Baadhi ya mihogo na samaki Coco Beach si salama, kuwa makini unapokula

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,147
Reaction score
20,080
Wakuu, habari za jumapili.

Hii mada ni kama tahadhari tu kwa watu wengine yasije kuwakuta kama yaliyonikuta jana.

Jana nilikua na maeneo ya masaki, baada ya shughuli zangu mdau mmoja akapendekeza tukale Coco Beach mihogo, basi tukajongea pale na kupata chakula.

Nilikula samaki na mihogo 2, wakuu toka jana jioni sitoki ndani, yaliyonikuta sio ya kawaida. Sasa nimejaribu ku share na jamaa zangu wengine kama 2 wanaoishi maeneo yale, nikaulizwa kama nilikula kwenye vibada vile vimepangana pale, nikasema ndio.

Jamaa wakanisisitiza kwamba nisirudie kula kwenye vile vibanda, wanakaangia chakula mafuta machafu, samaki wanakaangwa wanakaa hata wiki 2 kwenye fridge, kwa ujumla vile vibanda haijalishi ni cha nani ukila kula kwa tahadhari yako.

Wakuu ili yasije kuwakuta kama yaliyonikuta, nashauri kama hujawahi kwenda pale basi usiende na kama unaenda basi usije kusema hujatahadharishwa.

Sharing is caring wakuu.
 
Mimi nakula pale na familia yangu kila weekend kwa maisha yangu yote sijawahi kutana na changamoto yoyote mkuu
 
Wakuu ili yasije kuwakuta kama yaliyonikuta, nashauri kama hujawahi kwenda pale basi usiende na kama unaenda basi usije kusema hujatahadharishwa.πŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…