Baadhi ya wachezaji wa Tabora UTD kucheleweshewa leseni na TFF

Baadhi ya wachezaji wa Tabora UTD kucheleweshewa leseni na TFF

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
2,652
Reaction score
4,593
Mjumbe hauwawi. Nimeikuta sehemu wadau wa Tabora UTD wakiilalamikia TFF kuwa wamekuwa wakichelewesha leseni za wachezaji hasa wa kigeni kwa makusudi kwa maslahi yao.

Hili limeikumba Tabora UTD kwani wachezaji wao tegemezi mpaka muda huu hawajapewa leseni na TFF. Inawesemekana ni makusudi ili kuwapa uwepesi Simba kushinda mechi ya leo.

Ikumbukwe Tabora UTD walikuwa wamefungiwa na FIFA kufanya usajili kutokana na madeni na juzi kati ndio wamefunguliwa baada ya kulipa, lakini juhudi hizo hazionekanai kwa TFF. Timu imetoka kifungoni, kwa nini isipewe sapoti ya kutosha na TFF kama mlezi wa vilabu lakini wao hawana habari kutoa leseni za wachezaji kwa uharaka.

TFF wasome nyakati, mpira kwa sasa ni kazi kama kazi nyingine na ni chanzo cha mapato kwa hiyo wasitengeneze mazingira kwa vilabu pendwa viwe vinashinda tu vyenyewe wakati hata vilabu vidogo vimekuwa vikifanya usajili wa ushindani.
 
Za kutoka ndani ya Tabora UTD, wamehangaika kupata leseni siku tatu mfululizo lakini mpaka sasa TFF hawajatoa.

Ikumbukwe timu imefunguliwa usajili wiki iliyopita kwa hiyo walikuwa wanakimbizana na muda lakini juhudi zao zimegonga mwamba, ili Simba apate urahisi mechi ya leo.
Hii inakua mara ya pili sasa kwa Tabora .
 
Za kutoka ndani ya Tabora UTD, wamehangaika kupata leseni siku tatu mfululizo lakini mpaka sasa TFF hawajatoa.

Ikumbukwe timu imefunguliwa usajili wiki iliyopita kwa hiyo walikuwa wanakimbizana na muda lakini juhudi zao zimegonga mwamba, ili Simba apate urahisi mechi ya leo.
Jana imehairishwa mechi kati ya Namungo dhidi Fountain gate kisa maswala ya usajili lakini ni ajabu Tabora wao wameshindwa kuangaliwa katika hili.
 
Kama ni hivyo hii match ihairishwe kama ilivyokuwa match ya Namungo hapo saa moja maana sababu ni zile zile tuu.
 
Naangalia hapa mechi ya KEN GOLD SPORT vs SINGIDA BIG STARS

yaan TIMU ZOTE HAZINA UWEZO WA KUPIGA PASI 5 MFULULIZO

YAAN butua butua nyingi sanaa yaan kwa mtindo huu TIMU ZA KUTOA UPINZANI NA CHANGAMOTO HAZIFIKI 6 KWAKWELI
 
Kwa nini?
Yaani TFF icheleweshe usajili wa wachezaji wa Tabora ili Simba ishinde+
20240818_152524.jpg
 
Sijasema ili Simba ishinde. Nimesema ili Simba ipate urahisi wa mechi. Tofautisha kushinda na urahisi.

Muda ni msema ukweli. Tusubiri muda wa mechi tutaona.
Kwani Simba ndio waliwafungia tabora kusajili, mawazo yako ni Kama mtu hajielewi
 
Hata msimu uliopita TBR UNITED walicheza nane tu na AZAM akajipigia goli 8 na ndo yule FEi kubwa eti akawa mfungaji bora wa mechi na kutaka kuwa bora wa ligi.Hiyo mechi ya mchongo tu alifunga nne ! masuala haya utayakuta TZ tu.
Halafu yule Kasongo si mtu wa huko huko anashindwaje kuwasaidia ndugu zake ????
 
Hizi ndio figisu figisu zenyewe sasa. Kwani wewe hauna uzoefu na siasa za mpira wa Tanzania? Wabongo tunajuana.
Wewe lawama zako ulitakiwa uzielekeze tff na tabora kwa kuchelewa kukamilisha taratibu lakini Simba hausiki kwa chochote.
 
Wewe lawama zako ulitakiwa uzielekeze tff na tabora kwa kuchelewa kukamilisha taratibu lakini Simba hausiki kwa chochote.
Lawama ni kwa TFF kwa sababu ndiye mlezi mkuu wa vilabu vyotw kwa hiyo anatakiwa avipambanie vikue na siyo kuvidhoofisha.

Tabora UTD walikuwa wamefungiwa kwa sababu ya madeni. Wamefunguliwa wiki iliyopita na kuanza kukimbizana na usajili, hivyo TFF kama mlezi walitakiwa watambue hali ya Tabora UTD na wawe fasta kuwapa ushirikiano mana timu zinajiendesha kwa shida sana huku wao TFF wakikusanya pesa tu
 
Back
Top Bottom