugharamia huduma mbalimbali za mpango wa elimu bila malipo.

Vile vile katika kupunguza msongamano wa wanafunzi, Serikali imewezesha fedha za ujenzi vyumba vya madarasa katika shule za sekondari ,msingi na katika vituo shikizi vyenye uhitaji wa madarasa ikiwa ni sehemu ya mpango uliotekelezwa nchi nzima.

KATIKA AFYA: Hadi kufikia Mwezi Juni, Mkoa wa Lindi ulipokea jumla ya Bilioni 23.8 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ikiwepo ujenzi wa Hospitali mpya ya Rufaa yenye thamani ya shilingi bilioni 7.6 eneo la Mitwero Manispaa ya Lindi.

Pia ujenzi wa Hospitali muhimu ya Manispaa ya Lindi ambapo serikali ilitoa shilingi milioni 500, ukamilishaji wa Hospitali tatu za Wilaya za Liwale, Kiwalala na Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa kwaajili ya kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora na kwa ukaribu.

Vile vile Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia imewezesha ujenzi wa vituo: vipya vya Afya 11 vyenye thamani ya shilini bilioni 5.2, ujenzi wa nyumba za watumishi wa Afya 5 ambapo fedha kiasi cha shilingi milioni 450 zilitolewa. Hii ni ishara ya uongozi unaojali ustawi wa wananchi.

Pia, ujenzi wa ICU kwa Halmashauri ya Nachingwea, wodi za huduma za dharura(EMD), Ukamilishaji wa zahanati 26. Aidha Serikali imetoa shilingi bilioni 4.1 kwa kipindi cha kuanzia mwezi Machi 2021 kupitia MSD kwa ajili ya kununua dawa, vifaa tiba, vitendanishi na vifaa vya kutolea afya ya kinywa na meno.
IMG-20221201-WA0035.jpg


Sent from my SM-A325F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu huko lindi mbolea vp? Umeme je? Mfumuko wa bei ukoje?

Migogoro ya ardhi niaje?

Au nyie wenzetu mnakula shule na sindano za hospital?
 
Mkuu huko lindi mbolea vp? Umeme je? Mfumuko wa bei ukoje?

Migogoro ya ardhi niaje?

Au nyie wenzetu mnakula shule na sindano za hospital?
hayo matatizo ndo ya nchi zote za thirdworld.kwa mfano suala la upungufu wa nishati ya umeme ni kwasababu tunategemea saana hydro electrick power.nchi nyingine wana option ya nuclear plants
 
Back
Top Bottom