Baadhi ya marekebisho ya kodi, Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/2021

Baadhi ya marekebisho ya kodi, Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/2021

Nchi ya kilimo hii wangetoa Kodi zote kwa bidhaa Kama matrekta na vifaa vyake wapate mapato mengi kwa wakulima wanapouza mazao nje kuliko kukabana kuanzia mwanzo watu wanaendelea kulima kienyeji wakati ardhi tunayo kubwa tuu...
Labda wakubwa hilo wazo halijawapitia,,😃😃,ujue wanakazi nyingi sana,sometimes wanachoka
 
Drone Camera

Hapana, kuna tofauti kubwa baada ya muda.

Kumbuka, ongezeko la mshahara litaakisiwa kwenye makato na michango ya kisheria ya mfanyakazi na mwajiri. Punguzo la kodi litaongeza kipato Halisi (net income) cha mfanyakazi lakini hakitabadili kiwango cha makato mengine.

Hivyo, kuongeza mshahara kutaongeza makato na mfanyakazi na mwajiri ( Makato ya lazima yanapigiwa hesabu kwa aslilmia ya kipato ghafi) ambayo itapelekea kuongezeka kwa mafao pindi mfanyakazi anapoaachana na ajira kwa sababu zozote zile.
Ipi ina nafuu sasa kati ya kupunguza kodi na kuongeza mshahara
 
Ipi ina nafuu sasa kati ya kupunguza kodi na kuongeza mshahara

Kwa kuangalia ulinganifu wa muda mrefu, ongezeko la mshahara linampa ahueni mfanyakazi kwa kuongeza mafao. Punguzo la kodi (PAYE) halina athari zozote kwenye mafao.

Kwa muda mfupi, inabidi kuweka vigezo vya ulinganifu. Mfano punguzo kwa kodi la sasa kwa mfanyakazi anayepata mpaka 170k halina tofauti yeyote kwenye mapato yake, wakati anayepata 270k, yeye atapata ongezeko la asilimia 9 kwenye mapato ghafi. Sasa kwa anayepata 170k, ongezeko hata la asilimia moja kwake litampa nafuu na yule wa 270k, iwapo kiwango cha ongezeko la mshahara kitakuwa juu ya 11% basi atapata nafuu zaidi kwa kuongeza mshahara kuliko kupunguza Kodi,, lakini kinyume na hapo, nafuu ya kodi inamsaidia zaidi.

Vyovyote iwavyo, bora hata kidogo kuliko kutopata kabisa.
 
Back
Top Bottom