Uchaguzi 2020 Baadhi ya wagombea washauriwe kusitisha kampeni, hawana jipya

Uchaguzi 2020 Baadhi ya wagombea washauriwe kusitisha kampeni, hawana jipya

Mkuu unateseka bure.
Rais ni Magufuli tu . Huyo mpiga pambio asubili sana mpaka afikishe miaka 80

Kwa wizi akisaidiwa na nyie?

Safari mumuase asijaribu.

Mkapa masononeko hadi aliyaweka kitabuni.

Tunataka uchaguzi ulio huru na wa haki si pungufu si zaidi.
 
Ungefanya jambo la maana kama ungemwambia Lissu asitishe kampeni maana iko wazi na hata yeye anajua kuwa hatoshinda. Watanzania bado tuna imani na Magufuli na tutamchagua tena

Bottom line tunataka uchaguzi ulio huru na wa haki.

Upande wa pili hamjatoa kauli hiyo. Yaonyesha nia ya kukwiba uchaguzi mngali nayo.

Tahadhari nyingi zimeitishwa. Safari hii ni tofauti. Mtanzania wa leo siyo wa jana. Tusije kulaumiana.
 
Kampeni zimefanya kukosa watu wa kutukumbusha kuhusu uhatari wa corona na umuhimu wa kufuata ushauri wa wataalamu jinsi ya kujikinga na corona,matokeo yake wote tumeingia mtego wa Magufuli na kuamini Tz hakuna corona matokeo yake tunajazana kwenye kampeni.

Sasa hivi neno "corona" limeshuka umaarufu na kuchukua nafasi hiyo "Nyomi/mafuriko",tunashindanisha mafuriko hatuogopi tena matatizo ya kupumua wala kujali kuhisu watu kufa kimyakimya.
 
Kuna watu walijiaminisha kuwa mgombea wao atakuwa anapunga mkono tu amemaliza, nina mashaka kama bado wanafikiria hivyo hivyo.

“Harlequin waved his wand and said, Hey Presto! And immediately they were married.”

Huo uchawi wa kupunga vifimbo na kumaliza kazi hapo hapo haupo tena duniani.
 
Mbona Tundu anaongea risasi bima na magufuri lakini hamjamchoka?

Waulize Maalim, Hussein au Shein kama ni hayo tu ndiyo aliyoongea alipowapitia huko.

Waulize kina jiwe, mpole mpole au bashiri kama wanakubaliana nawe kwenye hilo.

Ile mashine tofauti jombi!

"Heri Slaa achukue urais lakini si Lissu mbunge." Alisema JK.
 
Mleta Maada hujielewi Sasa Kama barabara imejengwa Mikoa ishirini Kila mkoa akifika lazima aongee barabara hiyo hapo oneni hiyo Hapo
Chadema hamna Cha kuonyesha Kila mnapoenda ndio maana mnaongelea visivyokuwepo tu


CCM kila tuendapo tutaongea ununuzi wa Ndege kila mkoa wenye uwanja wa Ndege tutaongea sababu zinaenda

Kila kijiji chenye umeme tutaongea umeme tuliopeleka

Zahanati kila tulipojenga tutaongea kuwa hiyo Hapo

Hapo hamtutoi kwenye reli nyie bakini na vitu vyenu hewa sisi tinawaonyesha live tukivyofanya na kuwaomba watupe ridhaa tufanye zaidi

Nyie endeleeni na fix hewa zenu za ahadi hewa

Nyie Chadema endeleeni kuwalisha porojo zenu tukutane sanduku la kura October 28

Tukutane October 28 kwenye sanduku la kura lililo huru na la haki.

Sijui kwa nini mnaishia kusema "sanduku la kura" peke yake. Malizieni kabisa "lililo huru na la haki," nakazia.

Hamna jipya. Mliyosema mfululizo kwa miaka mitano siyo dili tena. Mmepoteza sifa kwani hamna jipya.

Barabara mlizojenga ni kama hizi?

Barabara ya Rusahunga Rusumo mtaji kwa wagombea

Haki na uhuru wetu mnadhani hatujui kuwa tumeporwa? Tuna usongo kinoma msituone hivi. Tunayemtaka ni huyu:

IMG_20200804_210728_515.jpg


Hata hivyo bottom ni uchaguzi huru na wa haki.

