jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 36,197
- 29,717
#7.0 Uingiliaji wakati wa majonzi na mshituko#
Katika kushughulikia masuala ya kijamii ya hali ya kushtua au
hisia kali kama vile ukatili, kutumia nguvu, matumizi ya dawa
za kulevya, ufuska, maneno machafu, waandishi wa habari
watawasilisha ukweli, maoni, picha na michoro kwa uangalifu
mkubwa na busara. Utekelezaji utafanywa kwa uangalifu na
busara. Kwa hali hiyo, waandishi wa habari:
i) Watajitambulisha na kupata idhini ya kuhoji kutoka kwa
mtendaji anayehusika kabla ya kuingia katika maeneo
yasiyokuwa ya wazi ya hospitali au taasisi nyingine.
ii) Wataepuka kutumia habari, picha na kutumia tena picha za
maktaba za matukio ya kifo na maradhi ya hatari ya watu,
kufufua majonzi miongoni mwa ndugu, jamaa na marafiki.
Hali kadhalika, watatumia taarifa kwa busara kuhusu
marehemu na sababu za kifo.
iii) Wasijinufaishe kwa utumiaji wa makusudi wa matukio ya
walioathiriwa na majonzi.