Baadhi ya sababu zinazomfanya Magufuli aendelee kuwa Rais 2020-2025

Baadhi ya sababu zinazomfanya Magufuli aendelee kuwa Rais 2020-2025

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Nina imani Magufuli ataendelea kuwa rais si kwa sababu amefanya vema sana au ameutendea haki urais, ni kwa sababu zifuatazo:

1. Uchama Dola

Piga Ua CCM isiposhinda kihalali inashindishwa, hili ni kutokana na mifumo yote ya kidola,polis na mahakama kuwa upande wa CCM, dhambi hii ilifanyika mwaka 1992 kutoivunja CCM kuanza upya,

2. Uelewa mdogo wa watanzania wapiga kura wa vijijini
Bado watanzania wengi wa vijijini ni wana CCM na ndo wengi pia ndo wapiga kura kwa wingi, wanaaminu katika habari za kuwa kila Mpinzani wa CCM ni mawakala wa mabeberu,

3. Wapinzani wamejikita sana mtandaoni badala ya kuimarisha upinzani mtaani, halina ubishi,

4. Washindani wa JPM wanaweza wakawa wasiwe presidential material, ndo kina Tundu Lissu na Membe

5. Uoga wa wana CCM Wenye nia ya kugombea

6. Maendeleo anayofanya Magufuli kwa kiasi fulani

Ni mjinga pekee anayeweza kuwaza kuwa Magufuli mwisho wake ni 2020

Thathmini za mtandao zinatudanganya watumiaji wa Mitandao, kumbe mtaani bado jamaa anakubalika.

Britannica
 
Kwahiyo sisi tunaishi na kulala mitandaoni, unasahau kuwa sisi wa mitandaoni ndio hawa hawa wa mitaani, unachokiona mitandaoni ni reperesentation ya kilichoko mitaani.

Hapa mitandaoni tunaongea na kujadili tuliyokutana nayo mitaani acha kujidanganya.
 
Wapinzani huwa wanashinda chaguzi nyingi na wapiga kura wapo hata huko vijijini lakini kazi ipo kwenye kutangaza matokeo ndipo CCM huwafanyia uchakachuaji na tayari Tume na Polisi wana matokeo ya 2020 mifukoni wanasubiri muda na tarehe kumtangaza Magufuli kuwa ndiye Rais kisha atamteua Daud Maliyamungu Bashite kuwa Waziri ili kutokomeza mfumo wa vyama vingi na kurejesha mfumo wa chama kimoja kisha Magufuli kuwa Rais mpaka 2035
 
Ukitaka kujua Wapinzani wa CCM ni wengi ingia mitandaoni kwani Wapinzani humu mitandaoni wanajitolea bura kuikosoa CCM lakini wao CCM wanatumia mabilioni kumlipa Le mutuz kuwaajiri vijana wa kupambana kuitetea CCM na kibaya zaidi mwalimu wa Watetezi wa CCM mitandaoni ni Cyprian Musiba ambaye IQ yake ni ndogo kama ya panya.

Ndiyo maana watetezi wa CCM siku zote wanafeli mitandaoni hawana hoja wengi wamekariri vya kuliashwa na hao vilaza Le mutuz na Cyprian.
 
Mkuu utatoaje sababu namba 1, uchama dola na sababu namba 2,3 zinazo maanisha wapigaji kura wengi ni wa vijijini na wachache wenye mlengo wq kushoto ni wamezoea upinzai wa mitandaoni... hizi sababu mbili zinakinzana.
 
Kwani yeye ndiye aliyeanzisha utaratibu huo?
Japokuwa c yeye lkn Anaendelea kuutumia kwa kuwa ndio turufu pekee alonayo ya kuendelea kumuweka ikulu,
vinginevyo asubuhi tu atakuwa amejua kuwa watanzania hawanioendi mbali ya kujiona atakubalika tokana na anayoyafanya
 
Sio dhambi akiamua kupumzika 2020. Maana hawakumtendea haki kwa kumsukumizia huko. Mara nyingi amekuwa akisema hii kazi ngumu anatamani aongoze kwa kipindi kimoja
Siku nyingine akisukumizwa sio anabuluza bichwa anaingia bila kufikiri.
 
Nina imani Magufuli ataendelea kuwa rais si kwa sababu amefanya vema sana au maeutendea haki urais ni kwa sababu zifuatazo
1.Uchama Dola
Piga Ua CCM isiposhinda kihalali inashindishwa, hili ni kutokana na mifumo yote ya kidola,polis na mahakama kuwa upande wa CCM, dhambi hii ilifanyika mwaka 1992 kutoivunja CCM kuanza upya,
2.Uelewa mdogo wa watanzania wapiga kura wa vijijini, bado watanzania wengi wa vijijini ni wana CCM na ndo wengi pia ndo wapiga kura kwa wingi, wanaaminu katika habari za kuwa kila Mpinzani wa CCM ni mawakala wa mabeberu,

3.Wapinzani wamejikita sana mtandaoni badala ya kuimarisha upinzani mtaani, halina ubishi,
4.Washindani wa JPM wanaweza wakawa wasiwe presidential material, ndo kina Tundu Lissu, na Membe
5.Uoga wa wana CCM Wenye nia ya kugombea
6.Maendeleo anayofanya Magufuli kwa kiasi fulani

Ni mjinga pekee anayeweza kuwaza kuwa Magufuli mwisho wake ni 2020

Thathmini za mtandao zinatudanganya watumiaji wa Mitandao, kumbe mtaani bado jamaa anakubalika

Britannica
No research no right to speak!! JK 2010 alibaki kiujanjaujanja, Huyu nae kaingia si kwa kura ila kwa dola, usiwasingizie wa vijijini, matokeo kwa karatasi hupoteza ila dola inawabeba.

Muarobaini wa haya machakachuzi ni tume huru tuu, lakini wananchi wanafanya maamuzi ila tume nao wanatoa yao.
 
Wapinzani huwa wanashinda chaguzi nyingi na wapiga kura wapo hata huko vijijini lakini kazi ipo kwenye kutangaza matokeo ndipo CCM huwafanyia uchakachuaji na tayari Tume na Polisi wana matokeo ya 2020 mifukoni wanasubiri muda na tarehe kumtangaza Magufuli kuwa ndiye Rais kisha atamteua Daud Maliyamungu Bashite kuwa Waziri ili kutokomeza mfumo wa vyama vingi na kurejesha mfumo wa chama kimoja kisha Magufuli kuwa Rais mpaka 2035
Mimi imani na tume iliniishia Mrema aliposhindwa uchaguzi na Mkapa kuwa rais.
 
Back
Top Bottom