Baadhi ya mihogo na samaki Coco Beach si salama, kuwa makini unapokula

Kwa hiyo jana ulikula sehemu moja tu mkuu baada ya wewe kula ndio ukagundua kuwa wanatunza samaki kwa wiki mbili na pia wanatumia mafuta machafu sio..
Acha kuchafua biashara za watu. Kwa Mtaji upi anunue samaki akaange wa kukaa wiki 2 katika fridge?
Pita jioni uone wenye hela zao wanavyonunua hizo bidhaa bila madhara.
Tafuta sababu sahihi ila sio hiyo.
 
Acha kuchafua biashara za watu. Kwa Mtaji upi anunue samaki akaange wa kukaa wiki 2 katika fridge?
Pita jioni uone wenye hela zao wanavyonunua hizo bidhaa bila madhara.
Tafuta sababu sahihi ila sio hiyo.
Mkuu mbona unanivamia mzala nimeandika kwa code ili jamaa atembee tu watu miaka nenda rudi wanakula hapo yeye katoka zake huko leo anaandika uzi tusile mihogo hapo..
 
Tumbo lako siyo himilivu.
Litaweza kuhimili deni la taifa kweli?
 
mada yako hii haina mashiko..yaani wauza mihogo wawe zaidi ya kumi alafu ww ukala kwa mmoja wao ambae kwa siku hio kaamka vibaya kwenye biashara kwa maandalizi yake machafu..alafu uje humu kulaumu eti biashara za watu wote coco nzima hazifai kisa mjinga mmoja.! ww dili na huyo uliyefanya nae biashara na sio kuchafua na kuharibu biashara za wengine ambao hukufanya nao biashara..usilazimishe bahati mbaya iliyokukuta ww iwe ya kila mtu kwani kosa la siku moja la bahati mbaya la chakula cha siku hiyo kuchafuka haimaanishi ndio ipo hivyo miaka miaka mingi ya hao jamaa kupika mihogo hapo..kwa huyo mpuuzi mmoja sio haki ww kuwaona wauza mihogo zaidi ya kumi wengine coco nzima hawafai..acha roho mbaya kwa walio wengi kisa mpuuzi mmoja
 
Nimekula hiyo mihogo na Samaki wiki mbili zilizopita, tena nilikuwa na Vijana wangu, ambao walitokea kuipenda Kwa namna ilivyokuwa laini.

Hakuna aliyeugua tumbo wala kulalamika maumivu ya tumbo.

Huenda wewe binafsi ulikuwa na tatizo kabla hujaenda kula hiyo mihogo.
 
Hapana mkuu, samaki na mihogo haiwezi kua ni chakula kugeni kwangu mathalani kwa mtanzania yeyote.
Kimsingi Tanzania ni nchi iliyofeli kwa kila kitu hivyo watu wanaishi kijanja janja sana. Ni kila eneo. Iwe hospital, iwe polisi cases au mahakama. Kiufupi kila mtu analipia matokeo ya kukubali kutawaliwa na viongozi wa hovyo na wahuni. Hakuna short-cut hata kama tungeanzisha thread milioni moja kila siku. Lazima tuanze upya, katiba nzuri yenye kutoa ruksa kwa wananchi kuchagua viongozi wazuri na kuwawajibisha pale wanapokosea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…