Baadhi ya marekebisho ya kodi, Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/2021

Nchi ya kilimo hii wangetoa Kodi zote kwa bidhaa Kama matrekta na vifaa vyake wapate mapato mengi kwa wakulima wanapouza mazao nje kuliko kukabana kuanzia mwanzo watu wanaendelea kulima kienyeji wakati ardhi tunayo kubwa tuu...
Labda wakubwa hilo wazo halijawapitia,,πŸ˜ƒπŸ˜ƒ,ujue wanakazi nyingi sana,sometimes wanachoka
 
Serikali Ya Wanyonge Imeona Mbali Sana
 
Ipi ina nafuu sasa kati ya kupunguza kodi na kuongeza mshahara
 
Ipi ina nafuu sasa kati ya kupunguza kodi na kuongeza mshahara

Kwa kuangalia ulinganifu wa muda mrefu, ongezeko la mshahara linampa ahueni mfanyakazi kwa kuongeza mafao. Punguzo la kodi (PAYE) halina athari zozote kwenye mafao.

Kwa muda mfupi, inabidi kuweka vigezo vya ulinganifu. Mfano punguzo kwa kodi la sasa kwa mfanyakazi anayepata mpaka 170k halina tofauti yeyote kwenye mapato yake, wakati anayepata 270k, yeye atapata ongezeko la asilimia 9 kwenye mapato ghafi. Sasa kwa anayepata 170k, ongezeko hata la asilimia moja kwake litampa nafuu na yule wa 270k, iwapo kiwango cha ongezeko la mshahara kitakuwa juu ya 11% basi atapata nafuu zaidi kwa kuongeza mshahara kuliko kupunguza Kodi,, lakini kinyume na hapo, nafuu ya kodi inamsaidia zaidi.

Vyovyote iwavyo, bora hata kidogo kuliko kutopata kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…