Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,122
- 5,104
Hii sio habari. Ni sawa na kusema mbwa kabwekea vibaka.
Tangu Azimio la Arusha lilipoondolewa kupisha Azimio la Zanzibar, hakuna awamu ya utawala wa CCM ambayo viongozi wakuu hawakujihusisha na wizi, ufisadi na rushwa bila kuchukuliwa hatua. Kusaka utajiri binafsi ndio lengo kuu la watawala wa CCM. Ni suala la makundi, mitandao na wateule katika mtindo wao wa kula kwa zamu, kutesa kwa zamu na kuimba kupokezana.
Tangu enzi zile, hakuna kiongozi wala kada wa CCM aliye kwenye moral high ground kiasi cha kuweza kuwafokea wenzie kuhusu ufisadi. Hivyo, "utajiri wa ghafla" wa baadhi ya viongozi wa CCM sio habari. Hakuna kipya kuhusu hilo. Tujadili mambo ya msingi.