Baadhi ya matajiri wakubwa sio wasomi

Mao ze dong

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2012
Posts
941
Reaction score
1,012
Nimekua nikifuatilia baadhi ya watu wenye pesa duniani na waliokufa wakiwa matajiri wakubwa hawakuwahi kufika vyuo vikuu na wengine waliacha.

Bill Gates mmoja wa watu matajiri mwanzilish wa kampuni ya microsoft. Hakuwah kusoma chuo kikuu na alikua akifel but leo anasema wanaofaulu kwa ufaulu wa juu vyuo mbalimbali ndo wadfanyakaz katika kampuni yake.

Je unaitaj kuwa na elimu ya chuo kikuu kuanzisha kampuni kama billgates? Unaitaj kuwa na elim ili kuwa na pesa kama billgates?.

Steve jobs mwanzilish wa kampuni ta apple ambayo kwasasa ndo kampuni kubwa yenye bidhaa za bei gali kama ipad, iphone, nk. Steve alisoma chuo kwa miez 6 akaacha coz hakuona kama elimu ya chuo ingemsaidia kufikia mlengo yake miaka michache badae akaja na kampuni yake ya apple na komyuta ya bei gal zaid macbook yenye oparating system tofaut kabisa na windows.

Leo wasomi wangapi wameajiriwa ktk kampuni ya mtu ambaye aliacha chuo na kuingia mtaani? Henry Ford mtengenezaji wa magar ya Ford hajawai kufika chuo.

Marc zuckerberg mmiliki wa facebook hajawai kufika chuo kikuu but he is the one of the multimillionaire. Joam mwanzilish wa whatsapp hajawai kufika chuo kikuu bt now he is multimillionaire.

Na wengineo weng mnaowafaham. Mtazamo wangu ni kwamba haiitaj kuwa na degree kufanikiwa ila utakachokifanya ukiwa mtaani ndo kitakufanya ufanikiwe au la.

Izi sio enz za kuwadanganya watoto nenda shule soma kwa bidii upate degree utapata kaz na kuish maisha mazur. Ukimwambia mtoto ivyo unakosea. Ni bora kumuendeleza mtu katika kitu anachoweza kufanya.

Leo hii mtu wa mtaani yupo garage anaweza kutengeneza magar aina zote na ana uwezo mkubwa kifedha kuliko mtu aliyemaliza degree kwenye fani ya mechanics.


Tubadili mfumo wa kufikir kuhusu elimu na pesa.
 
Mkuu acha upotoshaji. Steve Jobs aliacha chuo kwa sababu ya gharama kubwa za masomo lakini hata hivyo alibadili kozi na kuanza kusomea calligraphy pale pale chuoni japo kwa utaratibu usiokuwa formal na usipotoshe hostoria ya apple.

Unamjua Woz? Unajua role yake apple? Kama ulikuwa hujui huyo ndiye architect behind Mac.

Hata Bill Gates inaonekana humjui vizuri nani aalikudanganya kuwa Bill hakusoma?

Bill alicha chuo kwa kuwa alipokuwa chuo aligundua kitu muhimu. He left university to pursue his dream.

Hakuacha tu. Nakushauri pia usome family history ya akina Gates ni akina nani. Hata Ford mwenyewe inaonekana humjui. Kama ulikuwa hujui Ford aliajiliwa kwanza kama engineer kwenye kampuni ya Edson Illuminating Company.

Nakushauri hata akina Mark jisomee mafanikio yaliwakuta wapi
Usimwache elimu aende zake.
 
Ujinga mnaolishana kwenye network marketing huo, hivi chukulia Bill Gates angekuwa hajasoma programing angekuwa alipo?
 
Wangevumbua hayo yaliyowapatia utajiri pasipo hata kuingia la kwanza ningekuelewa.
 
Elimu katika maisha n mhimu sana, inakusaidia kuwa na horizon kubwa katika kufikiri na uwezo waq kichwa kuchanganua na kubadili mfumo wa kufikir.

kufikir walofanikiwa hawakusoma n uzembe wa kufikiri na ni utafutaji wa short cut kufikia mafanikio. hakuna shortcut kufikia malengo vngnevyo uwe fisadi, uibie wengne kujineemesha mwenyewe.
 
Ujinga mnaolishana kwenye network marketing huo, hivi chukulia Bill Gates angekuwa hajasoma programing angekuwa alipo?

Yaani hii atakuwa kamezeshwa huko watu washampiga ya kiingilio na yeye kalibeba tuu kalileta jf.
 

Mkuu yaani ingekuwa xul ningekwambia ur out of syllabus unacho ongea ni sahihi lakini sio kwa maisha ya bongo kaka.....na hata huo ushahidi wako ww ulie fanya utafiti umekusaidia nn umekuwa bilionere kama hao unao wataja o?