Hakwibi mtu uchaguzi safari hii!
 
Ushindi wa Magufuli utaletwa na jiji la Dsm. Hili jiji naona ccm wamelishika vilivyo, kila chaka na kila chocho unayokatiza unakutana na lipicha la Magufuli yaani kama vile hakuna wagombea wengine wa nafasi ya urais.

To my suprise tapeli mashuhuri bwana Gwajima amebandika hadi mabasi yake ya kusomba misukule wake mipicha picha ya kwake na ya msukuma mwenzake.
Mkuu iyo mipicha ni Tz nzima. Watu wanaenda kupigia kura wanayemuelewa sio kwa wingi wa picha
 
Tulieni kwanza JPM anajenga nchi.

Nyie endeleeni na maneno maneno.

JPM ni vitendo.
 
Corona: Ya Burundi ni somo tosha, hala hala majuto ni mjukuu

Corona: Ya Burundi ni somo tosha, hala hala majuto ni mjukuu

"Burundi, uchaguzi wao mkuu uliendelea kana kwamba hakukuwa na janga la ugonjwa. Michezo iliendelea kama kawaida, Ibada, masoko, nk na bila shaka hata mashule hayakutatizika.

Wenzetu walipo tayari wameshaonja joto ya jiwe. Mengine tunayoambiana kuhusiana na strokes nk, hizo zinabakia kuwa ni mbwembwe tu, ambazo aghalabu hapa kwetu hizo tunajua kuzicheza zaidi."


Lazima tukumbushane kuhusu hatari ya corona,huu uchaguzi wa mafuriko usitupumbaze tumeona yaliyotokea Burundi ni mfano tosha maisha ya watu ni muhimu kuliko hizi kampeni za mafuriko.
 
Tulieni kwanza JPM anajenga nchi.

Nyie endeleeni na maneno maneno.

JPM ni vitendo.
“In the land of the blind, the one eyed man isn’t a king but a thief. He will continue to rob us blind, loot and pillage everything until there is Nothing Left To Steal."

Kipangaspecial 2020
 
Kuna haja ya Mdahalo au wagombea wote wapewe nafasi kwenye kipindi kama kile cha dakika 45 za ITV
 
“In the land of the blind, the one eyed man isn’t a king but a thief. He will continue to rob us blind, loot and pillage everything until there is Nothing Left To Steal."

Kipangaspecial 2020
Ndio mnaanza na vingeleza vyeu, tukutane Oct 28.
 
Suala lolote la imani kazi kubwa ya viongozi ni kukumbushana. Biblia inakisiwa ipo hapa duniani zaidi ya miaka 2000 iliyopita na ina kumbushwa kumbushwa kila wakati kwa muda wote huu.

Sasa vitu vya miaka 5 au 10 iliyopita ndio inatakiwa vikumbushwe zaidi.
 
Ushindi wa Magufuli utaletwa na jiji la Dsm. Hili jiji naona ccm wamelishika vilivyo, kila chaka na kila chocho unayokatiza unakutana na lipicha la Magufuli yaani kama vile hakuna wagombea wengine wa nafasi ya urais.

To my suprise tapeli mashuhuri bwana Gwajima amebandika hadi mabasi yake ya kusomba misukule wake mipicha picha ya kwake na ya msukuma mwenzake.
Wengine posters TRA wanadai kodi, na ukibandika zinabanduliwa na green guard, sehemu zingine wananchi wanaogopa kuruhusu wagombea wabandike mabango ya vyama vya upinzani ili kukwepa kufuatiliwa na polisi au TRA kwenye biashara zao.

Tumekabidhi nchi kwa washamba na limbukeni wa madaraka.
 
Kuna haja ya Mdahalo au wagombea wote wapewe nafasi kwenye kipindi kama kile cha dakika 45 za ITV
Haina haja hiyo,2015 mgombea wa ukawa alikuwa hazidi hata dk 5 za kuongea kwenye kampeni zake ila bado watanzania wakampa kura za kutosha. Hivyo sidhani kama kuna umuhimu wa midahalo ya wagombea urais kwa Tanzania.
 
Back
Top Bottom