Usione watekaji ni wa chama pinzani wanaotekeleza mipango fichu ili kuipaka serikali matope na wanaitekeleza kwa siri kubwa kiasi ya kuwa hakuna ushahidi. Sasa serikali inakuwa ngumu kuwakamata kiushahidi .
Ila hawa G55 inawezekana wanawanalolijua ngojea kampeni huwenda kuna mambo yakajiri,
Nirudi Taifani - Bunge,vyombo vya ulinzi na Usalama na Serikali kuu.
Ila Serikali kama serikali inatakiwa kuja na majawabu ya matendo hayo ya utekwaji ambayo sasa yameeaza kusikika kila kona.
Hapa anaingia Waziri wa mambo ya ndani,anaingia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini na mwisho Wakuu wa JWTZ .
JWTZ wanapaswa kufuatilia na kupata ukweli na kama kuna ukiukwaji hii tabia ya kuteka waisimamishe ,kama wao ni Jeshi la wananchi kazi yao sio kulinda minyau tu ,je ikiwa kuna uvamizi wa siri hawa watekaji ni kutoka majeshi ya nchi jirani wametuvamia kiaina na wanatekeleza mauaji kiaina wao JWTZ watakuwa na faida gani ?
Hapa hapana siasa kusema jeshi linajiingiza katika siasa hapana.
Majeshi au mapolisi wana ndugu zao wengi tu uraiani ,sasa ikatokea ndugu baba mama wa walinzi hawa akatekwa akfanyiwa ya kufanyiwa .watafurahi watashangilia ?
Ni lini vyombo hivi vilikaa na kuyajadili haya kwa uwazi ? Mkosa kwa kosa lolote lile akamatwe mchana kweupe afikishwe kwenye vyombo vya sheria ndipo Rais au Chama kinaweza kujisifu kina mendeleo hakuna maendelea ikiwa wananchi wanaishi kwa hofu ,nasikia kuna nchi mkosa anapigiwa simu unatakiwa ufike kituo cha polisi unahitajika ,mtu anawambia wakaribu yake au kama atafuatana na mtu kuelekea huko kituoni. Na ikiwa atakaidi basi hapo ndipo ataenda kuchukuliwa mchana kweupe na ikiwa hapatikani tena hapo ndio inaingia hatua ya kumuwinda iwe usiku au mchana ila watu wote watakuwa weshakuwa na taarifa kuwa fulani anatafutwa na vyombo vya usalama.
Hatari iliopo kuna siku hawa wanaotekeleza vitendo hivi vya utekaji watakuja kutiwa mikononi na watawataja wanaowatuma unakuja kukuta ni viongozi wa CCM ,CCM hii inayosema imewaletea wananchi maendeleo.
Raisi Samia au yeyote yule anaposimama na kutetea kuwa wanafanya mazuri kuiendeleza nchi ,kwa kweli hili la utekwaji wa wananchi litakuwa kizingiti kikubwa sana mbele ya wananchi wapiga kura na mbele ya Mwenyezi Mungu ni kindende na kubwa huyu anaesimama na kusifu maendeleo ya serikali au chama chake jambo hili linamsugua na kumla ndani ya moyo ,inakuwa ni unafiki na kwa uislamu kuna alama za unafiki kuu tatu sijui kwa walokole.
Mkuu wa Nchi(Raisi) ajitahidi sana sana sana hili jambo alizime na likitokea awe mstari wa mbele kulifuatilia hata ikibidi kumfukuza Waziri ikiwa hatalifuatili Waziri amfukuze mkuu wa Polisi Mkuu wa polisi ikiwa hatolifuatilia kwa kina.
Tuchukulie lile la waliochukuliwa majuzi kwenye kesi ya mchochezi na kwenda kutupwa msituni ununio ,Mkuu wa Polis ilikuwa ni mhusika wa mwanzo ahoji kwa nini na kwa sababu gani ,gari za polisi zilionekana kuchukuwa watu pale kwenye viwanja vya mahakama kama walikuwa na haja ya kuwaondoa na kwenda kuwatupa mbali basi ilikuwa haina haja ya kuwapiga na kuwatia vilema au makovu. Wangeeenda kuwatupa tu ili kusafisha viwanja.
Kama Mkuu wa Polisi hakutolea maelezo basi ni Waziri wa mambo ya ndani angehiji sabab ya watu kwenda kutupwa wakiwa na majeraha ,vyombo vya ulinzi vya polisi mchana kweupe kila mtu aliona.
Kama waziri hakusema hapo ni Rais kumvuta ukosi Waziri hapo anamhoji na ikiwezekana kumfukuza au kumuondoa.
Inawezekana Serikali wao wanaona wanalinda Madaraka yao ya kuongoza nchi hawayajui yamjini ,Hivi ni visa au mambo kwa wapinzani walio ndani ya Serikali ambao wanakula njama kuichafua Serikali kwa vitendo vya aina hii vinavyowagusa raia ,matope yake yanamganda mpaka Rais bila ya yeye kujua pengine akiamini ili tuwepo serikalini lazima tuwwe na meno aina hii.
Panapo ichafua Serikali ni utekelezaji wake badala ya kuijenga Serikali inaibomoa ,ufuatiliaji na utekelezaji haviendani na uongozi bora wenye kujaribu kufuata sheria.
Vipi utasimama useme nchi imepiga hatua ya maendeleo maendeleo yanayoangushwa na vijisabu na vitendo vya kizembe kabisa , unachukuwa watu unaenda kuwatesa kisha unawatupa au kupotea ,tuchukulie watu wote waliopotea labda tuseme wapo sitini Serikali inashindwa kuwafunga au kuwaweka gerezani watu sitini ?
Sasa ukiwachukuwa ukawatesa ukawatia vilema kisha unaenda kuwatupa na kama amefariki unachoma hili halijengi linaweka kovu kwenye Chama tawala na donda ndugu kwa Raisi alieko madarakani.
Tanzania imebaki padogo sana kufikia maendeleo kamili hili la Utekaji na utekwaji CCM walimalize na kuachana nalo kabisa wasiiwache nafasi ya kulimaliza jambo hili kuja kufanywa na watu wengine au chama kingine. Kwa kweli itakuwa tumekula hasara.
CCM oyee.