Angalia na mazingira ya nchi yetu haya ruhusu kufanya hichoo oky we mwanao usimpeleke xul uone kama co kila cku utakuww unaitwa police....harafu hao unao wataja ni wa chache sana ambao hata ukisikia speech zao pamoja na kufanikiwa huwezi sikia kuwa wanakataza au kushauri mtu asisome.

Sawa wao wenyewe watoto wao hata test tu wakifeli ni shidaaa

USHAURI WA KIPUUZI HATUPENDI
 
Umesema vyema mkuu General8, wasingepita japo darasa moja, wangeishia katika shughuli nyingine, hata fb isingepatikana.
 
Last edited by a moderator:
Kijana acha kudanganya watu wote hao uliotaja walienda chuo ila wali dropout baada ya kuona project wanazofanya ni muhimu zaidi na wanahitaji kudevote muda mwingi kuendelea.

Duh eti Zuckerberg hakuenda chuo? Wakati hiyo facebook yenyewe ilianzia kwa wanafunzi wa harvard pwkee ambapo yeye ndo alikua mwanafunzi? Kama vitabu husomi basi hata movie huangalii?
 
Ujinga mnaolishana kwenye network marketing huo, hivi chukulia Bill Gates angekuwa hajasoma programing angekuwa alipo?

Ujinga jutokusoma mada na kuelewa. Sijasema watu wasiende shule kama ni darasani we mwanafunz usiyeelewa tipic.

Nimejaribu kulinganisha uhusiano wa elimu na pesa watu waache kufikiri kuwa jusoma tu ndo njia pekee ya jupata pesa.
 
anachosema ni kweli ila angetolea mifano kwa tanzania ndio ingeleta maana zaidi kwa mfano, tanzania maghorofa yote mjini yanamilikiwa na watu ambao hawana degree.
 

Nakufananisha na mwanafunz mwenye mwandiko mzur darasani alaf anapata F. Coz hamna uhusiano kati ya mwandiko mzuri na kudaulu vizuri darasani maana madactar wote na miandiko yao wasingefka popote.

Vivyo hivyo hamna uhusiano wowote kati ya kusoma sana na kuwa na pesa nying. Mtu ana miaka 25 hana jaz yoyote lakini anataka aka reseat mtiani wa form four kwa kuzan kuwa hamna namna yoyote ya kutoka bila kupata elimu.

Tubadili mtazamo ila sijasema watoto wasiende shule
 
Umesema vyema mkuu General8, wasingepita japo darasa moja, wangeishia katika shughuli nyingine, hata fb isingepatikana.

Uongo ni dhambi jamani elimu kwenye huu ulimwengu ndo kila kitu, kwani hata hao unaosema eti hawakwenda chuo kikuu lakin shule walienda!
 
Last edited by a moderator:

Una elewa maana ya neno ELIMU KAKA?
 

Umemsahau Eric James Shigongo. Alifeli darasa la saba ila kwa sasa millionaire.
 

Ndio steve alisoma calligraphy lakini sio kama mwanafunz halali ns alisoma kwa mwaka mmoja kwa kujiiba na kuudhuria vipind.

Sijasema watu wote hao hawajasoma kabisa ila elimu niliyolenga ni elimu ya juu.

Wengi hawakumaliza vyuo vikuu. Mtazamo ni kutaka watu kutafakari watafanya nini kama amefeli na kushindwa kuendelea na chuo kuliko mtu kumaliza ujana aki reseat mitiani kama ndo njia pekee ya kufanikiwa.

Pia mtu anapomaliza chuo kuacha kitegemea vyeti kumtoa kimaisha bali kufikiri nje ya box.
 
na walianza kuchakarika wakiwa bado vijana....sasa unakuta jamaa ana miaka 50, ali-drop shule miaka 30 iliyopita eti bado ana ndoto ya kuwa kama Bill Gates! na statement yake, eti mbona Bill hakuwa na degree.

Utajiri unautengeneza mwenyewe!
 
acha uonga marck zuckerberg amefika chuo kikuu harvard. Sema aliacha mwaka wa pili alikua anaxoma computer science.

And ili uwe tajiri ni uwezo wako binafsi wa kiakilli hata mwenyewe nataka niwe zaid ya bakharesa now nina 18 years paka kufika 25 nitakua tayari ni multmillionaire and kabla cjavuka 30 malengo yangu yatakua tayari nimeshayatimiza, Our God Is Our Controler
 
Nadhani anamaanisha kufika Elimu ya chuo kikuu.

Ila elimu ni kutumia maarifa kutatua matatizo ktk jamii.unaweza ukawa std.7 ukaja na maarifa ya kukomboa jamii kwa muda mrefu, maana elimu nyingine ni 'technical' na 'practicals' na si 'theories'ingawa theories muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…