Baadhi ya marekebisho ya kodi, Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/2021

Baadhi ya marekebisho ya kodi, Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/2021

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Baadhi ya marekebisho ya kodi

KODI YA KIPATO (PAYE)

Wanaopata chini ya tsh 270,000 kwa mwezi kutokakatwa kodi ya mapato.

Watu wa kipato cha Zaidi ya 270,000 kwa mwezi lakini ni chini ya 520,000 watalipa kodi 9%

KODI YA ZUIO KWA HUDUMA ZA MTANDAO
Bajeti imeweka kodi ya zuio ya 10% kwa mawakala wa huduma za kifedha za mtandao (m-pesa, tigo pesa nk)

Pia kuongeza kiwango cha kutuma kwa simu hadi Tsh Millioni 5

TAX ADMINISTRATION

PTRA watakusanya mapato yasiyo ya kodi, mapato hayo ni yanayokusanya na mamlaka za hifadhi, TANAPA, NCAA na TAWA

NAMBA SPECIAL ZA MAGARI
Namba special za magari kuanza kutolewa kwa Tsh 500,000

MAMLAKA YA WAZIRI

Waziri wa Fedha amepewa mamlaka ya kusamehe kodi isiyozidi Tsh bilioni moja


Ushuru wa Forodha
Kutotoza ushuru wa forodha kwenye malighafi zinazotumika katika uzalishaji wa vifaa maalum vinavyotumika katika kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19) vikiwemo Barakoa (Masks), kipukusi (sanitizer), mashine za kusaidia kupumua (ventilators), na mavazi maalum ya kujikinga yanayotumiwa na madaktari na wahudumu wa afya (PPE). Msamaha huu utatolewa kwa utaratibu wa “duty remission”. Hatua hii inalenga kutoa unafuu wa uzalishaji wa vifaa hivyo hapa nchini ili kuongeza kasi katika kupambana na ugonjwa huo;


Kutotoza ushuru wa forodha kwenye madawa na vifaa muhimu vinavyotumika kupima, kukinga, kutibu na kupambana na mlipuko wa magonjwa kama vile ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID- 19).

Hatua hii inalenga kutoa unafuu wa bidhaa hizo ili kurahisisha mapambano na udhibiti wa magonjwa hayo pindi yanapojitokeza;

OSHA
Napendekeza kufuta tozo ya mafunzo ya elimu kwa umma iliyokuwa inatozwa kiasi cha shilingi laki mbili na nusu (250,000/=) kwa kila mshiriki kwa kuwa hili ni jukumu la msingi la OSHA kuelimisha umma;
 

Attachments

Rais kajionea hana uwezo wa kuongeza mishahara imebidi apunguze tu Kodi,
 
Ila wametumia akili kubwa msamaha wa Kodi ndio ongezeko la salary
 
Hii sijaielewa tafsiri yake kwnye huo mchanganuo
Screenshot_20200611-192048.jpg
 
Hii sijaielewa tafsiri yake kwnye huo mchanganuoView attachment 1476540
Shortly kutakuwa na nafuu ya kodi ya PAYE kati ya approx 46,000 hadi 51,000. Tegemea ka fifty flani hivi amazing kama salary yako ni from 1,100,000 taxable income.

Ila zamani mshahara chini ya 170,000 walikuwa hawalipi kodi ila sasa chini ya 270,000 watakuwa hawalipi kodi.
 
Kwa vyovyote vile ila watu washapigika Sana na ukata for four yrs, yaani haina mvuto!
 
Jamani wafute kodi za vifaa ya kilimo kama tractor combiner harvester etc,,kilimo ni uti wa mgongo,,hii kuvuna kwa mkono inapoteza mda na rasilimali watu.
 
Akikuongezea halafu akaikata kama kodi si ni vilevile tu!

Drone Camera

Hapana, kuna tofauti kubwa baada ya muda.

Kumbuka, ongezeko la mshahara litaakisiwa kwenye makato na michango ya kisheria ya mfanyakazi na mwajiri. Punguzo la kodi litaongeza kipato Halisi (net income) cha mfanyakazi lakini hakitabadili kiwango cha makato mengine.

Hivyo, kuongeza mshahara kutaongeza makato na mfanyakazi na mwajiri ( Makato ya lazima yanapigiwa hesabu kwa aslilmia ya kipato ghafi) ambayo itapelekea kuongezeka kwa mafao pindi mfanyakazi anapoaachana na ajira kwa sababu zozote zile.
 
Jamani wafute kodi za vifaa ya kilimo kama tractor combiner harvester etc,,kilimo ni uti wa mgongo,,hii kuvuna kwa mkono inapoteza mda na rasilimali watu.

Hata kuwapa incentives wataalamu wetu wa kilimo wanaofanya kazi moja kwa moja na wakulima wadogo ili kuinua uwezo wao kwa uzalishaji.
 
Wapunguze kodi kwenye vifaa vya ujenzi pia.
 
Nchi ya kilimo hii wangetoa Kodi zote kwa bidhaa Kama matrekta na vifaa vyake wapate mapato mengi kwa wakulima wanapouza mazao nje kuliko kukabana kuanzia mwanzo watu wanaendelea kulima kienyeji wakati ardhi tunayo kubwa tuu...
 
Back
Top Bottom