Baadhi ya teknoloiia zilizogunduliwa locally na katika jamii za nyumbani

Baadhi ya teknoloiia zilizogunduliwa locally na katika jamii za nyumbani

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2022
Posts
3,644
Reaction score
4,315
Jana nimekaa nikatafakari sana;

Hivi ni nani anayesemaga kwamba waafrika hawajagundua chochote cha maana?

Isije ikawa cha maana anachokiona yeye ni mawasiliano tu, sijui na kupaa au kurusha vitu angani😢

Kimsingi ugunduzi huwa unatakiwa kutatua changamoto ya watu husika kwanza kabla haujafika kimataifa. Na hilo ndio la maana kwao hao watu.

Tusimshadadie saana anayesisitiza kuwa teknolojia ni kumwagilia kwa drones, tukampondea yule aliyekuwa anachota maji kwa ndoo na sasa amegundua chemchemu akachimba mfereji. Kiukweli hata kama angeendelea kutumia ndoo kama ndiyo amegundua yeye apewe pongezi zake ametatua changamoto (ukame) zake bwana alaa!

Tukizungumzia mfano hii changamoto ya njaa. Baa la njaa lilikuwa likiumiza kaya na jamii nyingi tu za kiafrika kwa muda mrefu.

Kwa hiyo yeyote aliyegundua teknolojia ya kuhifadhi chakula huyo alikuwa mbabu jiniazi tena shujaa wa kijiji chake.

Sijui kuhusu mila za makabila mengine sana lakini hebu chukulia Wasukuma kama mfano;

Waligundua maparage

Wakagundua matoborwa

Na kuna hii kitu tunaita Mbutee hiiiiii😋

Na vingine vingi tu kama kukausha na kusaga msusa na mlenda halafu unakuja kupikwa na karanga (nimelisahau jina)

Mbogamboga ni nyingi tu mfano kuna nsansa pia
Adobe_Express_20231021_0832270_1.png

Jamii ikishakuwa na uhakika wa chakula bora, mlo kamili kwa mwaka wote hivi bado tena utajiuliza ni kwa nini Wasukuma wanazaliana sana?

Ni wakati sasa wa kuamka na kila jamii ikajifunze kwa jamii nyingine namna ya kukabili changamoto mbalimbali za kijamii ili tuimarishe uchumi wetu na afya zetu pia.

Ongezea na wewe teknolojia zilizopo katika jamii yako na zilivyotatuliwa ki locally tujivunie vya kwetu na vya kwenu(vyetu tu).
 
Hii mada pasipo kuingiza suala la mapenzi wachangiaji lazima wakimbie mkuu
 
Nikajuaaa labda ndege,magar,umeme......
Sasa ayooo si nature ndo imeaamuaaaa
 
Tukiachana na njaa ivii kuna jamii yenye kitu ambacho mtumiaji anakuwa na udadisi na uwezo wa kuchanganua mambo yaani akili.

Nataka kuongezea hizi locally made technology maana tunalo local problem ya UJINGA. Hivi je kilocally kwenu kuna jamii imewahi tatua tatizo la ujinga hasa kwa watoto? (Achana na mambo ya viboko)

Binafsi utafiti unaendelea hapa;

 
Watu wanabuni Ai powered self-driving cars and Automation huko sasa hiki Nini
 
Back
Top Bottom