Kufuatia vita iliyoibuka kati ya Iran, Marekani na Israeli kumeibuka video mbalimbali kuhusu mashambulizi yaliyofanyika huko lakini nyingine si halisi bali zimetengenezwa kwa kutumia Teknolojia ya Akili Unde (AI).
- Tunachokijua
- JamiiCheck imefuatilia baadhi ya video zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kufuatia vita kati ya Iran, Israel na Marekani na kubaini kuwa baadhi ya hizo si halisi.
Baadhi ya video hizo ni inayodaiwa kuwa shambulizi katika uwanja wa ndege wa Dubai, Jengo la kifahali huko Bahrain pamoja na jengo la Burj khalifa.
Baada ya ufuatilia kupitia nyenzo za kidigitali za kubaini maudhui yaliyotengenezwa kwa Akili Unde ambazo zimebainisha kuwa picha hizo zimetengenezwa kwa AI.
Huu ni mfano mwingine ambao unaonesha namna matukio makubwa yanapoibuka yanavyopelekea Upotoshaji.