Baadhi ya Mawaziri Serikali ya Awamu ya Sita wamekuwa na Utajiri wa ghafla usio kifani

Hata kipindi cha dhalimu magu akina bashite, Sabaya, Kalemani, nk wakipata utajiri wa ghafla.
Mkuu kuwalalamikia hao walaji wa fedha za Umma ni kuwaonea bure. Wa kulaumiwa ni hawa wenye madaraka na mamlaka ya kuweka Idara ama Vitengo vya kupambana na hao watu unao watuhumu humu. Wenye Mamlaka ya kuunda Taasisi/Idara/Tume kama Takukuru, Maadili ya Viongozi, Takukuru Polisi, Usalama wa Taifa na vingine vinavyo fanana navyo. Vyombo hivi ndivyo vyenye wajibu wa kuhakikisha mambo haya hayapewi nafasi.
Aidha kama vyombo hivyo vipo na matukio hayo yapo na yana endelea kwa kasi, basi ni vyema VIKAFUTWA na watumishi WOTE waliopo kazini kufukuzwa kazi bila malipo, maana hawa kutimiza wajibu wao na hatimaye kuliangamiza Taifa.
 
Walisharuhusiwa na mkuu kula kwa urefu wa kamba zao, hakuna wa kuchunguzwa wala kufatiliwa , wanaofatiliwa ni akina yakhe wanaodunduliza mia mbili mia mbili
 
Sasa mtu anawaambia wale kwa urefu wa kamba zao, unategemea nini? Yani waziwazi Kiongozi wa nchi anaongea hivyo mbele ya vyombo vya habari, bila kujali chochote, bila kujali cheo chake! Tumepatikana Watanzania 😭
 
Hii inathibitishwa na maelezo ya Wabunge wenzao ambao hali zao ni ngumu kifedha kwa sasa. Mawaziri hao wamekuwa na tabia ya kugawa fedha ili Bajeti zao ziungwe mkono kwa mujibu wa maelezo ya mtoa taarifa kutoka Bungeni.
Yaani hao overpaid and underperforming wanaona kwamba hali zao ni ngumu kifedha ? Mwananchi kitaa asiyepata hata theluthi ya hio kwa miaka hata mitano aseme nini ?
 
"I have failed to reject the null hypothesis" Observation yako iko sahihi kabisa, hao uliowataja wana one thing in common (there is no significant difference between them) hahahahahahahahahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…