k2206
JF-Expert Member
- Apr 22, 2018
- 702
- 705
Yaani umemaliza Kila kitu mkuu.
Mimi binafsi nimekuelewa Sana [emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106]
Sent using LEAGOO M12
Mimi binafsi nimekuelewa Sana [emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106]
1.) Kule ni nyumbani kwake kama wewe unavyoenda nyumbani kwako, ushauri unaotolewa ni kaa nyumbani kama huna ulazima wa kutoka, hata wewe unaweza kufuata ushauri ambao Rais anaufanya kwa vitendo, kazi anafanya kwa simu na video conferencing, kwani nesi yule akahudumie wagonjwa? HUNA HOJA
2.) Tunajua nchi nyingi kama ilivyo sisi hawajaweka lockdown ila wamechukua hatua za kueleweka kama sisi pia, tumefunga shule, tumekataza watu kutoka bila barakoa, tumehakikisha kuna ndoo za maji na sabuni kila baada ya mita tatu, tumetoa sharti la watu kuchukua TAKEAWAY na masharti mengine mengi ya social distancing, HUNA HOJA
3.) Lockdown ina maana tu kama itawekwa hadi wagonjwa wabaki 0, pasiwe na mgonjwa hata mmoja aliyebaki maana huyo mmoja atasababisha tena mlipuko, maana hata hapo mwanzo palianza na mgonjwa mmoja tu, ukisema watachukua tahadhari za kujikinga ili mlipuko usirudi nami nitakwambia kwanini wasingechukua tu hizo tahadhari toka mwanzo badala ya kuweka lockdown? Maana cases zilizopo wakati wanatoa lockdown ni nyingi kuliko wakati wanaweka lockdown, so lockdown ina mantiki ipi hapo? HUNA HOJA
4.) Kuna ubaya gani kufunga shule maana wanafunzi hawana uwezo wa kujisimamia kutekeleza tahadhari za kitaalam za social distancing, kunawa, uvaaji barako nk. Halafu kujificha maananyake nini? Mtu kukaa kwake ni kajificha, ulitaka afanye nini wakati wataalam wamesema kama huna ulazima wa kutoka basi usitoke, na yeye anafanya hivyo, hata wewe kama unaweza kufanya kazi kwa simu/ online bila kutoka basi usitoke, maana hayo ndio maagizo ya wataalam. HUNA HOJA.
5.) Mtu ambae kajifungia ndani kwake automatically amelockout kila mtu nje, sasa sijui unamaanisha nini, HUNA HOJA
6.) Unaposema hatuna lolote tulilofanya (ukiacha hiyo lockdown), unamaanisha nini? Haya yote yaliyofanyika including kufunga shule sio chochote? Hizi restrictions zote especially Dar we unaona si chochote? HUNA HOJA
7.) Kweli ujinga ni tatizo, lakini elimu ipo na inatolewa kila kona ili kuondoa ujinga na hatimae umasikini, lakini tofautisha ujinga na kupingana, watu kutofautiana mawazo ni jambo lakawaida, hivyo jitahidi kuonyesha uhalali wa mawazo dhidi ya mawazo ya mtu mwingine kwa kutumia hoja, jenga hoja na utasikikizwa, HUNA HOJA
Sent using LEAGOO M12